Mahusiano ya kuwa na wanawake wengi na uchumi

Mahusiano ya kuwa na wanawake wengi na uchumi

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
41,558
Reaction score
64,966
Nimejaribu kuwaza sana, baada ya kuwa na watoto kadhaa kwa hizi pisi kali zangu.

Nikaona njia ya kuwaweka pamoja leo na kesho ni kuwashirikisha katika kutekeleza mawazo yangu kibiashara, ili wao na watoto wao waweze kupata chochote pamoja na kujivunia kuwa na mwanaume mwenye upeo wa kuona mbali.

Maeneo ninayotaka kuwashirikisha, ni katika upatikanaji wa malighafi pamoja na masoko yake.

Ikiwa na maana watakuwa kwenye mnyororo (supply chain) wa kuleta mali ghafi kwa equation x, na baada ya kufanyiwa kazi, watapelekewa bidhaa kama wasambazaji (distributors).

Mfano, kama nitashughulika na utengenezaji wa unga wa dengu; wao watatakiwa kuwa na ofisi zao za ukusanyaji wa dengu kutoka kwa wakulima, na kumuuzia equation x; ambapo equation x atasaga hizo dengu na kuwarudishia/kuwauzia unga kwa bei ya jumla ili waweze kuuza rejareja au jumla.

Mwisho wa siku kipato kinakuwa kinazunguka hapa na pale; hii itasaidia kwa watoto wangu 50, ambao kila mmoja na mama yake kuishi maisha mazuri pamoja na kujivunia kuwa na baba kama equation x.

Wakuu, wazo langu mnalionaje?​
 
Back
Top Bottom