Mahusiano yenye changamoto za ushirikina na kulazimishana

Mahusiano yenye changamoto za ushirikina na kulazimishana

Festi mbuya

New Member
Joined
Mar 15, 2020
Posts
2
Reaction score
4
Hello habari, nina changamoto kidogo naomba msaada, mwaka jana mwezi wanane nilikutana na mwanamke na nikaanzisha naye mahisiano na sababu ilo fanya mahusiano yaendelee alipodai kuwa anaujauzito niliendelea kumsapoti nilipoweza mpka ulipofika mwezi wa kumi na mbili ambapo alidai ujauzito umeharibika.

Tulivutana kidogo nilitaka niachane naye bahati mbaya sikufanikiwa changamoto na ugomvi ulikuwa ni mkubwa sana mpka ulipo fika mwezi wa pili mwishoni nilipoona haya mambo yafike mwisho, mwanamke alikuwa anafanya kazi kwa mtu kifupi alikuwa ni msimamizi wa guest house.

Kipindi ujauzito unaharibika alikuwa na binti walio kuwa wanaishi naye kama mdogo wake alinambia dada anatumia madawa na anasema ukiondoka akikutaka lazima uje" toka mwezi wa pili mwishoni nilipo toka ilipita miezi miwili na sehemu mawasiliano yakiwa mabovu na mwishoni mwa mwezi wanne alipiga simu kuwa kaka yake amemtafutia kazi sehemu ambayo nilikuwa naishi na amemwambia atampangia chumba ko anakuja nilimjibu sitakupokea, siku aliofika alianza kupiga simu kuanzia saa nane mpaka saa kumi na moja.

Nikaingiwa na huruma nikaenda kumpokea, alivyofika nyumbani swali la kwanza utakuwa kwa muda gani alosema siku tano nikamwambia sawa siku ya tatu nilitoka kwenda mishe zangu wilaya jirani baada ya hizo siku kuisha nilipiga simu akanambia kaka yake bado hajakamilisha mambo yake amemuomba tena muda, huo mida ulipo fika nilipo mkumbusha tena alinijibu kuwa hana kwa kwenda hapo ndipo amefika.

Nikaamuwa nikatishe harakati zangu nirudi nikamcheki nilipofika tulipishana kauli hivo alichukua visu na kutishia kujiua nilitoa ripoti kwa mabalozi na mwenye nyumba wangu bahati mbaya mtaani ukawa umetokea msiba, ko tulishindwa kukalishwa wote msiba ulivyopita niliamua kurudi mishe mwezi wapili ukawa unaingia mtu yuko nyumbani me nikawa nimerudi tuligombana sababu nilimwambia nimpe nauli anipishe ndipo nikaamua kurudi kwa balozi amekaa na sisi aliongea nasi pamoja alituitisha kikao pamoja hivyo tuliamuliwa tufanye amani.

Sasa changamoto zinapo kuja kuendelea kaka yake mmoja na mwanamke ananitishia kuja kunipiga ndugu zake wengine wanadai kuwa akiondoka ni ujinga wake yeye na yeye anasema nilipokuwa namtongoza nilikuwa nategemea nini kwake nimeyatimba nikachezee wengine na mama yake anayemwa kuwa ni mganga wananamnia sitokuja kufanikiwa mishani

Naombeni ushauri kujuwa nilipo kesea na nini naweza kufanya kuepukana na huyu mwanake mambo yake ni ya hovyo sana siku nakagua bag lake la kuhidhia nguo ake nilikuwa kitu kimefingwa kwenye chupa ya pafyum nilipoongea na watu niliambiwa nichome tu.
 
Umeshayakanyaga tayari kama na damu mshachanganya. Pole sana huyo ni wako na kama familia yao ndio ipo namna hiyo utapata tabu sana.

Ogopa sana familia ambayo hata kwenye mambo ya kijinga wanasapotiana kwa kila namna. Na ikishakua familia ina shirki n hatari zaidi
 
Nguvu unazotumia kushinda naebona kazi ndogo, tafuta hela. Tafuta nyumba mahali pengine. Siku unakuja na gari unabeba vitu vyako unasepa. Unaacha nguo zake, na funguo unamkabidhi kwenye nyumba.

Ashakuona muoga atakupeleka kwelikweli hadi akili ikuruke. Haya maisha hayahitaji uoga ndugu, ukiamini unarogwa hata ukipiga chafya utaenda kuagua kwa kuhisi umerogwa.
 
Kwanini usiondoke kimya kimya, au unaogopa huko kurogwa?, Hivi huoni kuwa ukiendelea kuishi naye ndo majanga zaidi na nakuhakikishia ukioa kabisa ndo utakuwa mwisho wa maisha ya amani na utakuwa hovyo kisaikolojia na kimwili pia, ww unadhani wazee waliochoka mtaani walikuwaje ujana wao, ujana wao ulikuwa kama hivyo ya kukumbatia vinuka mavi na baadaye kujuta milele na hakuna wa kukusaidia. Kuwa mwanaume basi.
 
Back
Top Bottom