Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Alipokuwa nchini Uturuki wiki iliyopita kiongozi wa mamlaka ya Palestina alihutubia bunge la nchi hiyo na kujigamba kuwa akirudi nyumbani atakwenda Gaza kwani eneo hilo ni sehemu ya Palestina na hatoruhusu litawaliwe na Israel.Wabunge wa bunge walimshangilia sana.
Tangu arudi ni wiki sasa na hakuna taarifa iwapo tayari ameingia eneo hilo kukagua uharibifu uliofanyika.Ahadi yake hii ni sawa na zile zilizotolewa na zinazoendelea kutolewa na wenzake bila vitendo.
Iran ameahidi mengi kuhusiana na Gaza na bado hawajatenda lolote.Uturuki nayo hivi karibuni ilikuja na kauli nzito iliyotoa matumaini kwa wapalestina.Hata Misri nayo imekuwa ikitoa maneno matupu huku wapalestina wakiuliwa upande wa pili tu wa mpaka.
Hayo yakitokea upande wa waliotarajiwa kuwa watetezi wa wanawake na watoto wa Palestina,viongozi wa Marekani wanaendelea kumiminika Israel na kutoa kauli ambazo ni kama kuilinda Israel kwa kuwatisha Hamas na watawala wa mashariki ya kati ili wakubaliane na matakwa ya Israel.