Mahekalu ya maaskofu kufuru

Mahekalu ya maaskofu kufuru

Kupata mali siyo dhambi maana neno lanena Utafuteni kwanza Ufalme wa Mungu na mengine yote mtazidishiwa.
Na wala umaskini siyo utakatifu.Vipi hebu tupe na data za Mashehe.
 
Kama wana Devote their life time.. entire day kuhudumia kanisa kupunguza vibaka,wazinzi na kufundisha watu kumjua Mungu, they Deserve More than that...

Anayeona ni rahisi kukusanya sadaka za waumini aanzishe kanisa lake aone kama atafikisha hata waumini kumi.
 
Kupata mali siyo dhambi maana neno lanena Utafuteni kwanza Ufalme wa Mungu na mengine yote mtazidishiwa.
Na wala umaskini siyo utakatifu.Vipi hebu tupe na data za Mashehe.
Matayo 19:23-24

Hatari Za Utajiri

23 Kisha Yesu akawaambia wanafunzi, "Nawaambieni kweli, itakuwa vigumu kwa mtu tajiri kuingia katika Ufalme wa mbinguni.24 Tena nawaambieni, ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano kuliko mtu tajiri kuingia katika Ufalme wa mbinguni."
cc MziziMkavu
 
Matayo 19:23-24

Hatari Za Utajiri

23 Kisha Yesu akawaambia wanafunzi, "Nawaambieni kweli, itakuwa vigumu kwa mtu tajiri kuingia katika Ufalme wa mbinguni.24 Tena nawaambieni, ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano kuliko mtu tajiri kuingia katika Ufalme wa mbinguni."

Hapa Yesu Kristo wa Nazarethi Bwana wa Mabwana na Mfalme wa Wafalme alimaanisha ni vigumu sana wenye kutegemea mali kuingia kwenye Ufalme wa Mungu.Mbona Ibrahimua likuwa tajiri wa fedha,dhahabu nk.,Mfalme Suelemani aliyekuwa tajiri na hatatokea tajiri kama huyo yeye hata vyombo vya kulia ilikuwa dhahabu.
 
Sasa Mnashangaa nini? Kwani Mlitaka Wachungaji wawe fukara? Kama Mnashangaa hizi nyumba vya kwawaida, mtasemaje mkiona Jumba la Pastor Allan Kiuna wa Jubilee Christian Centre Nairobi Kenya?

Mungu Wetu sii Masikini. Kwani hujui Mungu humheshimu mtu anaemtumikia? Sasa Mungu Akikuheshimu utakuaje Masikini? Hayo mafundisho kwamba Mtumishi wa Mungu anatakiwa kuwa Masikini sijui mumeyatoa wapi wakati hayapo katika Bibilia.

If anyone serves me, he must follow me; and where I am, there will my servant be also. If anyone serves me, the Father will honor him. John 12:26 ESV

here is the Link.
You will judge yourself
 
hivi yesu alikua tajiri?

Unadhani Mnazayo Kristo Yesu alikuwa lonya lonya?. Sema tu sifa za upako zilifunika utajiri wake tofauti na hawa wa sasa wanaishia kuonyesha majumba magari na mahekaru huku vitambi vikiwa mbele ka mimba ya panya badala ya kudhihirisha nguvu za Mungu. Yesu alikuwa anafunga na kuomba sana ndio maana hakuwa na kitambi ka hawa. Tena kudhihirisha ushua wake hadi samaki alitoa pesa wakalipa kodi hakuwa na shida na sadaka za masimango kutoka kwa watu. Nampenda sana Bwana wangu Yesu Kristo kila siku natamani kufanana naye ooh Hallelujah!.
 
Engeza na swali hili! Hivi Yesu alikuwa akicheza ngoma Kanisani?


Sent from my iPad using JamiiForums

Unasema kucheza ngoma tu kumbe humjui Mnazalayo alitwanga watu makonde hekaruni alipokuta wanafanya biashara hakaruni isivyo stahili na kupindua meza zao . Sasa kama alifanya haya sembuse kusakata sebene Takatifu?. We wacha tu tamani sana kumjua Mnazarayo achana na wanuka jasho.
 
Unadhani Mnazayo Kristo Yesu alikuwa lonya lonya?. Sema tu sifa za upako zilifunika utajiri wake tofauti na hawa wa sasa wanaishia kuonyesha majumba magari na mahekaru huku vitambi vikiwa mbele ka mimba ya panya badala ya kudhihirisha nguvu za Mungu. Yesu alikuwa anafunga na kuomba sana ndio maana hakuwa na kitambi ka hawa. Tena kudhihirisha ushua wake hadi samaki alitoa pesa wakalipa kodi hakuwa na shida na sadaka za masimango kutoka kwa watu. Nampenda sana Bwana wangu Yesu Kristo kila siku natamani kufanana naye ooh Hallelujah!.


Hawa jamaa unafikiri wanaelewa wao wanamjua Yesu ni yule wa kwenye picha ya maigizo tehetehe Yesu Kristo wa Nazarethi hakuhitaji cash maana alikuwa akiita chochote akitakacho kinatokea kwenye njaa akaomba samaki na mikate wakala maelfu mpaka kusaza,hakuhitaji meli maana juu ya maji alitembea,hakuhitaji ndege wala gari ndo maana ilipofika saa ya kwenda Mbinguni alipaa tu.
na ndiyo mwanaume pekee aliyekufa akafufuka na atarudi tena wengine wote udongo umeshawatafuna na hata mimi utanitafuna ila huyu mwanaume udongo wenyewe ulimtapika.
 
kwanza nani alisema utajiri ni dhambi? Utajiri sio dhambi na wala kua masikini haimaanishi wewe ndio una mjua Mungu kuliko Binadamu wote na wewe kua tajiri haimaanishi humjui Mungu na wala hutaki kusikia habari zake.. kuna madon kibao tu mjini na wana enda church kama kawa na kuna masikini waku tupwa hata mlango wa kanisa au msikiti hawa taki kujua uko wapi... Mungu achukii mtu kua tajiri so long as utajiri wako hau utumii kuwa dhalilisha watu, kuwa umiza watu, kuwa nyanyasa, kuwa toa uhai na mengineyo mengi.. kama hufanyi hivo trust me mwenyezi Mungu kila kukicha ata kumwagia mi hela tu..sasa wewe masikini unae shinda kwa waganga kuroga watu kisa wame kuzidi maendeleo badala ufanye kazi na wewe utoke uta endelea kua masikini tu..... mimi bwana nime soma Arusha na mbaya zaidi nime kaa hostel karibu na kituo cha redio cha (Nabii Geordavie ) kwa jinsi nilivo sikia kwa wazawa wa Arusha huyu ni babake mzazi kabisa wa (Nisher ) yes Nisher yule video director mnae mjua nyie bongo. Kwao na nisher ni arusha na kuna time alihojiwa na radio ya watu akasema babake ni mchungaji na anamiliki kituo cha redio. Mpaka hapa napata prove. Sasa huyu (Nabii Geodarvie) bwana kwanza alikua akipita barabarani lazima awe na msafara afu gari zake zote nyeusi zime pigwa full light yani kama wewe ni mgeni arusha uka bahatika kukutana na msafara wake wakienda church asubui unaweza uka hisi ni kiongozi gani wa kimataifa ame kuja arusha? Manake hio barabara duuu! Watu full kukaa pembezoni wana shangaa mi mwenyewe nili shangaa. Zamani nilikua na sikia kutoka kwa watu wa arusha kua alikua ana sindikizwa na polisi...
 
Tunasema ni mahekalu kwa sababu hakuna kati ya waumini wao wana nyumba za hadhi kama za kwao. Mbaya zaidi Mch Lwakatare kajenga hekalu lake kwenye mdomo wa mto unapoingia baharini. Wizara ya ardhi na NEMC walipotaka kuibomoa kakimbilia mahakamani. Hakusimamisha ujenzi hadi amemaliza na kuhamia! Sasa sijui serikali inaogopa watu wa dini au vipi maana wale wengine waliojenga pwani visivyo walibomolewa. Serikali haina dini na mtu yeyote akivunja sheria ashughulikiwe ipasavyo.

Ufahamu mwema huleta upendeleo.
 
Ahahahaa..Nimependa sana bendela ya nyumba ya Mtikila.... IDUMU TANGANYIKA..... kwani uienzi vema . Hamna cha bendela ya Tanzania.
 
Maisha ndio haya poteza muda wako kuangalia fulani kafanya hivi.Kama unaona ni mafisadi acha kutoa sadaka yako wewe na familia yako pamoja na ndugu na jamaa zako ili kusudi wakome
 
...LOOOH..!! nimeipenda sana hii, hakika Mungu wetu anabariki, hongereni maaskofu kwa kuonyesha kwa vitendo kazi za Mungu aliye hai...
 
Back
Top Bottom