Mwanasayansi Kalivubha
JF-Expert Member
- Feb 4, 2024
- 344
- 926
Kuna mtu toka umfahamu yupo na heka heka za mahusiano tu kuanzia maongezi mpaka vitendo ila KI UCHUMI hali yake mbaya
Yawezekana ukawa wewe pia 😊 Mawazo yanayotembea kichwani mwako kwa wingi ni mahusiano tu , unatafuta ubunifu wa mahusiano kwa kasi kubwa zaidi ya unavyotafuta ubunifu kwenye Biashara.
Kama uko hivyo na huna pesa baji jua mahusiano yatazidi kukutesa tu sana
Mahusiano ni hitaji pia la kiumbe hai ila haimaanishi kuwa ni hitaji pekee hivyo bila kujizuia ukalifanya kuwa lenyewe tu ndio hitaji la pekee basi utafanikiwa huko tu ila kwingine mambo yatakuwa magumu sana kwako, kila hitaji lipe kiasi kulingana na wakati na umuhimu wake.
Hata kama wahenga walisema mahusiano sio pesa ila sio sasa ndio uache kutafuta hiyo pesa ukahamia kwenye mahusiano tu , Pesa ni hitaji muhimu pia kwa sababu lazima maisha mengine yaendelee ambayo yanahitaji pesa.
Sio sifa nzuri kumakinika zaidi na upande mmoja tu ilihali kuna mengi huna na ya msingi, kuna muda kweli mahusiano mazuri ndio chanzo cha utajiri ila pia lazima kuwe na kiasi yaani uwe na muda wa kutosha kufikiria pia uboreshaji wa uchumi .
Mwanasayansi Saul kalivubha.
Fikia Ndoto Zako.