Mahekalu ya maaskofu kufuru

Mahekalu ya maaskofu kufuru

Hapo umechukua mstari 1 na biblia haina mstari mmoja wa ufalme wa mbingu na utajiri wa dunia.Sababu mbinguni hawataingia maskini tuu bwana Mzizimkavu.Utateseka duniani na mbinguni pia huendendi.Ndiyo hivyo hivyo hayo mahekalu ya maaskofu sio kigezo cha kuwa watenda dhambi.Hapo unahukumu.
Toa na wewe katika Biblia Mstari unaonyesha Matajiri wanaweza kuingia ndani ya Ufalme wa Mungu uipinge hiyo Aya aliyosema Bwana Yesu ? Usipende tu kuropoka maneno wakati huna hata Elimu nayo nipe jibu toka ndani ya Biblia usinipe majibu ya kichwani mwako majibu ya kichwa mchungwa majibu yako hayanitoshelezi kabisa theki
 
Last edited by a moderator:
Wakati Mungu akisema kuhusu fungu la kumi, watumishi walikuwa wakijitolea kutembea huku na huku kueneza injili, kulikuwa hakuna mishahara wala posho, miaka hii wanakoti mafungu hayo hayo wakati wanasaini mishahara mikubwa, wanamkosea Mungu, ni heri waseme fungu la kumi liende kwa yatima na wasiojiweza.

ETI? NI WAPI ILIANDIKWA KWAMBA BWANA YESU ALIKUSANYA SADAKA NA FUNGU LA KUMI AKACHUKUA?
WAPI?
WAPI?
:embarrassed::embarrassed::embarrassed:
 
Toa na wewe katika Biblia Mstari unaonyesha Matajiri wanaweza kuingia ndani ya Ufalme wa Mungu uipinge hiyo Aya aliyosema Bwana Yesu ? Usipende tu kuropoka maneno wakati huna hata Elimu nayo nipe jibu toka ndani ya Biblia usinipe majibu ya kichwani mwako majibu ya kichwa mchungwa majibu yako hayanitoshelezi kabisa theki
Tatizo hapana sio tatizo mtazamo wewe sio mkristo ndio maana uwelewa wako wa biblia sio mpana Hata mimi sijui hata aya moja ya quran kwa hiyo kuhoji lazima nitachapia.Ila kwenye huo mstari kasome toka mwanzo wa habari ujue kwa nini Yesu alisema matajiri ni ngumu kuingia ufalme wa mbingu.Ndio maana nikakwambia usihukumu sio kazi yako pia.Hayo mahekalu kuwa nayo sio kigezo kwamba ni watenda dhambi.
 
Haya Oneni "Kitofali" cha Pastor Allan Kyuna wa Jubilee Christian Centre- Nairobi Kenya. Wenye Wivu wajipege Mtama

right side
2.jpg

left side
1.jpg

back side
10.jpg

Front Side
12.jpg
 
wakati mungu akisema kuhusu fungu la kumi, watumishi walikuwa wakijitolea kutembea huku na huku kueneza injili, kulikuwa hakuna mishahara wala posho, miaka hii wanakoti mafungu hayo hayo wakati wanasaini mishahara mikubwa, wanamkosea mungu, ni heri waseme fungu la kumi liende kwa yatima na wasiojiweza.

umenena vyema mtumishi
 
Tatizo hapana sio tatizo mtazamo wewe sio mkristo ndio maana uwelewa wako wa biblia sio mpana Hata mimi sijui hata aya moja ya quran kwa hiyo kuhoji lazima nitachapia.Ila kwenye huo mstari kasome toka mwanzo wa habari ujue kwa nini Yesu alisema matajiri ni ngumu kuingia ufalme wa mbingu.Ndio maana nikakwambia usihukumu sio kazi yako pia.Hayo mahekalu kuwa nayo sio kigezo kwamba ni watenda dhambi.
Kwa usemi wa Bwana Yesu Kristo Matajiri hawawezi kuingia Ufalme wa Mbinguni kwa sababu zake kuwa Matajiri sio Rahisi kuingia Peponi.Masikini anaweza kuingia peponi lakini sio matajiri ndugu jaribu kumuelewa ni kwanini Bwana Yesu alisema hivyo? Ni fumbo hilo jaribu kulifumbuwa.
 
Ule mstari ni mfano wa jinsi ya kwanini matajiri ni vigumu kuingia mbinguni.Na pale sio sababu ya utajiri aliokuwa nao ila pale ni Moyo wa yule tajiri alivyokuwa amewekeza kwenye mali.Hata hao maaskofu usipime kwa mahekalu sababu mimi siombi mungu niwe maskini ila naomba utajiri.Ndio maana kila mtu anawajibika ila chunga sana moyo wako.Mfano Ayubu alikuwa tajiri sana ila moyo wake haukuwa kwenye mali.Hata alipojaribiwa hakusononeka.
Point ni usihukumu kwa kuangalia kwa macho.
 
Ninakuacha na Ubishi wako wa Kilokole mimi huwa sipendi kushinda na mambo ya kidini wakati ushahidi upo wazi wewe unanitolea ushahidi wako wa kichwani toa kwenye Biblia nipate kuona usilete ushahidi wa uongo wakati kitabu cha Biblia kipo wazi au hujuwi kusoma nikusomee vizuri?
 
Hahaha umeng'ang'ania nikupe mistari.Tatizo upo upande wa pili ndio maana tunakuwa hatuelewani wewe unaisoma biblia kama kitabu kingine cha ziada.
 
Hahaha umeng'ang'ania nikupe mistari.Tatizo upo upande wa pili ndio maana tunakuwa hatuelewani wewe unaisoma biblia kama kitabu kingine cha ziada.
Tatizo wewe kitabu chako lakini hukielewi wewe unacho zaidi Bwana YESU mtoto wa Mungu au Mungu mwenyewe Muamini Bwana YESU utaokoka basi hakuna zaidi ya kuelewa hivyo. Na ndivyo mnavyo fundishwa nyinyi Makanisani hakuna maswali wala majibu. Ninakuacha kama ulivyo Ukitaka kuongoka nitafute mimi nikuonyeshe njia ya kuongoka la kama hutaki kuongoka ninakuacha kama ulivyo asante.
 
Mbona hizo ni nyumba za kawaida kabisa kulingana na hadhi yao? Unatataka waishi katika nyumba za nyasi?

Huyu mtoa mada hajajipanga mbona hayo magorofa unayosema mengine yamekaa kama magofuu? Sijaona lakumfanya mtu anaepita barabarani asimame na kushangaa japo kuwa mm sina yakawaida saana.
 
Kuna mwingine anaitwa TB joshua nae ni company moja na hawa jamaa!
 
Ngoja wale maisha bana ilimradi hawamkwapui mtu njiani bali watu kutoa kwa hiari yao...
 
Bible ililetwa na jahaz ila sio la mzee yusuph ila makuhan wakuu waliwakuta na baadh yao walikuwa hawaingiliki kwa sound za mudy wala isa maria na mbona wenyewe walielewa na kukir ya kuwa ahimidiwe WA PEKEE ALIYEUMBA BARA LA AFRIKA kwa sababu walikuta vtabu na maandishi halali ambayo ukiyafuata na kuyaelewa pepo njia nyeupe wacha usumbufu wa kijinga cjui kutumia simu ili kuongea na mtu wa bukoba kwan saut yako haiwez fika mbona hapo karibu2 au we unazan mbu chakula chake damu?huko ndo kushndwa kwa hayo maneno yenu mzaniayo kuwa ya god kumbe dog kwa mana kihalisia yatakiwa kama kweli yana ukwel wahubiriwe sisimizi ili waache kushinda kwenye makopo yetu ya sukari alafu bnadamu ndo awe wa mwisho kuhubiriwa sio kutoka kwenye ibada kuwai kununua dudu kiler ili kuzuia mbao zisiliwe na wadudu hapo ndo kushindwa kwa uislajm na ukristo kunapoonekana wazi,ila c kosa letu isipokuwa tulifichwa na hao waloleta bible kwa kushirikiana na wapumbavu wachache walioamua kuyasaliti maandiko yetu ambayo yalikuwa na nguvu kubwa kulinganisha na ya wazungu na hao wazee wa kujitoa muhanga
 
Stori: Jelard Lucas na Makongoro Oging

MTU akifanya jambo la kupita kawaida lakini zuri watu husema amekufuru, yaani amefanya kitu kizuri! Imezoeleka hivyo. Sasa kauli hiyo imekuja baada ya Uwazi kufanya uchunguzi wa kina na kuyabaini mahekalu ya maaskofu wa Bongo kwamba nayo ni kufuru!

attachment.php

Ghorofa analomiliki Mwingira.

Katika uchunguzi huo, Uwazi lilitumia muda wa wiki mbili na kubaini kwamba, watumishi hao wa Mungu wapo vizuri na lile neno wanalolihubiri kwamba, kwa Mungu kuna raha, kwa Mungu kuna maisha mazuri na mtu akiyataka ampokee Bwana!

Nabii Mwingira.
UCHUNGUZI ULIPOANZIA
Uchunguzi ulianzia kwa askofu mkuu au Nabii George David Geordavie wa Kanisa la Ngurumo ya Upako (N.Y.U) lenye maskani yake jijini Arusha ambapo yeye anadaiwa kuwa na jumba kubwa analoishi na familia yake ndani ya jiji hilo na eneo hilo kupewa jina la Mji wa Daudi. Huyu amewafunika wenzake kwa ubora wa mjengo na pia utajiri alionao.

attachment.php

Ghorofa la Gwajima.

Habari zinasema mjengo wake huo una mandhari ya kiikulu ukilinganisha na mahekalu ya watumishi wenzake ambao wametajwa kumiliki pia.

Kwa mujibu wa chanzo, mjengo wa nabii huyo aliyejizolea umaarufu kwa kuwa na mfumo wa kiutawala kama ule wa wanasiasa, unapatikana katika Kitongoji cha Njiro, Arusha.
attachment.php

Mchungaji Gwajima.

Sijawahi kuona askofu au nabii anamiliki jumba la kifahari kama lile, lile ghorofa la ofisi tu pia ni balaa. Tena basi ameweka ulinzi mkubwa sijawahi kuona. Nilibahatika kupata picha ya sebuleni kwake utadhani ikulu. Pia niliwahi kuiona ofisi yake jamani! Jamani! (chanzo kinashangaa).

OFISI ZAKE ANAZIITA STATE HOUSE

Chanzo kiliendelea kudai kuwa, ofisi za nabii huyo ni maarufu kwa jina la state house (ikulu) ambapo pia hapo analindwa kama enzi za akina Mfalme Daudi ndiyo maana hata sehemu anayoishi panaitwa Mji wa Daudi.

attachment.php

Ghorofa la Mchungaji Mtikila.

MBALI NA HEKALU

Kwa Nabii Geordavie, mbali na kumiliki utajiri ambao umewahi kuandikwa na gazeti hili siku za nyuma, lakini imebainika kwamba ana kituo cha redio kinachojulikana kwa jina Ngurumo ya Upako FM chenye makao yake jijini Arusha.

MAHEKALU YA WENZAKE

Nyumba za maaskofu wengine ambao walizukiwa na Uwazi ni ile ya Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Nabii Josephat Mwingira wa Kanisa la Efatha Ministry, Askofu Zakary Kakobe wa Kanisa la Zakary Kakobe International Ministry (zamani Full Gospel Bible Fellowship F.G.B.F).

attachment.php

Mchungaji Mtikila.

Maaskofu wengine ni Lusekelo Anthony Mzee wa Upako wa Kanisa la Maombezi (G.R.C) Ubungo -Kibangu, Mchungaji Kiongozi Getrude Rwakatare wa Kanisa la Assemblies of God Mikocheni B na Mchungaji Christopher Mtikila wa Kanisa la Salvation Church, wanatajwa kumiliki mahekalu mazuri nchini.

MCHUNGAJI GWAJIMA

Mchungaji Gwajima hakamatiki kama Geordavie, kwani anatajwa kuwa na mjengo wenye ghorofa nne maeneo ya Salasala jijini Dar. Gwajima maarufu kwa kurudisha misukule, pia anamiliki magari ya kifahari achilia mbali mabasi yanayotumika kubeba waumini wake kwenda kanisani Kawe jijini Dar.

attachment.php

Ghorofa la Geordavie.
NABII MWINGIRA
Licha ya kuandamwa na skendo, Nabii Mwingira anamiliki jumba la ghorofa moja Mikocheni B, jijini Dar. Ina ulinzi balaa. Eneo kubwa la jumba hilo ni matumizi ya familia yake.

Pia Mwingira anamiliki Benki ya Efatha iliyopo Mwenge jijini Dar. Anatajwa kuwa miongoni mwa watumishi wa Mungu mabilionea sanjari na baadhi ya viwanja na mashamba anayomiliki.
MAMA RWAKATARE
Mama Rwakatare, wengi humwita Mbaya. Ni miongoni mwa watumishi wa Mungu waliofanikiwa kujenga nyumba mbili za kisasa, moja ipo Mikocheni B ikiwa na ghorofa moja na Mbezi, Dar yenye ghorofa moja.

attachment.php

Nabii Geordavie.
MCHUNGAJI MTIKILA
Mchungaji wa Kanisa la Salvation Church, Christopher Mtikila yeye anatajwa kumiliki hekalu moja maeneo ya Mikocheni B jijini Dar likiwa na ghorofa mbili.

MZEE WA UPAKO
Mzee wa Upako ni Mchungaji wa Kanisa la GRC, ni kama Mwingira tu, yeye anamiliki mjengo wa ghorofa moja uliopo Ubungo Kibangu jirani kabisa na kanisa lake.

Mchungaji huyo anatajwa kuwa miongoni mwa watumishi wa Mungu walio vizuri kimaisha. Mzee wa Upako aliwahi kula kiapo katika moja ya vyombo vya habari (jina kapuni) kuwa kwenye maisha yake haamini katika umaskini kwani umaskini siyo sifa nzuri.

Nyumba ya Askofu Kakobe.
ASKOFU KAKOBE
Askofu Kakobe (I.M) anatajwa kumiliki nyumba ya kawaida sana pale Mpakani B, Kijitonyama Dar. Nyumba yake haina ghorofa. Aliwahi kuburuzana mahakamani na baadhi ya waumini kwa madai ya hati miliki ya kanisa.

Jumamosi iliyopita waandishi wetu walifika nyumbani kwake na kubahatika kuzungumza na majirani ambao wengi walikuwa na swali moja ni kwa nini Kakobe hateremshi hekalu la kisasa ilihali fedha anayo?

attachment.php

Askofu Kakobe.
KUWAPATA ISHU
Miongoni mwa watu wagumu kupatikana na kuzungumza na wanahabari ni watumishi hao wa Mungu ambapo wote walipotafutwa kwa njia zote, simu na kufuatwa makanisani mwao hawakupatikana.

Kuna wakati Mchungaji Lusekelo aliwahi kuulizwa ni kwa nini hawapatikani, alisema hata Yesu alikuwa hapatikani kirahisi!!
Kumtumia Mungu Kuna faida
 
Back
Top Bottom