Omwami, nakuita hilo jina maana uliniambia umetokea Kagera, hivyo aidha utakua Mhaya au Mnyambo ambao wana undugu na Waluhya wa Kenya akina
NairobiWalker wao hutumia hilo Omwami na nilikuta linatumika kwenu.
Anyway, nikija kwenye kauli yako, sidhani kama kuna Mtanzania asiyeijua Kibera, hili neno Kibera limeenea hadi vijijini Tanzania. Hutumiwa sana kuwapa 'feel good mentality' kila mnapohoji kwanini Kenya imeishinda Tanzania kiuchumi, huwa kitu cha kwanza cha kuwaliwaza kwamba Kenya kuna umaskini mwingi na Wakenya mamilioni wanaishi Kibera hivyo mnatulia na kuacha kuhoji zaidi.
Kuhusu ufuatiliaji wa masuala ya Tanzania, kuna idadi ya Wakenya wanaopenda nyimbo zenu, hilo nakiri, haswa Wakenya wa maeneo ya Pwani ambao wana undugu na Watanzania wa Pwani na Tanga. Kingine ambacho Wakenya wanakifahamu sana kutokea Tanzania ni uganga, maana Kenya kuna mabango mengi sana ya waganga wenu. Halafu Wakenya wanawafahamu sana Watanzania kwa kupenda kuomba omba maana ndugu zenu wamejaa kwenye pembezoni mwa barabara zetu wakiomba omba.
Hatimaye Wakenya wanawajua sana Watanzania wenye asili ya Kichagga maana hawa jamaa hujituma sana Kenya na ni wajasiria, wapo wengi kwa maelfu, ukienda sehemu inaitwa Gikomba utadhani upo Moshi maana ndio wengi hapo. Japo kuna wale wamewekeza hata kwenye soko la ujenzi, jirani yangu Mchagga amejenga apartments za nguvu.
Sasa hayo ndio tunayoyafahamu kwa sana kuhusu Tanzania, japo Wakenya wazee wanamjua sana Nyerere lakini sio kwa vijana. Labda Magufuli siku hizi maana amengazwa sana kwenye hilo la kutumbua na kubana matumizi. Zaidi ya hao labda kwa Mkenya kama mimi ambaye nimekatiza vijijini kwenu, nimeingia mitaani, nimesafiri wilaya na mikoa mingi sana huko hivyo nimekua na muda wa kufuatlia hata siasa zenu kwa kina.
Lakini ukiingia upande wa Tanzania, wengi mnafuatlia sana mambo ya Kenya, sijasema ni vibaya lakini ndio hali ilivyo. Binafsi nikiongea Kiswahili ni vigumu kughamua asili yangu kwa lafudhi, hivyo huwa nikijichanganya na Wabongo bila wao kunishtukia, halafu nawakuta kwenye vijiwe wakijadili Kenya hadi napata raha. Kuna maeneo mengi sana nilishawakuta mkijadili Kenya na Wakenya na siasa za Kenya, ila wengi huwa wanasifia na sio kuponda.
Kwanza nilikuta wengine wanabishana balaa kuhusu siasa za Kenya, na huwa sijitambulishi ila nawaskliza tu kimya kimya na kucheka kimoyo moyo.
Halafu kwenye runinga mara nyingi unakuta mpo kwenye Citizen ya Kenya ambayo ni maarufu sana huko.