The Next MP
Member
- Nov 15, 2023
- 71
- 119
Wana JF natumaini mko salama.
Naomba kushirikisha suala moja hapa, Katika kupambana kwangu na harakati za kujikwamua, nikafanikiwa kununua Kiwanja na kujenga nyumba.
Pia nikafungua biashara ya bidhaa za Jumla jumla za Dukani. Nilianza na Mtaji wa milioni 4, Baadae Mtaji ukafika mpaka milioni 30 ndani ya miaka mitatu, lakini nikaja nikapata changamoto mwaka Jana mpaka mwaka huu ya kumuuguza mama Mzazi mpaka nikampeleka India hospitali ya Appolo. Namshukuru Mungu alifanyiwa operation na mpaka Sasa anaendelea vizuri tumerudi TZ.
Nikajikuta nimepungua kibiashara yaani kuelekea kufilisika. Mpaka Sasa Kuna mtaji wa milioni 5 tu.
Nimejaribu kutafuta mikopo bank...wanahitaji hati lakini Mimi hati bado sijapata ndio ipo kwenye mchakato, hati za mauziano na za Halmashauri ndio ninazo.
Nilishaweka base ya wateja kubwa sana kiasi kwamba biashara ina mzunguko Mkubwa sana.
Binafsi nahitaji milioni 20 tu.
Kama Kuna mtu anaweza kunikopesha, tukatumia dhamana ya nyumba na akaweka riba au kama atataka tu-collaborate kwa mtaji huo wa 20m na kufanya makubaliano ya Faida basi Karibu sana tuzungumze.
Pia kama Kuna mtu anayekopesha na hana Masharti magumu sana unamfahamu naombeni ushauri.
Natanguliza Shukrani.