Mahusiano ya Kimataifa: Rais Magufuli amefungua balozi mpya katika nchi 8 ikiwemo Israel, Mungu ambariki sana!

Mahusiano ya Kimataifa: Rais Magufuli amefungua balozi mpya katika nchi 8 ikiwemo Israel, Mungu ambariki sana!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Kwa ufupi kabisa kwa wale CHADEMA pamoja na Tundu Lisu mnaodai Rais Magufuli amefifisha mahusiano na dunia nataka niwakumbushe tu Rais Magufuli amefungua balozi katika nchi nane duniani ikiwemo Israel.

Tunapokosoa jambo tuwe tunaweka na uhalisia wa ukosoaji siyo kukurupuka.

Hata Ethiopia alikoishi Simon wa Kirene imefungua ubalozi wake Tanzania awamu hii ya Rais Magufuli.

Mungu wa mbinguni mbariki Rais Magufuli.

Maendeleo hayana vyama!
 
..pia Jpm hajui kuzungumza Kiingereza hivyo anashindwa kuwasiliana na kujadiliana moja kwa moja na viongozi wenzake.
Kwahiyo akihitaji kuwasiliana na rais wa ufaransa itabidi ajifunze Kwanza kifaransa. Na akihitaji kuwasiliana na viongozi wa china itabidi ajifunze kichina Kwanza?

kweli Tanzania tuanahitaji jambo la ziada Kwenye elimu yetu maana haitufunzi kufikiri

Sent from my Infinix X603 using JamiiForums mobile app
 
Baada ya kubanisha hivyo, kwa jinsi wapinzani (husani CHADEMA & ACT) walivyo na akili mbovu usishangae utakaposikia wakipinga tanzania kufungua balozi
 
Unamkumbuka Benjamin William Mkapa jinsi alivyokuwa akiipaisha Tz kimataifa?

JPM hata Kiswahili anazungumza cha kuunga-unga.

Na ana tatizo la kuzungumza matusi na lugha za kudhalilisha wanawake akiwa majukwaani.

Ni jambo jema kwamba hasafiri nje ya nchi, kwani akifika huko na kutoa lugha za kudhalilisha wanaweza kumtimua.
 
..Jpm ameleta magomvi na nchi majirani.

..cdm itarejesha mahusiano mema na majirani zetu ili BIASHARA zimeweze kushamiri.
Taja ugomvi huo unahusiana na nini acha utoporo wako hapa kwa kushikiwa akiri na tundu lisu, taja huo ugomvi umetikana na nini?
 
..pia Jpm hajui kuzungumza Kiingereza hivyo anashindwa kuwasiliana na kujadiliana moja kwa moja na viongozi wenzake.
Fullish? Hujui siku hizi translators. Unaseti kwenye lugha yako matukio yote yanakuja kwa lugha.
 
Baada ya kubanisha hivyo, kwa jinsi wapinzani (husani CHADEMA & ACT) walivyo na akili mbovu usishangae utakaposikia wakipinga tanzania kufungua balozi

..Jpm ametugombanisha na majirani zetu wa sadc na eac.

..Jpm anatukana marafiki zetu wa muda mrefu wa ulaya na america.

..ni kweli amefungua balozi 8 mpya, lakini ameharibu mahusiano yetu na nchi na jumuiya lukuki za kimataifa.

..kufungua ofisi za ubalozi ni jambo moja, kuwa na mahusiano mazuri na nchi mbalimbali ni jambo tofauti.
 
Kwahiyo akihitaji kuwasiliana na rais wa ufaransa itabidi ajifunze Kwanza kifaransa.
Na akihitaji kuwasiliana na viongozi wa china itabidi ajifunze kichina Kwanza?
kweli Tanzania tuanahitaji jambo la ziada Kwenye elimu yetu maana haitufunzi kufikiri

Sent from my Infinix X603 using JamiiForums mobile app
Umehoji vizuri sana!
 
Umehoji vizuri sana!

..mnakumbuka Benjamin William Mkapa alivyokuwa akiipaisha heshima ya Tz?

..huyu wa sasa hivi ni takataka ukimlinganisha na watangulizi wake.

..heshima yetu kimataifa imeporomoka. mahusiano yetu na nchi na jumuiya mbalimbali yamevurugika.
 
Rais Magufuli anaheshimika dunia nzima kwa kudhibiti Corona nchini.

Kama haitoshi Rais Magufuli karejesha uhusiano wetu na Israel kwa kumtuma balozi.

Rais Magufuli ameziongoza vizuri EAC na SADC kama mwenyekiti.

Maendeleo hayana vyama!
 
Ni kweli ameiwezesha na Tanzania kutoa misaada kwa nchi mbali mbali, donors country
 
Baada ya kubanisha hivyo, kwa jinsi wapinzani (husani CHADEMA & ACT) walivyo na akili mbovu usishangae utakaposikia wakipinga tanzania kufungua balozi

..hivi lile zoezi la kuzifanya nchi za Sadc zizungumze Kiswahili limefikia wapi?

..ndiyo maana tunasisitiza kwamba kufungua ofisi za ubalozi ni jambo moja, lakini kuwa na mahusiano mema, na kutumia fursa za kidiplomasia ni jambo lingine.

..Mara ya kwanza Jpm kwenda kusini mwa Afrika alikusanya kamusi za Kiswahili na kwenda kumbwagia Raisi Ramaphosa akimtaka ajifunze Kiswahili!! Badala ya kuzungumzia fursa za kiuchumi na kibiashara yeye amedata kwenye kuficha madhaifu yake ya lugha.

cc Nguruvi3
 
Back
Top Bottom