Pre GE2025 Maigizo Bungeni: Waziri Nape na viongozi wengine wakaribishwa Bungeni na Roboti Eunice

Pre GE2025 Maigizo Bungeni: Waziri Nape na viongozi wengine wakaribishwa Bungeni na Roboti Eunice

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hii nchi skuizi imekua na maigizo ya kipuuzi sana alooo......
Sasa hilo dude lina faidagani kwa mwananchi wa kawaida??
Tuliza makalio. Hiyo ndiyo teknojia ya habari inakokwenda kwa kutumia akili mnembe (artificial intelligence).

Kilichofanyika leo ni kitu kizuri sana kwa taifa letu kuonyesha utayari wa kwenda na technology. Usipojuhusisha nayo utabaki peke yako duniani
 
Kama kawaida yetu lina quality ya kitanzania kama ilivyokuwa Sanamu ya Kingwangallah.[emoji23]

Roboti haigeuki, iko fixed, mkono inasogeza direction moja tu na kurudisha. Yaani jinsi ilivyosetiwa ndio iko vile vile.

Si ajabu litakuwa kimepangiwa bajeti[emoji23][emoji23]
Bajeti yake sio chini ya B na kamati ilikaa
 
Ikiwa zamu ya waziri wa Utalii itakuwa vizuri nae akiweka hapo Simba na tembo na fisi , kuonesha uhalisia wa wizara yake. Ummy Mwalimu sasa sijui aweke nini
 
Mambo mazuri na ya fahari kwa sasa yanapachikwa lile jina pendwa.

Eunice "asilimishwe"
 
Huu ni ujinga kama ujinga mwingine tu na kuonyesha namna gani hatuko serious.

Halafu unaingia bungeni unaanza kutuambia 59% ya budget ni hela za wahisani.
 
Teknolojia ya mawasiliano kwa sasa imebebwa na mfumo wa AI au robotic kwa kiasi kikubwa, huduma za kujibiwa kwa robotic kwenye mawasiliano ndo tumeshaingia na dunia kugeuka kuwa kama kijiji, hivyo huyo robotic anatakiwa aondoe uoga kwa waTanzania na Waziri yupo Sawa kutuondoa uoga ili kujua huduma tunazotumia zinakwenda kuwa na mfumo wa dunia kama kijiji na wanaoweza kutoa hizo huduma masaa yote ni robotic maana binadamu anahitaji kupumzika, kwenda haja na wakati Huo huduma mawasiliano zinatakiwa kujibiwa masaa 24 bila kuchoka.
 
Hizo pesa za maigizo washushe bei za Bundle sio kutuletea midoli hapa huenda vijana wangekuwa na bundle affordable wangekuja na kitu cha maana zaidi ya hilo doli la kizungu....

 
Back
Top Bottom