Mahusiano ya mtandaoni

Mahusiano ya mtandaoni

Nlipataga mama humu moja
Comments za kipisi kali kingereza mingi
nikaona ewaa mtoto kaja Dm tukaongea mwsho namba zikatoka
Kwenda whatsap nkamtumia picha tufahamiane (that was a grave mistake)
Ving'ora vikaanza Wow wow wow
Kuja kutuma yeye nikabaki hiiiih
Sikuamini nkampgia video call La haula almanusura ntupe simu


Sjui yupo wapi saivi Aggy wa jukwaa la entertainment
🤣🤣🤣🤣🤣🤣 Ulikutana na "tuongee kiume"
 
Enzi za Facebook imetaradadi
Nilipost kapicha kangu by that time ndyo nmemaliza advance nasubiri kwenda chuo
Mkaka mmoja akaja messenger tukaanza kuchat chat
Simu niliyokuwa nayo ikaharibika nikawa naenda kwa jirani nachat weee halafu narudisha simu
Siku hiyo akaniomba no ya simu nilikuwa na kitochi
Mahaba yakahamia huko
Tulikuwa tunachat na kuongea the whole night
Enzi za chombeza time tunaongea sanaaa
Yeye alikuwa yupo kilimanjaro Same ni muhasibu wa chuo fulani mimi nipo Arusha.
Wakati naaply chuo akasisitiza niombe vyuo vya kilimanjaro ili tuwe karibu..
Nikawzaa nimesoma kilimanjaro na Arusha kwanzia chekechea hadi advance na chuo nisome kilimanjaro......nikamuitikia tu ila vyuo nikaomba Dar

Hapo hatujawahi onana ila tumeiva kwenye hubaa na maokoto alikuwa anatuma hadi pesa ya kuapply alinitumia nikaibana maana nilikuwa na mama akalipa
Nikachaguliwa chuo dar.. alimind sana kwamba nmefanya makusudi
Baadae tukapatana vizuri hadi siku naenda Dar tukachaguliana hadi nguo za kuvaa🤣🤣🤣
Nmefika chuo tukaendelea ila nikaona changes kwake
Kumbe kule nilikokuwa Naazima simu Kuna siku sikulogout huyo dada akaiba namba za simu kwenye chats za messenger wapo wanachat
Akampa uongo kibao kuhusu mimi hadi bwana yule akanichukiaa mwishowe tukaachana bila kuonana
Ikapita miaka bwana yule akanitafuta maana sijawahi badilisha number ndyo kunipa mkanda mzima alivyochat na jirani yangu hadi wakakutana na kunyaduana 😀😀😀
Akaomba turudiane hapo nshapata mupenzi nikamkatalia....sijui yupo wapi Johnson jamani 😆😆😆
Hadithi nzuri
 
Naanza kuelewa sasa mahusiano yanayoanzaga kwa kuwapa hela hawa viumbe ni njia rahisi ya ulaghai kwa kuwa ndiyo njia ya kula pisi yoyote ya kibongo... Kinachonishangaza kwanini wana hutumia njia hii ndefu? Ni kwanini asiombe dau tu na kumalizana fastafasta
 
STORY 2
Huyu tulikutana kwenye email
Nilikuwa namtumia yeye kuhusu kazi flani kwenye kampuni X
Sasa yeye alikuwa nje ya nchi
Tulitumiana email kadhaa kuhusu kazi baadae akachukua no yangu kwenye email
Siku sina hili wala lile akanicheki akajitambulisha vizuri tukawa tunachat ila hakupenda video call
Tukaenda hivyo hadi December 2018 akaja Tanzania akaomba tuonane
Nikajikoki mwenyewe vile naenda kuonana na mtu wa abroad asije kuniona wa kuja🤣🤣🤣
Tumekutana Capetown pale masaki
Mama weeee nilijuta
Kaka ni yupo very rough kavaa kama konda wa daladala za mbagala mchafuuu hutajua katoka German huko na PhD yake
Nilikuwa very disappointed maskini....nikaja kugundua ni mtu fulani amesoma sana hadi kama anapitiliza anazingatia sana mambo ya kazi kuliko vingine....nilishukuru aliniletea zawadi ya saa nzuri sana ninayo hadi leo....
Sikutaka kukatisha mawasiliano hadi ameenda German tunawasiliana hadi leo ila we don't date nilimdanganya Nina mpenzi 🤣🤣🤣
 
Baada ya kusoma visa vingi humu nimegundua Vijana mmerahisishiwa sana maisha ya mahusiano na TEHAMA.

Ukiwa serious, unaweza kupata Mke au Mume humu humu mitandaoni, muhimu mjue lengo la mahusiano yenu ni yapi.

Kuna wakati hadi natamani Umri ungerudi nyuma kidogo walau namimi nijaribu kutupia Vocal huko PM walau nipate cha kuhadithia, lakini kwa umri huu wa miaka 78 Mdada gani atakubali kukutana na Mzee wa Umri wangu, Mvi za kutosha kichwani, Sura ina makunyazi, na hii miwani yangu mikubwa ya macho jamani si atasema namtisha 🤪
 
Nlipataga mama humu moja
Comments za kipisi kali kingereza mingi
nikaona ewaa mtoto kaja Dm tukaongea mwsho namba zikatoka
Kwenda whatsap nkamtumia picha tufahamiane (that was a grave mistake)
Ving'ora vikaanza Wow wow wow
Kuja kutuma yeye nikabaki hiiiih
Sikuamini nkampgia video call La haula almanusura ntupe simu


Sjui yupo wapi saivi Aggy wa jukwaa la entertainment

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] best njoo umalizie story

Uliibuka na Mmongolii dadeq
 
Back
Top Bottom