Mahojiano yangu na washirika wa FDLR kuhusu uhasama wao na RPF- Inkotanyi

Mahojiano yangu na washirika wa FDLR kuhusu uhasama wao na RPF- Inkotanyi

Naomba kujua mauaji ya kimbali ya Burundi yalisababishwa na nini.
 
INAENDELEA..................!!!
GOMA ZAIRE 1994:
Afande ""f""" anasema kua alikua hana jinsi ila na yeye kuanzisha vuguvugu lake la kijeshi ili kujitimizia ndoto zake za kisiasa.
Kwanza alichukia kuishi ugenini.
Pili alichukia kusalitiwa na PAULO.
Tatu alichukia kupoteza maliasili watu kwa chuki za kikabila.
Nne aliumia kupoteza madaeaka yake kijeshi na kiutawala.
Na anasema afande F kua katika makundi yote ya wanyarwanda waliokimbilia nchini Zaire,kulikua na mgawanyiko mkubwa sana wa kikabila na kisiasa na kiutendaji na kinidhamu kijeshi.
Makundi ya wanamgambo wauaji wa raia na wabakaji yalikua yamejichanganya na makundi ya wanajeshi walioangushwa wa serikali ya Rwanda na yalikua yanaendesha kambi za wakimbizi kwa mkono wa chuma na kuiba vifaa na misaada iliyokua inatolewa kwa wakimbizi na jambo hilo lililalamikiwa sana na wafanyakazi wa mashirika ya misaada ya umoja wa mataifa na mashirika ya hisani za kutoa misaada ya dini mbalimbali.
Walioumia zaidi anasema afande F kua walikua raia wa kawaida ambao walikua wahanga wa mauaji ya kimbari bila kujali ni wahutu au watusi.
Na anaendelea kusema afande F kua katika harakati zake za kujiimarisha kijeshi alikua anapata full support kutoka kwa wanajeshi wa Zaire wenye asili ya kinyarwanda hasa wahutu na hata mwanzo kabisa wa jeshi lake,,aliwasajili vijana wengi wa kinyarwanda waliokua wamelowea Zaire kwa miongo mingi tokea miaka ya 1960,s.Ambao wazazi wao walikimbia rwanda kwa sababu za kiuchumi na kisiasa na kulowea nchini Zaire kutafuta maisha,,,wengi wao wakiwa vijana wa kihutu na watwa na watusi wachache.
Anasema roho ilimuuma sana sababu wale watu waliomsaliti ndio waliochukua madaraka na kusababisha mauaji ya kimbari,alafu lawama akabebeshwa yeye.
Na kwanini abebeshwe lawama kwa mipango waliosuka watu wengine na ambao baadhi yao wanashikilia madaraka kwa wakati huo nchini Rwanda na Burundi.
Afu yeye akiwa ukimbizini alikua anabebeshwa lawama kama mmojawapo wa waanzilishi wa mauaji ya kimbari.
Anasema afande""f"" ila hakua na jinsi akaamua kua ipo siku huko mbele atakuja kusafishwa na historia.
Basi afande F akaja na mpango kazi wake kimkakati kama anavyofafanua mwenyewe kwa kifupi.
MPANGO KAZI ULIKUA HIVI.
1: Kuondoa upinzani ndani ya jeshi lililopinduliwa na RPF na kukimbilia Zaire,kwa kuunganisha vikosi vya wanajeshi wa RDF na kubadilisha mitazamo ya vijana wa iliyokua intarehamwe militia force.
2:Kuondoa ushawishi wa kisiasa wa Mzee Sindikubwayo na washirika wengine wa serikali iliyopinduliwa na RPF.
3:Kuingia ubia na jeshi la Zaire ili kupata silaha na intelejisia network.
4:Kuwatumia intarehamwe kwa manufaa yake kijeshi na kuwabadili mitazamo yao ya chuki za kikabila.
5:Kumiliki maeneo yote ambayo wanyamulenge walikua na ngome zao ili kuvunja nguvu za RPF huko mashariki mwa Zaire.
6: Kurudi Rwanda na kushambulia kijeshi na hilo ndio lengo la afande"""f"""toka alipokimbia Rwanda.
Afande F anasema anasikitika kua mpango kazi namba sita ulishindikana kutekelezwa kwa wakati baada ya wafadhili wake kumnyima zana za kivita kwa makusudi kwa manufaa yao ya kiuchumi na kisiasa.
Na waliomchelewesha anadai ni watu walewale waliohusika na kupanga mauaji ya kimbari nchini Rwanda na Burundi miaka hiyo ya 90,s.
Anasema kua mpango namba mbili ulikua mgumu pia ila ulifanikiwa na ulifanikiwa baada ya watu kuanza kuona ukweli kua,,ukabila na chuki waga havina mshindi kwa upande wowote ule ila vinaleta madhara ya kudumu katika jamii.
Mzee Sindikubwayo alikua mbaguzi na aliamini katika ubaguzi na aliwavutia watu wanaoamini katika ubaguzi.
Na kuna kitu cha muhimu sana ambacho ningependa hapa ninukuu asemacho afande""F"""
Watu kila wanaposikia mauaji ya kimbari basi wanawaza 1994 ila hawajui kwamba kwa wanyarwanda kumekuwepo na mauaji ya kimbariya kuuana kutokea mwaka 1920 na 1936 na 1939 na 1944 na 1952 na 1958 na 1964 na 1968 na 1972 na 1976 na 1987 na 1991 na na 1992 na 1996 na 1998 na 2002 na 2011 na 2016 na mauaji haya yote yaliwakumba either watusi au wahutu kwa nyakati tofauti ndani ya Rwanda na DRC kwa sababu ya uchochezi wa wanasiasa na uroho wa madaraka na ukabila miongoni mwa jamii za kinyarwanda
Anasema afande kua hivyo taratibu basi akaaanza kuunda jeshi lake la vuguvugu za kisiasa na kijeshi akiwa kama kamanda wa vikosi vya serikali ya Rwanda iliyopinduliwa na RPF.
Anasema haikua kazi rahisi kwa sababu vikosi vya RPF navyo vilivuka mpaka na kuungana na vikosi vya wanyamulenge wenye asili ya kitusi ili kuwashambulia wao.
Na anasema hali ilikua ni vita juu ya vita kwa miezi yote iliyobakia ya mwaka huo 94 ila ilikua ni mapambano ya kimya kimya kwa takribani miezi mitatu,,,,,akilijenga kundi lake kijeshi na pia akiwazuia wanyamulenge na RPF kumsogelea.
Na ikumbukwe makamanda wengine pia wa lilulokua jeshi la Rwanda RDF nao waliunda makundi yao ya kijeshi mwaka huo ila yalizidiwa nguvu na RPF pamoja na Banyamulenge walipovamia mashariki mwa Zaire kimya kimya mwaka huo kuwasaka intarehamwe na wanajeshi wa RDF huko kivu kusini na kivu kaskazini
Afande F anasema kua,,yeye kama kamanda wa kijeshi mwenye uzoefu wa mapambano aliamua kutumia busara na kuhamishia kambi zake za kijeshi na wanajeshi wake na silaha zao ndani zaidi ya Zaire karibia na mpaka wa Uganda na kuacha kukaa karibu na mji wa Goma au mji wa Bukavu ili kupata mda wa kujijenga upya.
Aliamua kutulia na kujipanga upya kijeshi kwa mikakati maalumu na wala hakutaka kua na mihemuko ya kisiasa au kikabila na afande""F"'
Anasema katika vita na mapambano ya kijeshi****JITAHIDI SANA USIENDESHWE NA MIHEMUKO NA UPEPO WA KISIASA****la sivyo utafeli.
Na aliposema kufeli alikua anamaanisha kua utashindwa kutimiza mipango yako yoote ya kijeshi na kisiasa kama utakua mtu wa mihemuko na ukawa unaendeshwa kwa hisia zaidi kuliko akili.
*****************
CHOMBEZO LA UDAKU
MKUTANO WA RPF KIGALI 1994:
Baada ya wanachama wa RPF kuichukua Kigali basi waliitisha mkutano wa siri na kuanza kupanga mikakati ya kutawala na aina ya serikali watakayokua wanaitumia.
Siku ya mkutano ulizuka ugomvi mkubwa sana kati ya afande PAULO 😂😂 na BIZZY GOD 😂😂 na ugomvi wao ulikua ni kwamba BIZZY GOD 😂😂 hakutaka kutumiwa kama kivuli cha utawala.Alikua na hasira sana kwa yote aliyojitolea kwa RPF afu akaishia kuwekwa kua kiongozi kivuli chini ya afande PAULO 😂😂.
Na hilo lilipelekea mvutano mkubwa baina yao na ambao ulikua na faida kubwa kwa afande""F""" siku za usoni.
Mkutanoni afande PAULO alidai kua watu wote wanaombishia ni kama inzi na atachukua rungu na kuwatwanga mmoja mmoja na haoni ajabu kufanya hivyo wakati wowote.
Badala ya kujenga ila huu ulikua ni mkutano wa kuanza kutenganisha wanachama wa RPF kimatabaka na kisiasa.
BIZZY GOD😂😂 na afande PAULO🤣🤣 walitoleana maneno machafu na kuvimbiana misuli adharani mbele ya wanachama wengine wa RPF pale mkutanoni.
******************************
MWISHO WA UDAKU
Tuendelee na Afande""F""
Anasema kua mambo hayakua marahisi mwanzoni ila yeye kama mwanajeshi mzoefu aliamua kupambana hadi mwisho.
Kwanza ilibidi atafute vyanzo vipya vya mapato na atafute washirika wapya wa kusapoti harakati zake akiwa ukimbizini Zaire.
Na wakati huo huo akihakikisha kua hakuna jambo lolote linaloweza kuvuruga maandalizi yake ya kijeshi na harakati zake za kisiasa.
Maana vikosi vya wanyamulenge na RPF vilikua vinamsogelea siku zote kumkabili na kutaka kusitisha harakati zake za kijeshi ndani ya kivu kasikazini na kivu kusini katika mwaka huo 1994 na walimshambulia kimya kimya bila ulimwengu wa kimataifa kujua.
Ikumbukwe kua RPF walikua na sera yao ya kuwafuata maadui wao kisiasa na kijeshi popote pale ndani ya Zaire na kupambana nao kijeshi,,maana Zaire ilikua ni kama SHAMBA LA BIBI.
Anasema afande ""F"" kua maisha ni safari na safari hiyo ya maisha ndio iliyompelekea kua pale alipo ukimbizini Zaire,,kutoka ikulu kumlinda raisi mpaka kulala maporini chini ya miti na kujikimu kwa hali tete tete za ukimbizini katika nchi ya ugenini.
Na mbaya zaidi akiteswa na hisia za wale washirika wenzake ambao walimsaliti na kumuua mshirika wake FRED.
Alijiapiza kulipa kisasi wakati wowote ule atakapopata nafasi ya kukutana nao katika uwanja wa mapambano na alijua ipo siku fursa hiyo itawadia.
Kiufupi afande""f"" alikua hana roho ya huruma kwenye uwanja wa mapambano na alinieleza roho ya huruma kwenye uwanja wa mapambano ndio ilimponza swahiba wake FRED.
TOLEO LIJALO TUTAANZA KUANGAZIA MWAKA 1995 NA AFANDE""F"""ALIKUA NA NINI CHA KUNIELEZEA.
ITAENDELEA................!!!!!!
 
Back
Top Bottom