Najua hali ni mbaya sana hamna haja ya salamu
Wakuu nimesoma nyuzi nyingi na nimezungumza na watu wengi nimegundua kuwa kuna asilimia kubwa ya watu wapo kwenye mahusiano lakini mahusiano hayo ni Toxic
Acha wale wenzetu wa kuchukua sheria mkononi, wale wa kuangalia video za porn na wale wanaonunua huduma ya ngono kuna hawa watu wanaume kwa wanawake kwa sababu mbalimbali wamejikuta kwenye hayo wanayoyaita mahusiano lakini hawana raha, hawana furaha, wamechunda wakachurura
Wanatuma msg hawajibiwi, wakijibiwa wanacheleweshwa kwa visingizio lukuki
Simu zao hazipokelewi, na muda mwingine zinapokelewa wapenzi wao wakiwa katikati ya game na mtu mwingine (asee😂)
Wanablockiwa😂 (yani una mpenzi na anakubloku)
Na mengine mtaongezea
Lengo la uzi huu ni kuwakumbusha kuwa mahusiano hayo ni Toxic, ya kishenzi, hayakufai kwa ustawi wako wala wa mtu mwingine
Muache huyo mtu asee muacheee,
Achaneni muishi kwa amani
There’s more to life than these Toxic-Exploitative so-called relationship!
Kataa unyonyaji, Kataa Toxic Relationship
View attachment 2499927