Mahita: Jeshi la Polisi halihitaji Waziri, linajiendesha lenyewe

Mahita: Jeshi la Polisi halihitaji Waziri, linajiendesha lenyewe

Aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP Mstaafu), Omar Mahita, ameshikilia msimamo wake wa kimfumo akisisitiza kuwa chombo hicho kina uwezo kamili wa kujiendesha chenyewe kiutendaji bila kuhitaji uwepo wa msimamizi wa kisiasa (Waziri).

Msimamo huo mzito wa Mahita umeibuka tena hivi karibuni wakati akizungumza kwenye mahojiano maalumu katika kipindi cha matangazo ya mtandaoni (Podcast), kauli ambayo imeamsha mjadala mpana miongoni mwa wataalamu wa sheria na mifumo ya utawala bora nchini.

Katika mahojiano hayo, kiongozi huyo wa zamani wa usalama alieleza kuwa Jeshi la Polisi lina mfumo dhabiti, wa kimדרgala na unaojitosheleza kuanzia ngazi ya Makao Makuu hadi chini, jambo linalofanya muundo wa sasa wa Wizara kuonekana kama kiunganishi kinachoweza kupunguzwa ili kuongeza ufanisi.

"Niliwaambia Jeshi la Polisi halihitaji Waziri, linajiendesha lenyewe," alikaririwa Mahita, akirejea mtazamo wake unaogusa kiini cha namna taasisi kuu za ulinzi na usalama zinavyopaswa kusimamiwa kijeshi na kiprofeshonali.

Wataalamu wa mifumo ya ulinzi na utawala waliofuatilia mahojiano hayo wamegawanyika katika mitazamo miwili; ambapo wanaounga mkono hoja ya Mahita wanasema ina tija katika kuongeza uhuru wa kiutendaji (Professional Autonomy) na kupunguza urasimu wa kimaamuzi mbele ya majanga au matukio ya kiusalama.

Hata hivyo, wachambuzi wa sheria za Katiba wanabainisha kuwa usimamizi wa kiraia (Civilian Oversight) unaofanywa na Waziri ni nguzo ya kidemokrasia. Wameeleza kuwa Waziri anasimama kama sauti ya wananchi bungeni kuwajibika kwa masuala ya bajeti na kisera, majukumu ambayo kiapo cha kijeshi hakiwezi kumruhusu IGP kuyajibu mbele ya wanasiasa.

Mjadala huo ulioibuliwa na Mahita kwenye Podcast unatajwa na wachambuzi wengi wa masuala ya kijamii kama fursa nzuri ya kitafiti na kisheria katika kuangalia mageuzi ya sekta ya usalama ili kuendana na kasi na mahitaji ya karne ya 21.View attachment 3596269
Hapa jamaa Kwa kujua au kutokujua anaanza kulitenga jeshi la polisi na wanasiasa

Kinachofuata lawama zote za mauaji na utekaji zinatupia jeshi la polisi kama Waziri alivyoanza kujitenga nalo Jana

Kwa hiyo wanasiasa baada kulitumia jeshi Hilo wanataka libebe lawama lenyewe
 
Naona kama huu ni mkakati maalum
 
Cha kumfanya kipo kaka ,hawa uwa kamfereji kanakatwa kimya kimya ikiwa mdomo utaendelea kuponza bichwa .

Anyway ,karibu kurasini uone vyeo vipya na vijana wadogo je kiapo kitazingatiwa au wataendelea kupiga viboko ?
Uapisho wa Kurasini ni lini? Mtaalika wanasiasa kama wageni rasmi?
 
"polisi akitishiwa kulengwa jiwe na raia mara moja polisi anatakiwa kushambulia kwa silaha aliyo nayo ambayo ni bunduki, Shut and kill"

THABIT KOMBO
1779949888571.jpg
 
Katambi anajibiwa kitaalam au anafundishwa kazi au siyo!!

Inamaana Camillius wambura aliliendesha jeshi la polisi kimedani bila siasa wala amri kutoka juu coz jeshi halina siasa au siyo!!!?

Yona akitoswa anatoswa na amri zake za October 29 kwa jeshi la polisi ama sivyo!!?

Nawaza na kuwazua nikijiandaa ku tick tena 2030 kunako majaaliwa ya baba mwenyezi Mungu!!
Kwani alichokiongea ni uongo?

IGP ameruhusiwa kutoa amri na tangazo la curfew kwa muongozo upi?

Ukifanikiwa kulijua hilo utafahamu na kujua October 29 akina nani waliua watu.

Ukimsikiliza hapa Khalifa utajua jeshi la policcm linafanyaje kazi na kwanini ni kituo pendwa cha kuilinda CCM na kwanini hawatakubali kirahisi litoke kwenye force kwenda service kama walivyofanya Kenya 2010, kimsingi kwa Tanzania policcm hawawajibiki kamwe kwa wananchi ila inahitaji jicho la tai kulijua hilo kama Khalifa alivyowafumbua macho waliokua hawajui

View: https://youtu.be/0tVb2dIEsTI?si=Tz7oerxKisc5YTh9
 
Uapisho wa Kurasini ni lini? Mtaalika wanasiasa kama wageni rasmi?
Uapisho upo leo ulianza saa 4:30 asubuhi na mgeni rasmi ni Amiri jeshi mkuu na raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ,dkt ,Samia suluhu Hassan akiwa ameambatana na wateule wake katika jeshi hilo hususani waziri wa mambo ya ndani pamoja na wasaidizi wengine.

Kaka umenikosea tutaalika kwa maana umenijumuisha mimi kuwepo huko ? Hapana nipo kama mwanafamilia tu sihusiki kualika wala kufuzu mafunzo hayo 🧐

Wanasiasa bado wapo katika teuzi za kisiasa kwaajili ya kuliongoza jeshi la polisi bado utaratibu haujabadilika mbali na kauli ile ya inspector generali wa jeshi la polisi mstaafu bwana Mahita
 
Sikusema kwa bahati mbaya.. Tunafahamiana Ila hujui kama ni Jr.! 😀
 
Kenya baada ya PEV 2007/08 walilifuta jeshi la polisi kutoka kuwa jeshi hadi huduma 2010 baada ya katiba mpya ndio maana wana Kenya Police Service na kaulimbiu yao ni "UTUMISHI KWA WOTE"

Na wana independent body ya kuichunguza polisi inaitwa Indepedent Policing Oversight Authority [IPOA ] iliyoundwa 2011 kuchunguza makosa yatokanayo na polisi.

Ndio maana hata raia anaweza kudeal na polisi Kenya vizuri tu maana ni watumishi wao .
 
Back
Top Bottom