Mahusiano kati ya namba ya NIDA na mfumo wa ajira yakoje? Dogo kazinguliwa ajira mpya, naomba ushauri wenu

Mahusiano kati ya namba ya NIDA na mfumo wa ajira yakoje? Dogo kazinguliwa ajira mpya, naomba ushauri wenu

muafi

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2015
Posts
2,557
Reaction score
6,128
Dogo ni mwalimu idara ya msingi,

Majina yake ya vyeti vyote ni MARIAM ELIAS (mfano)

Majina ya Nida ni MARIAM ELIAS MMASA.

Wakati wa kuomba ajira Tamisemi details zilikubali vizuri kabisa na mimi ndiye nilimuombea.

Selection zimetoka kachaguliwa lakini halmashauri wanamiweka kwenye mfumo eti nida inagoma!

Tunashangaa hata sisi, sababu inaweza kuwa ipi, wazoefu tatizo linaeza kuwa nn details zimepishana wapi
 
Dogo ni mwalimu idara ya msingi,

majina yake ya vyeti vyote ni MARIAM ELIAS (mfano)

Majina ya Nida ni MARIAM ELIAS MMASA.

wakati wa kuomba ajira Tamisemi details zilikubali vizuri kabisa na mimi ndiye nilimuombea,

selection zimetoka kachaguliwa lakini halmashauri wanamiweka kwenye mfumo eti nida inagoma!


Tunashangaa hata sisi, sababu inaweza kuwa ipi, wazoefu tatizo linaeza kuwa nn details zimepishana wapi
Changamoto hayatofautiani kweli
 
VYETI VYOTE MARIAM ELIAS
NIDA MARIAM ELIAS MMASA

kipindi anaomba TAMISEMI mfumo wa oteas ulikubali,

lakini huku Halmashauri walipoemda kuripoti , eti namba yake ya NIDA inagoma kwenye mfumo sasa sielewi wao mfumo ukoje
Hapo angalia cheti cha kuzaliwa majina yanafanana na vyeti vya taaluma.? Maana hiyo kawaida watu wanamajina mawili kwenye vyeti afu kwa NIDA wana majina matatu.
 
hao ni watu wawili tofauti... kwa msaada nenda katafute deed poll, mtafute mwanasheria akusaidie tofauti na hapo ajira umeikosa...
mkuu huwenda kuna kitu kingine labda, maana wapo walioripoti na wana majina mawili kwenye vyeti na nida matatu ila wamepokelewa
 
mtoa mada labda kama kuna yatizo lingne kabisa majina mawili kwenye vyeti haina shida yoyote kama jina la tatu kwenye kitambulisho cha nida na cheti cha kuzaliwa yanafanana

mfano cheti cha kuzaliwa yanatakiwa yasomeke
birth name Mariam
jina la baba elias mmasa

hapa hakuna shida yoyote ile ila

majina ya kwenye vyeti yakitofautiana hata herufi moja kwenye nida umeenda na maji maana nida kubadilisha ni mlolongo ila cheti cha kuzaliwa kubadili ni simple

mfano nida Mariam elius mmasa
vyeti mariam elias
yaani elias na elius zikatofautiana iyo a na u ni kwisha

mwisho vyeti vikiwa na majina mawili halafu nida majina matatu hamna tatizo lolote lile sema jina la tatu la nida liwe sawasawa na jina la tatu kwenye cheti cha kuzaliwa
 
Au mkuu tarehe zake za kuzaliwa aliziweka kule NIDA ni tofauti na za kule kwenye cheti cha kuzaliwa
hi pia ni virahisi ni kubadilisha cheti cha kuzaliwa tu ili tarehe ziendane na nida shida ipo kwenye majina ya nida pamoja na majina ya vyeti ivi kubadilisha ni shida vyeti havibadilishiki nida pia mlolongo wake sio wa nchi hii ila cheti cha kuzaliwa unaweza rekebisha hata majina
 
Au mkuu tarehe zake za kuzaliwa aliziweka kule NIDA ni tofauti na za kule kwenye cheti cha kuzaliwa
nahisi huwenda tarehe zake za kuzaliwa zilizopo NECTA ni tofaut na zilizopo nida, nahisi labda maana nida na cheti cha kuzaliwa ziko sawa, majina yako sawa, au NECTA haihusiki mkuu?
 
Back
Top Bottom