Mahusiano chuoni huwa kama 'drama'

Mahusiano chuoni huwa kama 'drama'

Utakuta wanachuo wanatembea kwa kufuatana kama kumbi kumbi; mwanaume hataki kumuacha mwanamke, na mwanamke naye hataki kumuacha mwanaume.

Mmoja akienda maktaba, mwenzake anamfuata, hivyo hivyo hata kwenye magrupu ya 'discussion'. Ulikuwa ukiingia kwenye vyumba vyao, utakuta matunda, juisi, wine n.k zimejaa kwenye friji; sisi wengine tuliishia kutamani tu.

Kulikuwepo na dada mmoja alikuwa na chura hatari sana, ilikuwa kila ukikutana naye lazima uishiwe pumzi; ingawa baadhi ya watu waliowahi kumuona huko nyuma, walikuwa wanasema hiyo chura ameitengeneza. Halafu miaka hiyo, ndio vipedo vimeingia, alikuwa akivipiga vinamtoa hatari. Kwa upande wangu niliishia kutamani tu, kwa sababu sikuwa na meno.

Nilikuwa kila binti nikimtongoza hapo chuoni, wananipiga kalenda, na mwisho wa siku nikawa najiongeza, kuwa hapa nimekataliwa. Baadaye nilikuja kugundua, kwa sababu nilikuwa navaa rafu sana, nilikuwa navaa mashati makubwa huku nyuma yanaachia mkia kama wa mjusi ,halafu sichomekei, pia nywele nilikwa naziacha ziwe ndefu.

Baada ya kuona chuoni sipati, nikaanza harakati za kutafuta wapenzi kwenye vyuo vingine pamoja na wafanyakazi. Ikawa kila wikiendi inabidi nisafiri nikakutane na mwenzangu.

Changamoto zilianza baada ya kuhitimu chuo, hakuna kazi hakuna hela, maisha yamesimama, wote niliokuwa nao tukapotezana kwenye mawasiliano, akabaki mmoja tu alisoma 'pspa' akawa amepata kazi sehemu ya kujishikiza; tukawa tunaendelea naye mpaka kuja kubeba ujauzito.

Kutokana na harakati za maisha, ikanilazimu tuwe mbali mpaka mtoto alipozaliwa; nimekuja kuonana naye amekuwa mama mtu mzima kwa sababu alikuwa amenizidi miaka kama 3 pia ana ule mwili mkubwa; ukichangia na ukuaji wa mwili baada ya kujifungua, akawa anaonekana kama mama kwangu. Kwa hiyo hatukuweza tena kuendelea, ila alikuja kuolewa na mtu mwingine.

Je, katika harakati zako za masomo, zilikupatia mahusiano ya kudumu?
Wa kwangu nilianza nae primary...sekondar..chuo kikuu...na sasa tuna WATOTO wawili. Kama napenz ya Ukweli... Inawezekana
 
Sijawahi tongoza chuo ila niliwahi kupendwa na madem wawili nyakati tofauti,mmoja ni mke wa kigogo flani saizi na alikua anakuja hadi geto nikawa namuona mbovu nikampotezea hadi akakata tamaa. Saizi ni bonge la kisu yan (Sityupidi mi)
 
u
Kuna couple moja chuo ilikuwa ya mfano kuanzia walimu mpaka wanafunzi wote walikuwa wanaijua tukajua watakuja kuoana aisee walipomaliza chuo yule demu alipata ujauzito wa mwanaume mwingine huku yule jamaa yake alikuwa mkoa mwingine kikazi ndo nikajua kweli mademu wanajua kuigizau
umeona uje kutusema huku😀😀😀
 
Nikiwa chuo, nilipata mpenzi mwaka wa kwanza semester ya pili! Ilikua kazi sana kunfanya atulie, nilifanya kazi kubwa ya kumjenga. Alikua anapenda kuwa karibu sana na wavulana ma bishoo!

I was so cool, life gheto ilikua chini sana. Tulikua tunaishi watatu, na tumelalia godoro bila kitanda kwa miaka miwili ingawa tulikua na mikopo wote 100%.

Sometimes manzi akawa ananishawishi nihame, nikapange naye. Nikawaambia rafiki zangu, wakasema usipange, utapoteza malengo yako. Nikamkazia.

Nilimjenga sana, tulipita nae katika mambo mengi, ila mpaka leo, nipo nae nimeoa (si kwa harusi) tunalea mtoto mmoja.
 
Back
Top Bottom