Mahusiano: ni maajabu sana, Kuna jinsia ya tatu ( ukiacha KE/me )

Metronidazole 400mg

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2016
Posts
941
Reaction score
2,062
Sijui kama huu Uzi utabaki hapa, ila lengo kuu mjifunze kitu


Mnaweza msinielewe kabisa, na kujua lengo la thread hii ni Nini ok??

Hii Dunia imekwishwa wakuu, mpaka naandika hichi kitu natokwa na machozi kuanzia moyoni mpaka machoni.

Imebidi niaze na neno mahusiano, ili huu Uzi uwe hapa ili mjifunze.

Ni hivi, weekend hii iliyoisha nilikuwa jijini dar es salaam kwa Mambo yangu Fulani Fulani ( Mimi natokea mkoani ), Sasa baada ya mishe mishe za siku na kuhangaika ikanibidi niinge mtaani ( bar ) Fulani maeneo ya sinza kujipongeza na kuwaza Mambo yangu Fulani Fulani.

Hiyo bar niliyoingia ilikuwa na vibe sana, nikiri Mimi Metronidazole 400mg sikuwa na mawazo yoyote ya kifisi, lengo langu ni kupiga mbili tatu huku nawaza future ya maisha yangu.

Lakini Sasa Cha kustaajabisha nilijikuta na vutiwa na mwanamke Fulani ( ambaye ndiye alikuwa akiniudumia kwa wakati huo )

Mawazo yalihama kabisa, nikajikuta akili na hisia vinaenda sambamba kabisa, kiufupi nilimtani na nikawa kama fisi, mawazo yangu Mimi ni kwenda kumla TU ( hicho ndio kilichokuwa kichwani kwangu )

Kiufupi, kimwonekana, alikuwa mzuri sana kuanzia sura, shepu, mwonekano na kila kitu ndio maana nilimtamani

Kiufupi, nilifanikiwa na kukubaliana kulala wote kwa usiku huo, ila tulipofika hotel ni tofauti kabisa hakuwa mwanamke Bali ni SHOGA.....nilichukia sana na kuumia kwa wakati Mmoja.

Ila kama binadamu, nilimuhoji kwanini ameamua kuwa hivyo, majibu aliyonipa ndio msingi wa Mimi kuanzisha Uzi huu.......kesho nitawapa huo mkasa wake (Usimuhukumu mtu bila kujua chanzo ), lengo kuu ni ili mjifunze na kuwalea watoto wenu kwa kumtegemea Mungu na maadili sahihi

Nawaahidi kesho nitaandika kumalizia, haya maisha ni fumbo wakuu, inabidi tumtegemee mwenyezi Mungu sana, kuanzia sisi wenyewe Hadi familia zetu
 
kwamba alinizid kila kitu,coz sio kwa sifa ulizomwaga apo juu yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…