- Source #1
- View Source #1
Wakuu hii ni kweli kuwa Mahinyila amesema vijana wa CHADEMA wanafanya mambo ya kihalifu, wakikamatwa wanataka chama kiseme wametekwa na watu wasiojulikana?
- Tunachokijua
- Deogratias Mahinyila ni Mwenyekiti wa baraza la vijana wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA (BAVICHA) Taifa. Mnamo Machi 4, 2025 akiwa na viongozi wengine wa baraza hilo alifanya mkutano na waandishi wa habari ukiwa na lengo la kuongelea hali ya usalama kwa vijana Tanzania, ikiwemo tukio la utekaji lililomkumba katibu mkuu wa BAVICHA mkoa wa Mwanza Amani Manengelo, Februari 14, 2025.
Madai
Kumekuwapo na taarifa inayosambazwa mtandaoni kuwa Mahinyila amesema vijana wa CHADEMA wanafanya mambo ya kihalifu, wakikamatwa wanataka chama kiseme wametekwa na watu wasiojulikana.
Uhalisia wa madai
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia maneno muhimu (Key Word Search) umebaini kuwa Taarifa hiyo Si ya Kweli, pia haikuchapishwa na Jambo TV.
Aidha kupitia mkutano wa Machi 04, 2025 na waandishi wa habari alikemea matukio ya utekaji kwa vijana nchini huku akizitaka mamlaka kuchukua hatua stahiki, vilevile Mahinyila hakutoa kauli hiyo kwenye mkutano huo.
JamiiCheck inakukumbusha kufanya uhakiki wa kila taarifa unayokutana nayo mtandaoni kwani kumekuwapo na machapisho mengi yakitumia machapisho ya vyombo mbalimbali vya habari mbalimbali vya habari. Tazama hapa, hapa, hapa na hapa, ni taarifa za upotoshaji zilizotumia utambulisho wa Jambo TV.