Mahusiano ya mtandaoni

Mahusiano ya mtandaoni

Visa ninavyo vitano. wote nilikutana nao na wanne kati yao wote nilitembea nao. Nawapa kimoja kwanza ambacho ni the best

Mwaka 2019 kabla sijaacha kutumia Facebook niliwahi kupata msichana mmoja kutoka Arusha, by that time nikiwa Dar. Kuna siku nilinyuka pamba nikapiga picha nikazipost Facebook then nikatoka online. Nilipokuja kufungua data jioni kabisa nikaona kuna msichana katembelea page nzima na kulike kila kitu changu, kacomment picha za siku ile na akatuma ujumbe messenger.

Ikabidi nipitie zile comment zake na kusoma ujumbe wa messenger. Ni kama alikuwa akinisifia tu namna nilivyo. Ikabidi nipitie page yake pia kuona alivyo. Tulianza kuwa tunachat tu kama kawaida, akawa kaomba nimtumie namba sababu si muda wote tutakuwa online, nikaona sio case nikamtumia. Tulizoeana sana hadi ikafikia muda nisipomtafuta kwa muda au asiponitafuta najikuta namiss sana uwepo wake. Muda huo wote ni kama marafiki tu. Kuna siku usiku tukiwa tunaongea kwenye simu hadi mida ya saa 7 tukajikita kwenye deep conversation kama tayari tupo kwenye mahusiano, and that day was the beginning of our relationship.

Japo tulikuwa mbali ila alikuwa alinisisitiza niwe na imani tutakuja kukutana tu siku moja, nikawa namkubalia ila siamini. Nilijikuta nampenda na alikuwa akinipenda kupita kiasi, kwakuwa kwao ilikuwa ni familia yenye uwezo kuna muda nilikuwa nakwama mambo kibao na alinivuta mkono na kunisisitiza nikikwama nisisite kumwambia, na hapo hatujaonana kabisa...

Miezi kama minne ikakatika, kuna harusi ilitokea Dar ya mtoto wa baba yake mkubwa ikabidi waje kama familia, na hili alianza kuniambia muda kidogo kabla. Kweli, ndio ilikuwa nafasi ya kuonana nae kwa mara ya kwanza. Muda wote nilikuwa naona tu picha na kujenga imagination zangu tu kichwani juu ya muonekano wake halisi. The day I met her ndio siku niliamini kuwa sometime camera lies. She was so so beautiful, kimo cha kawaida, shaped na ni mweupe, anang'aa kama kifaranga kimetoka kwenye yai. Hakuna makovu wala mabaka kwenye ngozi. Hapo nilikutana nae Mawasiliano kituo cha daladala siku mbili kabla ya ile harusi. Hadi nikawa najistukia, how come a beautiful lady like this one kunizimikia kidume mimi? Yupo so charming, mchangamfu na mengine kama hayo. Ni kama tumeshawahi kuonana kabla. Ikabidi niondoke nae hadi sehemu moja niliyokuwa nimepaandaa na tukafanya yetu. I enjoyed for sure. Nikampa zawadi niliyokuwa nimemuandalia kama surprise, and she surprised me too kwa zawadi aliyonipa nje na sexy.

Baada ya pale, ni mengi sana yalipota pale katikati ila kufupisha story tuliendelea nae kama kawaida. I visited her and she visited me alipopata nafasi. Alikuwa hata akitengeneza safari za kuja kwa baba yake mkubwa Dar ila lengo ni kuonana na mimi. Ilifikia time zikaja habari za kuoana na mambo yalikuwa yanaelekea kutamu ila alikuja kunikosea nikajikuta sitaki hata kumsamehe kabisa, sijui shetani gani aliniingia. Kosa lililofuta mazuri yoote na kosa ambalo leo hii nikipima naona halikuwa na ulazima wa kutokumsamehe. She regretted a lot hadi anasema kabisa Rhymez, niambie basi nikufanyie nini unisamehe na ufute kosa langu iwe kama hakijatokea kitu, tuwe kama zamani niwe mkeo kabisa.. sikutaka kumsikiliza Rose, niliamua kuvunja line zote na nilifuta account yangu moja kwa moja ili nisipatikane kabisa kwake na kwa watu wa karibu niliokuwa nikiwasiliana nao kama dada yake, Mamdogo wake na marafiki zake. Nikasajili laini moja mpya kabisa.

Leo najutia mimi..[emoji19][emoji19] I lost a Gold
Ohhhh jamani, beautiful story with sad ending....poleee
 
Ngoja waje..sie wengine tunakutanaga vituo vya daladala tunakimbiwa[emoji38][emoji38]
Ukiomba buku tu ya salio limekuishia unashangaa uko blocked[emoji38]

NB:situmii mitandao yoyote wala sijipost na sijawahi hayo mahusiano.ndo nasubiri Jf kama itanibariki haya
Ikitokea jf nipatiwe kadi tafadhari.
 
Back
Top Bottom