Mwande na Mndewa
JF-Expert Member
- Feb 26, 2021
- 1,117
- 3,153
Abdul alipokutana na Rais wa Uganda, nlimsema sana kwenye mikutano yangu, Abdul alitaka kujua kwa nini nilimsema, nilimwambia hii sio nchi ya kifalme au kimalkia hadi wewe ukaiwakilishe nchi, Mama yako ni Rais sio Malkia, wa hiyo wewe sio wa kuiwakilisha nchi popote.
1. Kuhusu hoja ya Abdul kupelekwa kwa Lissu na watu wema ama Wasamaria kama alivyowaita.
Kwanza, lazima mhusika ajiulize, huyo au hao watu wema/wasamaria ni nani/akina nani?
Automatically, kama alivyosema ni wenzake na kwa uthibitisho nilionao ni wakubwa wenzake na Lissu ndani ya Chadema.
Sasa kama hao WEMA ni wenzake, huwezi kuona ni kwa kiwango gani Lissu analitumia jina la wema ama wasamaria kinafiki,kama kweli ni watu wema, kwa nini aliukataa huo mpango wa wema wao!?
Kama kweli ni wema, mbona wameingia mahusiano ya kufuatana na Mtoto wa Mama ambaye anaongoza Chama ambacho ni adui namba moja wa Chadema.
Pia soma: Kuelekea 2025 - Tundu Lissu: Abdul alitaka tukutane kwenye hoteli moja Masaki anihonge, nikamwambia njoo kwangu
Kama kweli mhusika/wahusika ni wema mbele ya Lissu kama huyu anavyomaanisha, mbona Chadema ipo vipande viwili sasa na hakuna maelewano totally?
Kama kweli aliye/waliompeleka Abdul ni wema, mbona wamepeleka Rushwa/Hongo kwa Kiongozi wa Chama Kikuu cha upinzani?
Kama kweli Lissu anamaanisha huyo/hao ni mwema/wema mbona aliamua KUTEMBEA hadharani akiomba michango ya kununuliwa gari na akaacha fedha za wema waliotaka akanunue gari jipya?
2. Kuhusu hoja ya Mama za Barua za Lissu kulipwa gharama zake za matibabu.
Kimsingi huu ndio uliokuwa msimamo wa Lissu kwamba, sitaki hizi fedha haramu mlizoniletea, badala yake kama kweli mnanionea huruma, nenda umwambie mama yako anilipe zile gharama zangu za hospital.
Abdul akasema, Mama anasema hujaandika Barua, naye Lissu akamjibu, nilishaandika mpaka sasa zimefika Barua 2 na hapo hapo Video inaonyesha Lissu akimpa nakala ya Barua mojawapo ili Abdul ampelekee Mama yake.
Wakati, hilo jinga lingine la Chadema lilikuwa limezubaa jinsi Lissu anavyoweka msimamo.
3. Hoja ya tatu ni kuhusu assumptions za mtoa hoja kwamba, huenda Abdul alimdanganya mkubwa wa CHADEMA kwamba anampelekea hela za matibabu.
Kwa jinsi ambavyo Tundu Lissu ameelezea kwamba kuna watu wema ndani ya Chadema walimpeleka Abdul nyumbani kwake, basi Chadema kuna watu wajinga na hizi ndio aina ya akili za baadhi yao.
Yaani fedha za malipo ya matibabu ya Lissu zipekekwe kwa Lissu sebuleni zikiwa kwenye bahasha; tena Kiongozi wa juu ndani ya chadema asijue kwamba, malipo ya fedha za serikali yanafanyika kwa mujibu wa Sheria na sio mkononi.
Lakini pia, kama sio akili za kijinga, unawezaje kufikiria jambo kama hili hata usijiulize kwamba, kama kweli yale yalikuwa malipo ya matibabu ya Lissu;
1. Kwa nini yapelekwe kwa Lissu yakiwa kwenye bahasha?
2. Kwa yapelekwe kwa Lissu na Mtoto wa Mama asiye na cheo chochote Serikalini? Huyu kiongozi wa juu wa Chadema alikuwa Bogus kiasi gani mpaka aamini zile ni fedha za malipo ya aliyekuwa Mbunge? Hata sio Waziri, Kiongozi wa Bunge, Mkuu wa Wilaya wala hata (Abdul) sio Mfagizi wala Shamba Boy kwenye Ofisi yoyote ya Serikali.
Punguzeni ujinga huu wa rejareja mkisaidie Chama chenu kinaelekea kufa.