Mahojiano Kituo cha Polisi na Kesi Hipo Mahakamani ni Sahihi?

Mahojiano Kituo cha Polisi na Kesi Hipo Mahakamani ni Sahihi?

jaduu

Member
Joined
Aug 8, 2013
Posts
7
Reaction score
0
Habari wana JF, nina rafiki yangu ana kesi mahakamani kwa tuhuma ya kushiriki katika tukio la wizi wa pikipiki tukio limetokea January mwaka huu yeye pamoja na wenzake wawili wapo nje kwa dhamana.

Tatizo ni kwamba polisi bado wanataka kuwafanyia mahojiano kituoni na lihali kesi ipo mahakamani naomba ufumbuzi kwa hili.

Nawasilisha
 
Nijiavyo mimi, hata kama kesi iko mahakamani upelelezi huendelea. Kwahiyo waweza hojiwa if need be.
 
Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai 'The Criminal Procedure Act' inataja Muda maalumu Wa kuhojiwa mtuhumiwa akikamatwa. Mtuhumiwa anapaswa kuhojiwa ndani ya Masaa manne baada ya kukamatwa. Baada ya hapo ni kinyume cha sheria kumhoji mtuhumiwa. Polisi wanaweza kumhoji baada ya Masaa manne yaliyotajwa hapo juu kama watapata kibali cha mahakama cha kuongozewa Muda Wa kumhoji mtuhumiwa/mshitakiwa.
 
Back
Top Bottom