Mahusiano ya Uganda na M23 na athari zake kwa usalama wa DRC

Mahusiano ya Uganda na M23 na athari zake kwa usalama wa DRC

Mahojiano hayo hapo chini yanatoa mwanga kuhusu hujuma za Uganda dhidi ya DRC.

Huyu Mzee M7 amekuwa mtu wa hovyo sana.
Atamaliza siku zake kwa kupoteza heshima aliyojijengea alipokuwa bado anazo akili nzuri.

Katika watu wasioaminika kabisa sasa hivi ni huyu, pamoja na "Bahima Empire"mwenzake.
 
..umeona eeh?

..M23 walishabamizwa na kutimuliwa DRC na vikosi vya SADC.

..Wakakimbilia Rwanda na Uganda na kupewa hifadhi.

..Sasa wamerudi kwa nguvu na ari mpya.
 
Chanzo cha hili tatizo naona ni hivi vi nchi vyetu visivyo na misimamo na kujiamini, inajulikana wazi miaka yote tatizo la DRC ni Uganda na Rwanda, lakini sioni jitihada zozote za maana zinazofanyika kumaliza huo mzozo wa miaka mingi.

Mfano, hao Rwanda na Uganda wapo kwenye jumuia ya Afrika Mashariki, mara nyingi hizo nchi hukutana kuzungumzia mambo mbalimbali yanayohusu hiyo jumuia, kwanini hili la DRC huwa halizungumziwi hata kama DRC sio mwanachama?

Kwasababu, kwangu haiwezekani uwe na jirani au member wa familia yako anayetuhumiwa kwa wizi na uporaji halafu humuulizi chochote, huku kama sio kumuogopa sijui ni kitu gani kingine, ndio sababu huwa sioni maana ya kuwa na hizi jumuia za kikanda.

Nachokiona sasa Uganda na Rwanda wamekuwa kama wababe wa hiyo jumuia, wanafanya uhuni kwa makusudi wakijua wazi hawataulizwa chochote na yeyote.
 
Kwa hiyo kama kenya imepeleka majeshi yake na juzi Tshesejedi kaja Bongo inamaana itakuwa tz+kenya vs Rwanda+uganda!?

Hatma ya EAC itakuaje!?

Kazi kweli kweli!
EeeenHeeee!
Kenya kapeleka majeshi yake, na hao hao M23 wanashangilia hatua hiyo?

Hapo hakuna kitu hapo mkuu 'Mwl Athumani', hizo ni hadaa tu za kutafuta sifa tu basi.
Hao wanajeshi wa Kenya hawana tofauti yoyote na hao wa Umoja wa Mataifa yaliyopo huko kwa miaka na miaka.

Ni wakati mwafaka sasa, Congo asimame mwenyewe kama taifa. AAchane na hii tabia ya kulialia kama mwanamke.
 
Kwa hiyo kama kenya imepeleka majeshi yake na juzi Tshesejedi kaja Bongo inamaana itakuwa tz+kenya vs Rwanda+uganda!?

Hatma ya EAC itakuaje!?

Kazi kweli kweli!
Nitashangaa sana Tanzania akikubali uhayawani huo.
Kwanza tayari tupo SADC, ya nini tena turukie kwenye hii jumuia ya wahuni?
Tubakie huko huko SADC na mchango wetu huko.
 
Nitashangaa sana Tanzania akikubali uhayawani huo.
Kwanza tayari tupo SADC, ya nini tena turukie kwenye hii jumuia ya wahuni?
Tubakie huko huko SADC na mchango wetu huko.
Hatuwezi kujitoa, ukitoa faida nyingi za kuwepo huko lakini moja ya hasara kujitoa ni kuipa Kenya nguvu zaidi kuwa na influence nchi hizo na sisi kupoteza kabisa. Bado tuna ushawishi nchi hizo lazima tusimame nao.
 
Huenda hukuelewa nilichokusudia.
Tuna wanajeshi wetu tayari wapo huko DRC, tukiwa chini ya SADC.

Sasa unataka tuchangie jeshi lingine tena tukiwa ndani ya EAC?
Mbona itaonekana kama 'comedy'.

Lakini hata katika hiyo maana uliyokusudia wewe, Kenya kuwa na 'influence' kutuzidi sisi katika eneo hili halina msingi wowote. Ni Kenya huyo huyo aliyejaribu kwa kila njia, kujitafutia 'ujiko' dhidi yetu wakati wa ile 'CoW', (Coalition of the Willing), unakumbuka? Hebu nieleze juhudi hizo zilifikia wapi!

"Sisi kupoteza kabisa" kama unavyosema wewe, ni viongozi wetu wasijue jinsi ya kushughulikia maswala haya ipasavyo. Nafasi yetu katika eneo hili hakuna anayetishia lolote juu yetu.

Unapoona Kenya anajirusharusha kila sehemu bila mafanikio yoyote, ujue nafasi yake ni finyu sana.
 
Samahani wakuu, tungeanzia hapa.....hawa M23 ni kina nani???

Sijui kama kuna ukweli, nasikia hawa ni Banyamulenge!, ..kama ni kweli, hawa ni wajukuu na vitukuu wa watusi waliokimbilia DRC kitambo na ni vizalia wa Congo, sasa basi kama mtu amezaliwa hapo, babake kazaliwa hapo na hata babu kazaliwa hapo, leo hii umwambie aende kwao na hapo si kwao! hapo sijui inakuwaje!!!
 
Back
Top Bottom