Mahusiano Kati ya Kijana, Mama wa Kijana, dada wa Kijana na mke wa Kijana

Kuna jamaa yangu mmoja alivyoona figisu zimezidi akamwambia mama yake tafadhali maana naomba uniache na Mimi nifurahie maisha ya ndoa Kama wewe ulivyofaidi na baba yangu..

Hapo si ndio kuanzisha vita kabisa? Mke atachukiwa wazi wazi
 
Kweli kabisa mkuu, unakuga maza yupo zake Mbeya, sister kaolewa Mtwara, we na familia mnaishi Arusha, hapo huwezi ona figisi hata siku moja.
YOU NAILED IT.[emoji625][emoji625]
 
SAsa hivi ndo naiona comment yako..loh!kwanini sasa na wewe..totoz zote hizo mtaani..hebu acha mambo ya ajabu basi

Bado nipo nipo kwanza, totoz kibao lakin wife material ndio changamoto nikipata kama wale ambao @Jokajeusi anaotuasa ndio naoa. 25+ afu awe virgin nasukuma ndani.
 
Mimi binafsi nimejitahid kusuluhisha utata kati ya mke na mama yangu na ndugu zangu wote lakini mara kadhaa naishia kufeli na kuachana na mkewangu mpendwa na baada ya kufikiri kwa kina naamua kumrudia tena mkewangu nimeachana na kurudiana na mkewangu mara 4 kwa Sasa nimeamua niishi tu na mkewangu sitaki kabisa kusikiliza chokochoko za mama na nduguzangu wengine japo wao wanaamini nimewekewa limbwata na nimerogwa na mkewangu.

Lakini me sijali maana nampenda mkewangu namama nampenda pia na tayari mama yangu kesha nilaani kuwa kama naendelea kuwa na mkewangu basi yeye sie mama yangu na kwenye msiba wake nisikanyage. Kimsingi mama yangu anadai mkewangu ni maskini kwao kwahiyo mzigo wa majukumu utanielemea pia ananicheka eti sijui kuchagua wanawake wazuri basi nimeamua poa tu sasa ni miaka 5 bado mama yangu amekaza tuna mtoto wakike ana miaka 3 hamjui kabisa bibi yake kutokana na kutokuwepo kwa maelewano.
Doh!. Pole sana, pia hongera zaidi kua na maamuzi ya kweli.
Mungu akubariki.

Sent from my Redmi 5 using JamiiForums mobile app
 
Mimi binafsi nimejitahid kusuluhisha utata kati ya mke na mama yangu na ndugu zangu wote lakini mara kadhaa naishia kufeli na kuachana na mkewangu mpendwa na baada ya kufikiri kwa kina naamua kumrudia tena mkewangu nimeachana na kurudiana na mkewangu mara 4 kwa Sasa nimeamua niishi tu na mkewangu sitaki kabisa kusikiliza chokochoko za mama na nduguzangu wengine japo wao wanaamini nimewekewa limbwata na nimerogwa na mkewangu.

Lakini me sijali maana nampenda mkewangu namama nampenda pia na tayari mama yangu kesha nilaani kuwa kama naendelea kuwa na mkewangu basi yeye sie mama yangu na kwenye msiba wake nisikanyage. Kimsingi mama yangu anadai mkewangu ni maskini kwao kwahiyo mzigo wa majukumu utanielemea pia ananicheka eti sijui kuchagua wanawake wazuri basi nimeamua poa tu sasa ni miaka 5 bado mama yangu amekaza tuna mtoto wakike ana miaka 3 hamjui kabisa bibi yake kutokana na kutokuwepo kwa maelewano.
Hee wewe yako mazito.Mungu akufungulie njia utatue hilo najua linakuumiza sana.
 
Nimetafakari Sana Mahusiano ya watu tajwa hapo juu, Yan kabla ya kijana kuoa na baada ya kijana kuoa.

Katika uchunguzi wangu mdogo familia nyingi kabla ya kijana kuoa zinakuwaga na utulivu amani na upendo baina ya kijana, Mama wa kijana na (ma)dada wa Kijana.

Lakini baada ya kijana kuoa na kuanza maisha yake mapya ya ndoa, mahusiano haya hupukutika taratibu na mwisho kuishia kabisa au kubakia na upendo wa kinafki.

Unakuta mwanamke ameolewa na kijana Hana tatizo lolote na wakwe au mawifi zake tabia njema, ustaarabu, heshima utiii vyote anavyo, lakini muda unavyozidi kwenda kunakuwaga na chuki zisizo julikana hutokea wapi kutoka kwa mama wa kijana kwenda kwa mwali, au Dada wa Kijana kwenda kwa wifi yake huyo.

Hapa sijazungumzia upande wa mke mkorofi. Nimezungumzia upande wa mke mwenye utii, heshima,adabu na kila sifa impasayo kuwa nayo " wife material"

Vitaanza visa, mikasa, chuki uchonganishi wa ajabu ajabu hapo usiombe kijana awe ameoa halafu anakaa na mama yake Mzazi au dada nyumba moja.. Huyo mke Cha moto atakiona...

Najaribu kuwaza ni kwanini mama mkwe hajawahi kukubaliana na Hali ya kwamba kijana ameoa na ampende mwali wake upendo ule ule anaompa kijana wake.. maana kimsingi hawa wote ni watoto wake.

Hii chuki huenda mbali mpaka kwa watoto wa Kijana na watoto wa dada wa Kijana.. upendo wa Bibi Mara nyingi kwa hawa wajukuu zake Mara nyingi hauwezagi kuwa sawa lazima tunkwa kiasi fulan watoto wa dada wa Kijana watapendelewa zaidi..😔😔

Mwisho wa siku Kama kijana atashindwa kuwa na msimamo mkali na kuweka mipaka Kati ya pande hizi mbili (mama mkwe)mawifi na familia yake mpya) ndoa hii huvunjika kabisa.🤔🤔

Ni kwanini familia ya kijana inashindwa kabisa kumpokea binti anayeingia kwenye familia yao moja kwa moja bila hizi figisu.🤓🤓

Japokuwa kuna baadhi ya familia mambo ni shwari upendo baina ya pande zote mbili upo wa kutosha.

Karibuni tubadilishane mawazo wanajamvi, wengi tunapitia hizi changamoto na zinaumiza Sana.
hii hotokea sana hasa kama wenyewe hamjaamua kufanya lile agano la asili
 
Ili huwepukane na hizi songombingo kama kijana unapotaka kuoa unashauriwa kukaa mbali na wazazi au ndugu.UNDUGU LAWAMA.
 
Mkuu wanawake hawapendani na hawana urafiki wa kudumu mara zote wanaishi kinafikinafiki hawawezi kuishi mwezi pamoja bila kununiana, kusengenyana au kugombana.
Pia hawa viumbe hawawezi kutunziana siri ndio mana hawaishi kusutana.

Epuka ile kujuana sana kama mwanaume yakupasa kujitahidi wewe pamoja na mke wako kutunza mambo yenu ya ndani na madhaifu yenu ya ndoa kwa ndugu na jamaa zenu.
Pia kuishi mbali na familia yako kwa wilaya au mkoa tofauti itapendeza zaidi na hata ukienda kusalimia msikae zaidi ya mwezi mmoja.
Na usisahau kujitahidi kutoa misaada ya hali na mali kwa wazazi na ndugu zako pale inapohitajika.
 
Mimi binafsi nimejitahid kusuluhisha utata kati ya mke na mama yangu na ndugu zangu wote lakini mara kadhaa naishia kufeli na kuachana na mkewangu mpendwa na baada ya kufikiri kwa kina naamua kumrudia tena mkewangu nimeachana na kurudiana na mkewangu mara 4 kwa Sasa nimeamua niishi tu na mkewangu sitaki kabisa kusikiliza chokochoko za mama na nduguzangu wengine japo wao wanaamini nimewekewa limbwata na nimerogwa na mkewangu.

Lakini me sijali maana nampenda mkewangu namama nampenda pia na tayari mama yangu kesha nilaani kuwa kama naendelea kuwa na mkewangu basi yeye sie mama yangu na kwenye msiba wake nisikanyage. Kimsingi mama yangu anadai mkewangu ni maskini kwao kwahiyo mzigo wa majukumu utanielemea pia ananicheka eti sijui kuchagua wanawake wazuri basi nimeamua poa tu sasa ni miaka 5 bado mama yangu amekaza tuna mtoto wakike ana miaka 3 hamjui kabisa bibi yake kutokana na kutokuwepo kwa maelewano.
Duuuuu pole sana kwa changamoto.
 
Back
Top Bottom