Mahusiano yetu bila Maxence Mello hayatadumu!

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Tumo humu kujadiliana mambo ya mahusiano kwa kuwa kuna mtu anaitwa Maxence Melo na wenzake usiku na mchana wanahangaika tuwe humu tena tukiwa salama. Melo kakamatwa na bado anashikiliwa na Polisi. Haya mahusiano yetu hayatadumu kama Melo ataamua kusalimu amri.

Sote tusimame pamoja kuzuia mahusiano yetu na Melo yasivunjwe!

[HASHTAG]#freemaxencemello[/HASHTAG]
 
tafadhali sana dada zetu tunahitaji sauti zenu mpendwa wetu melo anashikiliwa na polisi
 
Mimi naomba kujua tunasimama nae kwa maneno au vitendo? hv serikali itatusikiliza huku tukiwa tumejifisha nyuma ya computer tena kwa majina fake? mana sijaona anaesema tujitokeze tubebe na mabango yenye hii hashtag freemaxencemello twende hadi kwenye hicho kituo alipofungiwa
 
mimi niko tayari. weka mipango mezani tuitekeleze
 
nenda jukwaa la siasa utapata majibu ya swali lako ,siku moja moja sio mbaya kupitia majukwaa tofauti tofauti kidogo ya jf
Niliuliza kabla sijachunguza kidogo
Nimeshapata majibu
 
Yaani huwezi msaidia mtu kwa kuandika sijui mahash tag, hata uyaandike mara ngapi bila vitendo ni sifuri. Sawa na machozi ya samaki, kinachotakiwa ni mikakati ya vitendo na sio maneno matupuu. Majukwaa meengi nimepita maneno ni yale yale je kuna lililobadilika maana kuanzia akamatwe threads ni nyingi sana za kumhusu huku yeye akiwa hana uhuru sie tuko busy kuanzisha threads cha muhimu ni matendo sio threads na kitendawili ni hiki nani mwenye uthubutu wa kuonyesha vitendo????
Kila mtu anajihami hamna atakayetaka kujiingiza kwenye mdomo wa mamba kama yupo na aseme
 
Sky Eclat, hata mimi nataka kutetea ila cjui nifanyeje mkuu. Muongozo tafadhal
Kupambana kuko kwa aina nyingi, hata Mandela kupambana kwake ilikuwa ni kukataa "kuachiliwa" kama kuachiliwa kwake kulikuwa na sharti kwamba akitoka jela asijihusishe na mapambano dhidi ya Makaburu. Kuna watu wanadhani mapambano ni lazima tuingie barabarani tukiwa na mabango. Ni kweli lakini kwa sasa haijafikia kiwango cha kwenda barabarani lakini ikibidi tutakwenda.

Sky Eclat katoa hoja ya msingi sana, hapo ulipo simama kama ulivyo uwezavyo. Tukisema tuingie barabarani siye tulioko Iringa wenzetu wa Dar watasema kuwa tunawategea!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…