Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 10,509
- 16,734
Katika mkutano wake na waziri mkuu wa Lebanon,Nawaf Salam kiongozi wa mamlaka ya Palestina amewahimiza raia wake warudi kwenye ardhi zao huko Palestina ambayo sasa inaitwa Israel.
Malaki ya raia hao ni wale waliofukuzwa kwenye ardhi zao wakati wa kuanzishwa kwa taifa la Israel mwaka 1948.Wapalestina hao pamoja na vizazi vyao tangu muda huo wamekuwa wakiishi kwenye makambi ya wakimbizi yaliyoanzishwa nchini humo
Pamoja na kuwahimiza ndugu zake hao kurudi kwao vile vile viongozi hao wamehimiza kupatikana kwa haraka taifa la Palestina litakalokuwa na makoo makuu yake Jerusalem.
Suala jengine walilokubaliana viongozi hao wawili na serikali ya Lebanon kuchukua mamlaka kamili ya kuzisimamia kambi hizo za wakimbizi mpaka hapo taifa la Palestina litakapokuwa limeanzishwa.