Mahojiano ya Rais Samia na BBC yataongeza maswali na sio majibu

Rais anaingilia kesi iliyoko mahakamani. Kwa kauli yake hiyo aliyotoa tayari keshamuweka hakimu katika wakati mgumu

Kwa jinsi ilivyo mahakama zetu zinafanya kazi kwa tone ya rais. Kwa maneno marahisi hakimu/ Jaji tayari ameshaandikiwa hukumu iweje. Hatuna mahakama ya kutoa haki kinyume na mtazamo wa rais.
 
Leo kwenye interview kaupigwa mwingi sana..kikeke kalabiwa juu mpaka anakosa cha kuuliza. Kila swali anapata jibu sahihi mpaka na yeye anatungisha kichwa cha kukubali jibu murua...

Yale yalikuwa ni majibu na sio majawabu. Imeisha hiyo.
 
Leo kwenye interview kaupigwa mwingi sana..kikeke kalabiwa juu mpaka anakosa cha kuuliza. Kila swali anapata jibu sahihi mpaka na yeye anatungisha kichwa cha kukubali jibu murua...
Itabd waje na Agenda nyingine
 
Kwenye hili la Mbowe mama kajiharibia sana ,sijui kama anashauriwa na wanao mpenda!
Kile kinachodaiwa ni makosa ya awamu ya sita mnasema mama hashauriwi vizuri.lawama zinaelekezwa kwa washauri wake.kana kwamba yeye ni too immature.

Ila 'Makosa' yanayotajwa kutokea wakati wa awamu ya tano ni ya magufuli peke yake.kana kwamba hakuwa na washauri wake.
 
Kama umemsikiliza akihojiwa na salim kikeke hajashindwa swali hata moja, kikete kaishia kutingisha tu kichwa cha kukubali kwa kila swali...
Hapa ni kwamba yale mafisi yatakosa pa kushikia, kama yalipanga angefeli basi imekula kwao...
Salimu kikeke alijua wazi anaenda kuleta mjadala sio kuwapa watu majibu.
 
Kama umemsikiliza akihojiwa na salim kikeke hajashindwa swali hata moja, kikete kaishia kutingisha tu kichwa cha kukubali kwa kila swali...
Hapa ni kwamba yale mafisi yatakosa pa kushikia, kama yalipanga angefeli basi imekula kwao...
Ukiwa mjinga, unaweza kuamini kuwa mtu akiropoka chochote baada ya kuulizwa, basi ameweza kujibu.
 
Umeonaje mama yako asiye dhalimu?

Sio dhalimu kama lile dubwasha lako lililoko motoni, yeye anaiga tembo kunya, na uzuri mama wa kambo yuko mwenyewe humu humu jukwaani tunampa ukweli wake.
 
Sio dhalimu kama lile dubwasha lako lililoko motoni, yeye anaiga tembo kunya, na uzuri mama wa kambo yuko mwenyewe humu humu jukwaani tunampa ukweli wake.
Siyo dhalimu kama lile dubwasha lako!

Na anaupiga mwingi! Magaidi ndani! Alafu kumbe yalijificha Nairobi!

Mi 10 kwa mama
 
Salimu kikeke alijua wazi anaenda kuleta mjadala sio kuwapa watu majibu.

Hapana sio majibu bali majawabu. Majibu yanaweza kuwa yoyote kama mama wa kambo alivyofanya hata kama sio sahihi, lakini majawabu ni yale yaliyo sahihi, kitu ambacho mama wa kambo hakufanikiwa.
 



Tatizo la Tanzania vyombo vya usalama vimeingizwa sana kwenye siasa. Tatizo lingine ukisha ingiza vyombo vya usalama kwenye kazi na siasa utakuwa na matatizo makubwa sana mfano angalieni uchaguzi na wizi wa kura 2020 yaani mgombea anapata kura zero hata kwenye kituo ambacho yeye kapiga kura! Sasa kama nchi ni kwanini tulitumia mabilioni kwenye uchaguzi kama pesa zinapotezwa hivi kwa shughuli ambazo ni za kudanganya wananchi. Hatuwezi kuacha kumlaumu Hayati Magufuli kwa hili kafanya makosa makubwa sana kwa kuingiza usalama na polisi kwa kiasi hiki serikalini. Sasa wanajiona wenyewe ndiyo wanajua wafanye nini kuanzia ulinzi mpaka siasa
 
LEO MAMA KATUANGUSHA SANA WATETEZI WAKE SIAMINI KAMA ANGEWEZA KUJIINGIZA KWENYE MAHIJIANO AMBAYO YAMELETA MASWALI KULIKO MAJIBU

SUALA ZIMA LA KUKAMATWA NA KUPEWA UHAINI MBOWE TULIAMINI ATALIMALIZA KATIKA HALI AMBAYO ISINGEMUUMIZA KISIASA LAKINI LEO KATUMBUKIA MAZIMA KWENYE MTEGO WA MAADUI zake HASA NDANI YA CCM AMBAO WANATAKA KUMUWEKA KWENYE HALI YA TAHARUKI NA KUKOSA UTULIVU ILI UTAWALA WAKE UKOMEEE 2025

SANA SANA HAKUA HATA NA HAJA YA KUJIBU HILO SWALI ANGESEMA TU KESI IKO MAHAKAMANI

MAMA LEO KAANGUSHA WANAOMTAKIA MEMA NDANI YA CCM NA HATA NJE YA CCM

WAKATI HAYA YAKITOKEA ULINZANI NDANI YA CCM UNAENDELEA KUWA IIMARA

MAMAA ANATAKIWA MAOMBI ILI ATULIZE AKILI
 
Tunamshukuru Mungu kwa kutuondolea lile jitu liovu bila damu kumwagika. kwa sasa tuko na mama wa kambo, na inaeleweka mama wa kambo si mama.
Kabisa lile jitu lenu ovu mungu wenu aliliondoa bila damu kumwagika.
Na sasa tuko vizuri hadi magaidi sasa yanakamatwa, kumbe lilie jitu ovu lilikuwa linalea magaidi!

Nashauri huyu mama kwa kuwa siyo dhalimu aipige miaka elfu kabisa, tunakuwaje na magaidi nchini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…