Kuna point umesema kwamba akina baba waongee vizuri na watoto wao wa kike kujua maswahibu wanayokutana nayo na kuwapa msaada na kama siyo wao basi kaka wachukue nafasi.
Mimi binafsi huwa sipendi kuona mtoto wa kike akinyanyasika mbele yangu halafu nishindwe kumsaidia, huwa ninaingilia ugomvi kwasababu mama yangu aliwahi kusema 'tangia niwe na baba yako sikuwahi kupigwa hata kibao '
Kuna mzee mmoja aliwahi kunambia hata siku moja usikubali mwanamke akanyanyasika na kuonewa mbele yako,ukimuacha bila kumsaidia utaonekana dhaifu.
Sasa dada yangu mmojawapo aliolewa, akapata watoto ,baadaye mwanaume akaanza kumzingua akimuona hana maana tena, kesi zote napewa mimi, nilivyovumilia nikachoka, siku moja nilikwenda na gari la mizigo nikamwambia fungasha kila kilicho chako nakurudisha nyumbani.
Yeye na watoto wake mpaka leo hii wapo nyumbani nilichomwambia kama atahitaji kuona watoto aje hapa hapa nyumbani maana hawezi kukunyanyasa ukiwa kwenu, shemeji yangu sikuwahi kumwambia chochote na huwa tukikutana ni salamu na story as if hakijatokea kitu.
Kwahiyo kaka ku- act kuisadia jinsia ya kike haijalishi ni mkubwa kwako au mdogo cha msingi simama kwenye uanaume wako. Nyinyi mnatutegemea sana kwenye kuwapa miongozo.
Pole sana Kasie.