ng`wana ong`wa kulwa
JF-Expert Member
- Mar 14, 2013
- 2,420
- 1,752
hivi yesu alikua tajiri?
Mimi sijaon@ nyumba ya kutisha, za kawaida tu mbona
Matayo 19:23-24Kupata mali siyo dhambi maana neno lanena Utafuteni kwanza Ufalme wa Mungu na mengine yote mtazidishiwa.
Na wala umaskini siyo utakatifu.Vipi hebu tupe na data za Mashehe.
Matayo 19:23-24
Hatari Za Utajiri
23 Kisha Yesu akawaambia wanafunzi, "Nawaambieni kweli, itakuwa vigumu kwa mtu tajiri kuingia katika Ufalme wa mbinguni.24 Tena nawaambieni, ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano kuliko mtu tajiri kuingia katika Ufalme wa mbinguni."
hivi yesu alikua tajiri?
Engeza na swali hili! Hivi Yesu alikuwa akicheza ngoma Kanisani?
Sent from my iPad using JamiiForums
Unadhani Mnazayo Kristo Yesu alikuwa lonya lonya?. Sema tu sifa za upako zilifunika utajiri wake tofauti na hawa wa sasa wanaishia kuonyesha majumba magari na mahekaru huku vitambi vikiwa mbele ka mimba ya panya badala ya kudhihirisha nguvu za Mungu. Yesu alikuwa anafunga na kuomba sana ndio maana hakuwa na kitambi ka hawa. Tena kudhihirisha ushua wake hadi samaki alitoa pesa wakalipa kodi hakuwa na shida na sadaka za masimango kutoka kwa watu. Nampenda sana Bwana wangu Yesu Kristo kila siku natamani kufanana naye ooh Hallelujah!.
Tunasema ni mahekalu kwa sababu hakuna kati ya waumini wao wana nyumba za hadhi kama za kwao. Mbaya zaidi Mch Lwakatare kajenga hekalu lake kwenye mdomo wa mto unapoingia baharini. Wizara ya ardhi na NEMC walipotaka kuibomoa kakimbilia mahakamani. Hakusimamisha ujenzi hadi amemaliza na kuhamia! Sasa sijui serikali inaogopa watu wa dini au vipi maana wale wengine waliojenga pwani visivyo walibomolewa. Serikali haina dini na mtu yeyote akivunja sheria ashughulikiwe ipasavyo.
Nani tuungane tujenge kanisa?
Maisha ni ya hapa ni nani ajuaye ya huko juu?