MaHessy Na Gangsters

MaHessy Na Gangsters

kuna programme fulani niliondokea kuipenda sana iliyoitwa MEDICAL DETECTIVES...yani wale jamaa hutumia ujuzi wa hali ya juu sana kufata ushahidi katika crime scenes...sijui kama bado inapeperushwa...ni katika etv..pia ungemshauri afatilie story za crime kwenye listverse.com....wanaandika vizuri sana pia
hii programme ni ya zamani sana. hata mm nilikuwa nikiifuatilia enzi hizo. sijui kama bado inapeperushwa
 
The guy has set his device to capitalize every first letter of the word!
Yeah, I have realized that. But when was trying to read his initial post, I found myself distracted by the numerous caps within the text. It is as hard to read as when a long text is in all caps. I just couldnt read past the few lines.

So, I had to copy- paste that cluttered epistle into the word document, removed the caps, introduced the paragraphs....and the jamaa actually had interestings things to say contrary to my initial impression.
 
So, I had to copy- paste that cluttered epistle into the word document, removed the caps, introduced the paragraphs....

Man u did all that? [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] the guy owes you an apology[emoji28] [emoji28] [emoji28]
 
Guys Napenda Tu Kuandika Ivyo. Naona Kama Identity. Sorry Kama Nawaboa Nayo.
Nilikuwa na shauku kuhusu uraia wako jombaa lakini nimedhibitisha we mtz nilivoona tu umetumia neno nawaboa,wakenya hawalitumii neno hilo kamwe.Kwa sheng wanasema nawabooh,unabooh,mnabooh si kuboa.Sawa,mimi mwenyewe fan wa crime fiction vitabu lakini,si movie.Crime kule Eastlands ishakuwa ni fiction jombaa ni hatar si siri!Leo ukiona kwa fb Hessy wa Dar utaskia kwenye nyuz panya road mkuu kauwawa!
 
Sasa Why Are Guns That Easily Accesible Huko Kenya. Tena Kwa MaKids Hata Hawajamaliza School.
Guns are not that easily accessible as mobile phones in Kenya. Those kids obtain guns, not by buying them from stores. In fact, they do not even own them.

These kids upon being inducted into the criminal gangs, are provided these weapons by the gang leaders who themselves obtained these guns from some underground criminal organizations importing these weapons from countries such as Somalia and Sudan, where there is such an influx of small arms due to the raging comflicts in those places.
 
Sasa Why Are Guns That Easily Accesible Huko Kenya. Tena Kwa MaKids Hata Hawajamaliza School.

Maybe uchunguze borders za Kenya na South Sudan, Southern Ethiopia, Western Uganda and Somalia. Kenya imezungukwa na nchi nyingi ambazo zipo vitani au zina maeneo ambaza zina mrundiko wa silaha mikononi mwa raia. The only functional borders ni ya Tanzania na South Western Uganda.

Kwa kawaida maeneo kama haya, kuzuia silaha kuingia nchini ni kazi kweli kweli. Inaonesha state capacity ya Kenya as a nation ni nzuri kwa kuwa Kenya imekuwa na maendeleo muda huu wote ilhali majirani zake ni wa aina hii. Sio nchi nyingi huzingirwa na so much turmoil na zikabaki salama.

Ukifanya research kidogo utakuta kwamba kati ya nchi za Afrika Mashariki Kenya inakadiriwa kuwa na silaha 680,000 ndani ya mipaka yake. Gun deaths (Total homicides au vifo vinavyosababishwa na silaha hizo) ni 2,761. Ukilinganisha na nchi zingine za ukanda huu, Kenya ina silaha nyingi lakini vifo vinavyotokana na silaha hizo ni chache. Mfano Ethiopia ina silaha 320,000 na vifo 11,048 wakati Tanzania ina silaha 550,000 na vifo 6,071, Uganda idadi silaha ni 400,000 na vifo 3,753.

Nadhani sababu kubwa ya kuonekana kuwa Kenya ina gun problem ni aina ya uandishi wa habari. Kenyan news ziko a bit more sensational kwa hio mauaji/ukame etc kuliko her neighbors.
 
Gun deaths in Tanzania three times that in Kenya? How comes? I thot Tanzania is a very safe country, gun violence quite a rarity.
 
Maybe uchunguze borders za Kenya na South Sudan, Southern Ethiopia, Western Uganda and Somalia. Kenya imezungukwa na nchi nyingi ambazo zipo vitani au zina maeneo ambaza zina mrundiko wa silaha mikononi mwa raia. The only functional borders ni ya Tanzania na South Western Uganda.

Kwa kawaida maeneo kama haya, kuzuia silaha kuingia nchini ni kazi kweli kweli. Inaonesha state capacity ya Kenya as a nation ni nzuri kwa kuwa Kenya imekuwa na maendeleo muda huu wote ilhali majirani zake ni wa aina hii. Sio nchi nyingi huzingirwa na so much turmoil na zikabaki salama.

Ukifanya research kidogo utakuta kwamba kati ya nchi za Afrika Mashariki Kenya inakadiriwa kuwa na silaha 680,000 ndani ya mipaka yake. Gun deaths (Total homicides au vifo vinavyosababishwa na silaha hizo) ni 2,761. Ukilinganisha na nchi zingine za ukanda huu, Kenya ina silaha nyingi lakini vifo vinavyotokana na silaha hizo ni chache. Mfano Ethiopia ina silaha 320,000 na vifo 11,048 wakati Tanzania ina silaha 550,000 na vifo 6,071, Uganda idadi silaha ni 400,000 na vifo 3,753.

Nadhani sababu kubwa ya kuonekana kuwa Kenya ina gun problem ni aina ya uandishi wa habari. Kenyan news ziko a bit more sensational kwa hio mauaji/ukame etc kuliko her neighbors.

Hizo bunduki zinazohesabiwa ni zipi? Hata zile za maafisa wa usalama. Asante kwa data uliyoleta. Hili ni Jipya
 
Habari Wakenya. Mimi Ni M-Tz Na Sijawah Fika Kenya. Ila Kutokana Na Kupenda Kusoma Crime Stories And Maybe Because Am A Lawyer To Be.. Imenipelekea Kusoma Na Kufuatilia Sana Mambo Za Mafias And Criminals (Not Terrorists)But Wale Wasee Wanaoperate Within A Country Either Individually Or Wale Wako Kwa Gangs Or Organized Crimes Like Mafia ie Ndrangheta.
Sasa Nkawa So Insinuated Na Kenyan Crime News Nikisikia Tu Huwa Napenda Kufuatilia Na Kusoma. So From Mohamed Ali's Documentaries "Jambazi Sugu Wanugu" Kina Wacucu Na Yule Rasta Nimeangalia Pia Yule Officer Alienusurika Kufa Wakati Alikua Hot On Trails Za Robbers Nimesahau Jina Lake Na Pia Yule Officer Aliuliwa Allegedly To Be A Robber. Btw Napenda Sana Ile Nyimbo "Dunia Ina Mambo" Moha Alitumia Katika Izo Documentaries.
Sasa Ni Kuhusu Hizi Issue Za Hawa MaHessy Mara Wa Kayole Au Dandora Then Nikaona Hao Girls Wanasemwa Majambazi Wameuawa Very Young Na Ile Profile Allegedly Of Mwane(A Husband Of One Of Killed Girls) Akipost Kua Hamuogopi Hessy. If There Is One Thing That Makes Me Afraid Of Coming To Nairobi,Is Crime And Violence. Wasee Wa Kenya Mnachukuliaje Hawa MaHessy Wanaofanya Things We Only See In Indian Movies!!Maana Kukula Coppers Nje Nje Apo Nairobi. Mpaka Naanza Ogopa Unaweza Ukaja Naii Ukapatana Na Msupuu Kumbe Ako Kwa List Ya Hessy Na Ashapewa Mko Mmekaa Hivi Hessy Akakuunga Na Ww Ni Robber Ukala Copper. Wasee Mnipe Views Zenu Kuhusu Hii. Nawakilisha!!

Kwanza kabisa kama unataka kuwa wakili kama unavyosema, basi ni muhimu sana ukaanza kwa kurekebisha uandishi wako, matumizi ya herufi kubwa kwenye kila neno sio utaratibu unaoruhusiwa kifasaha.

Tukija kwenye mada husika, hayo mambo ya Hessy hayatendeki Nairobi yote, ni baadhi ya vituko vya uswazi. Binafsi nikiwa kijana hustler mjini kuna kipindi niliishi uswazi Nairobi na kuna askari mmoja alikua na hulka kama za huyu Hessy. Yeye alikua anawapa washukiwa nauli kwamba warudi kwao vijijini, na yeyote aliyekiuka aliishia kuuawa akiwa kwenye harakati za ujambazi.

Huyo polisi alikua kila akikuonya, anaanza michakato ya kukuwinda hadi pale atakukuta ukitenda uhalifu na atakuulia mbali bila kupepesa macho. Nakumbuka kipindi fulani alimuonya jamaa awache ujambazi na akampa nauli arudi kijijini, jamaa akakiuka na kuendelea na uhalifu, sasa askari akamuwinda bila kufanikiwa, japo aliendelea kusikia sifa za jamaa alivyokua anafanya ujambazi. Siku moja wazazi wake jamaa ambao walikua wanaishi mjini pia, wakamtembelea huyo askari na kumwomba asamehe mwana wao. Yeye akajibu kwamba yupo radhi kumsamehe ila waandae kitita cha hela za kumhonga na kwamba wakutane wote na mshukiwa ili waongee jinsi ya kusuluhisha, akawaomba waandae elfu hamsini za Kenya, kama zaidi ya milioni moja za Bongo.

Baada ya hapo wazazi wakakusanya hela na kumpa askari, na wakaita kikao kati yake na mshukiwa, walipokutana, jamaa aliwaskliza wote akiwa kimya, ghafla akanyanyuka na kuchomoa bastola na kumwulia mbali mshukiwa mbele ya wazazi wake. Halafu akarejesha hela zao na kuwaambia wazitumie katika kusafirisha maiti hadi kijijini ili wakamzike bila gharama zaidi.
Huyo askari tulikua tunampenda sana huko gheto, alikua komando wetu maana jamaa alikua na utashi wa kazi yake. Nakumbuka alivyokua anaamka mapema saa kumi za usiku na kujichanganya na wauza maziwa kitaa, akijifanya na yeye ni mchuuzi wa maziwa pia. Kwa mtindo huo alikua akiwaibukia majambazi kiulaini na kuwapa risasi za ghafla.

Mwisho wake ulifika siku alimpiga risasi mtoto wa kiongozi fulani, ambaye mwanaye alijiingiza kwenye uhalifu baada ya kuwa teja. Alihama kwao maeneo ya kifahali kule Karen na kuanza kuishi uswazi huku akiwa teja na kuhusika na uhalifu, baada ya askari komando wetu kumpiga risasi, wazazi wa jamaa wakacheza figisu figisu askari wetu akaishia rumande. Tuliandamana kwa fujo lakini ndio hivyo tena, hapakua na jinsi wala nini, kuna watu wasioguswa dunia hii.

Hivyo nikihitimisha, wapo maaskari kama huyo Hessy wasioangazwa kwenye vyombo vya habari na wanapendwa sana uswazi. Lakini sio kweli mlivyoaminishwa huko Tanzania eti ukija Kenya utakufa mara moja kwa kupigwa risasi.
 
Gun deaths in Tanzania three times that of Kenya? How comes? I thot Tanzania is a very safe country, gun violence quite a rarity.
Could be that other forms of violent crimes are more prevalent in Kenya. (Knives/Pangas/Clubs/arrows etc) which aren't covered here. This only covers guns. Security covers a wider scope that just gun homicide.
 
dude..you have really done ur homework...you know ur stuff....but mbona nikuulize, kwanini watz wanajua sana kuhusu Kenya? yaani mko obssessed ama nini? sikumbuki last time nilitaka kujua chochote kuhusu tz...pengine mambo ya juu juu tu...lakini nyie mnaweka effort kujua sana kuhusu kenya...mbona?

tunapenda umbea umbea utuzoeee tu
 
Maybe uchunguze borders za Kenya na South Sudan, Southern Ethiopia, Western Uganda and Somalia. Kenya imezungukwa na nchi nyingi ambazo zipo vitani au zina maeneo ambaza zina mrundiko wa silaha mikononi mwa raia. The only functional borders ni ya Tanzania na South Western Uganda.

Kwa kawaida maeneo kama haya, kuzuia silaha kuingia nchini ni kazi kweli kweli. Inaonesha state capacity ya Kenya as a nation ni nzuri kwa kuwa Kenya imekuwa na maendeleo muda huu wote ilhali majirani zake ni wa aina hii. Sio nchi nyingi huzingirwa na so much turmoil na zikabaki salama.

Ukifanya research kidogo utakuta kwamba kati ya nchi za Afrika Mashariki Kenya inakadiriwa kuwa na silaha 680,000 ndani ya mipaka yake. Gun deaths (Total homicides au vifo vinavyosababishwa na silaha hizo) ni 2,761. Ukilinganisha na nchi zingine za ukanda huu, Kenya ina silaha nyingi lakini vifo vinavyotokana na silaha hizo ni chache. Mfano Ethiopia ina silaha 320,000 na vifo 11,048 wakati Tanzania ina silaha 550,000 na vifo 6,071, Uganda idadi silaha ni 400,000 na vifo 3,753.

Nadhani sababu kubwa ya kuonekana kuwa Kenya ina gun problem ni aina ya uandishi wa habari. Kenyan news ziko a bit more sensational kwa hio mauaji/ukame etc kuliko her neighbors.

Hizo takwimu umetoa wapi? Chooni ama Kibera?
 
dude..you have really done ur homework...you know ur stuff....but mbona nikuulize, kwanini watz wanajua sana kuhusu Kenya? yaani mko obssessed ama nini? sikumbuki last time nilitaka kujua chochote kuhusu tz...pengine mambo ya juu juu tu...lakini nyie mnaweka effort kujua sana kuhusu kenya...mbona?
Wakenya waliopo Tanzania ni wengi kuliko watanzania waliopo Kenya ... hii inamaanisha kuwa wakenya wengi wanaijua Tanzania kuliko watanzania wanaoijua Kenya...

Kuna vipindi kama vya churchill live ambavyo comedians wake wengi huiongelea Tz na bado hujaiongelea nyimbo wanazozitumia...

tamthilia nyingi za wakenya zimeanza kufeature watanzania na pia angalia showbiz ya Kenya na Tanzania uone ni ipi inayoiathiri nyingine...

ukiangalia forums za wakenya kama JamiiForums.com ama reddit huwa hawajiangaishi na Rwanda na hata sudan.. ni Tz na somalia na mkijitahidi sana mtaiongelea Ethiopia ...ila mkija Jf huwa mnaigiza kuifuatilia SA ,nigeria na Egypt

Sasa kama wewe hujui lolote kuhusu Tanzania .....its your own probleme coz nina uhakika kuna watanzania wengi kama wewe wasiojua hata kuna Kibera
 
Omwami, nakuita hilo jina maana uliniambia umetokea Kagera, hivyo aidha utakua Mhaya au Mnyambo ambao wana undugu na Waluhya wa Kenya akina NairobiWalker wao hutumia hilo Omwami na nilikuta linatumika kwenu.

Anyway, nikija kwenye kauli yako, sidhani kama kuna Mtanzania asiyeijua Kibera, hili neno Kibera limeenea hadi vijijini Tanzania. Hutumiwa sana kuwapa 'feel good mentality' kila mnapohoji kwanini Kenya imeishinda Tanzania kiuchumi, huwa kitu cha kwanza cha kuwaliwaza kwamba Kenya kuna umaskini mwingi na Wakenya mamilioni wanaishi Kibera hivyo mnatulia na kuacha kuhoji zaidi.

Kuhusu ufuatiliaji wa masuala ya Tanzania, kuna idadi ya Wakenya wanaopenda nyimbo zenu, hilo nakiri, haswa Wakenya wa maeneo ya Pwani ambao wana undugu na Watanzania wa Pwani na Tanga. Kingine ambacho Wakenya wanakifahamu sana kutokea Tanzania ni uganga, maana Kenya kuna mabango mengi sana ya waganga wenu. Halafu Wakenya wanawafahamu sana Watanzania kwa kupenda kuomba omba maana ndugu zenu wamejaa kwenye pembezoni mwa barabara zetu wakiomba omba.
Hatimaye Wakenya wanawajua sana Watanzania wenye asili ya Kichagga maana hawa jamaa hujituma sana Kenya na ni wajasiria, wapo wengi kwa maelfu, ukienda sehemu inaitwa Gikomba utadhani upo Moshi maana ndio wengi hapo. Japo kuna wale wamewekeza hata kwenye soko la ujenzi, jirani yangu Mchagga amejenga apartments za nguvu.

Sasa hayo ndio tunayoyafahamu kwa sana kuhusu Tanzania, japo Wakenya wazee wanamjua sana Nyerere lakini sio kwa vijana. Labda Magufuli siku hizi maana amengazwa sana kwenye hilo la kutumbua na kubana matumizi. Zaidi ya hao labda kwa Mkenya kama mimi ambaye nimekatiza vijijini kwenu, nimeingia mitaani, nimesafiri wilaya na mikoa mingi sana huko hivyo nimekua na muda wa kufuatlia hata siasa zenu kwa kina.

Lakini ukiingia upande wa Tanzania, wengi mnafuatlia sana mambo ya Kenya, sijasema ni vibaya lakini ndio hali ilivyo. Binafsi nikiongea Kiswahili ni vigumu kughamua asili yangu kwa lafudhi, hivyo huwa nikijichanganya na Wabongo bila wao kunishtukia, halafu nawakuta kwenye vijiwe wakijadili Kenya hadi napata raha. Kuna maeneo mengi sana nilishawakuta mkijadili Kenya na Wakenya na siasa za Kenya, ila wengi huwa wanasifia na sio kuponda.
Kwanza nilikuta wengine wanabishana balaa kuhusu siasa za Kenya, na huwa sijitambulishi ila nawaskliza tu kimya kimya na kucheka kimoyo moyo.
Halafu kwenye runinga mara nyingi unakuta mpo kwenye Citizen ya Kenya ambayo ni maarufu sana huko.
 
Hahahaaaaaa sawa bhanaa yap ni muhaya ndio lakini wahaya ni group kubwa la watu hivyo huwezi kuunganisha dots kirahisi hivyo maana kuna wahaya wenye asili ya bunyoro Ug (ambapo ndipo inaaminika kama chimbuko) haswaa waziba NA wengine ni kama sisi tu tuliopo muleba ambao mchanganyiko wake huwezi kujua ni yupi ana origin ya Uganda ,Burundi ama Rwanda ... Si unajua mipaka ni ya wakoloni ila wazee wetu walikuwa NA mipaka yao

Kiukweli na kiuhalisia huwezi kuwakuta watanzania wa kawaida wakiiongelea Kenya na hawana hata habari na Kenya vs Tanzania ama GDP yetu kwa kuwa wanachojali ni huduma NA bei za bidhaa mbalimbali tu ...
Kitu kilichopo popular katika Tanzania ni entertainment industry ingawa kiukweli SIKU hizi wanafuatilia siasa toka uchaguzi wa 2015 ambayo inaathiri hata muziki wenyewe...
Kuna wakenya wanaojulikana kama Kenyatta ambalo jina lake limebebwa NA mzee jomo ambalo lina barabara nyingi nchini...
Mwingine labda ni huddah ,vera NA sauti Sol NA hawa ni kwa Instagram Lakini ukitoka huko hakuna anayewajua ....

Kibera sio popular in Tanzania kwa maana sehemu maarufu Tanzania nyingi ni za dar kama kariakoo ....
Kizazi cha watanzania kinachowajua wakenya ni cha WATU waliopita maana hata wakenya ni maarufu duniani kwa riadha lakini mchezo huo hauna washabiki na hata utalii wenu hauna nguvu kubwa maana watanzania wengi wanazungukwa na mbuga na fukwe ndo maana hata utalii wa ndani hauna nguvu....

Kuhusu citizen ni kweli tunaikubali maana IPO vizuri haswaa kwenye tamthilia kama zamani nilikuwa naipenda tahidi high and mother in law..hii ni kawaida kama wakenya mlivyokuwa mnaihusudu EATV au channel 5

Haya mambo mengine ni kama yapo jf tu ila ukitoka nje na kukutana NA watanzania halisi hupenda wageni na haswaa wajuao kiswahili ambao wengi ni wakenya
 
Mosi ,Juan Moses siyo mtanzania Juan Moses is an impostor. Pili, criminal gangs to tishio kubwa baadhi ya mitaa hadi kuwakosesha wananchi amani. Bila "summary dismissal" criminals gangs were taking over estates with impunity,maiming killing robbing innocent wananchi. Hanna jinsi zaidi ya kuwafagia. Watajuahawajui tu.
 
Hessy wa Kayole is doing a commandable job. Hessy superman wa Nairobi protecting the law abiding citizen.
 
Back
Top Bottom