Maini ya mnyama ni matamu sana lakini...

Maini ya mnyama ni matamu sana lakini...

Equitable

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2021
Posts
2,017
Reaction score
5,462
Nilikuwa napenda sana kula maini ya wanyama wote wanaoliwa . Yote yawe ya kuchemsha, kurosti au kuchoma.

Daktari mmoja alinikuta nakula akanishauri niache kabisa mazoea haya. Aliniambia kuwa " ini ndicho kiungo kinachopokea na kuchuja sumu ya chakula anachokula mnyama hivyo basi maini yanakuwa na sumu nyingi isiyofaa kwa afya yako". Nimevumilia siku nyingi ila leo nimeyamisi mno .

Wadau nipeni ukweli maana nikiyakumbuka hata nanii ikasome jinsi ninavyoyamisi.
 
Ninavyo yapenda siwezi acha kula aisee[emoji39][emoji39]
 
Nilikuwa napenda sana kula maini ya wanyama wote wanaoliwa . Yote yawe ya kuchemsha, kurosti au kuchoma.

Daktari mmoja alinikuta nakula akanishauri niache kabisa mazoea haya. Aliniambia kuwa " ini ndicho kiungo kinachopokea na kuchuja sumu ya chakula anachokula mnyama hivyo basi maini yanakuwa na sumu nyingi isiyofaa kwa afya yako". Nimevumilia siku nyingi ila leo nimeyamisi mno .

Wadau nipeni ukweli maana nikiyakumbuka hata nanii ikasome jinsi ninavyoyamisi.

Upate ya kitimoto sasa!!!!
Yana kauchungu fulani hivi amazini wee acha tuu
 
Kuna sumu mbaya kama papuchi???
Lakini walimwengu wanaichakata na wengine wanafyonza kama mlenda.

Usiamini kila uambiwalo. Kama ulikula miaka yote na leo unaandika uzi huu ndio ujue za kuambiwa changanya na za kwako.
 
Alisikika bi kikongwe m1 maeneo ya mnazi m1 hosp akimjibu daktari aliekua akimpa ushauri

Bibi: Kyaaa nyeee nimechoka Sasa na Kama kufa nife maana kila nikija Mara niache kula wali, Mara chipsi, Mara hiki Mara kile Nile nn Sasa nyama zenu... ??
 
Yanapokea sumu na kufanya detoxification..hivyo sumu inaondoshwa kwenye ini kupitia hepatic vein.

#MaendeleoHayanaChama
 
Hizi hsbari za uongo, wamadai wanayala kila siku hawajafa mbona
 
IMG_0865.jpg

1.husaidia kuupa mwili nguvu ya kutosha
2.huboresha afya ya ngozi
3.huimarisha afya ya mifupa
3.huimarisha afya ya moyo
4. Husaidia afya ya ubongo
5.chakula kizuri kwa afya ya misuli
6.huondosha sumu mwilini
7.husaidia kulinda mwili dhidi ya saratani
8.huupa nguvu mfumo wa kinga

NB: maini huuzwa ghali sehemu zote kuliko nyama ya kawaida.
 
Mmeandika. Ukweli utabaki kuwa elimu inazidi kuongezeka. Sayansi inazidi kupanuka. Uelewa unazidi kuwepo.
Kwa sasa yanayosemwa ni ukweli kuwa ndio uchunguzi wa kisasa.
Nani alijua miaka 50 iliyopita kuwa ugali, wali, viazi vinasababiaha mishipa ya damu kuziba? Nani alijua zamani kuwa chumvi inaongeza presha?
Zamani kukikuwa na vidonda ndugu. Kumbe ni kansa.
Ukweli utabaki ukweli kwamba twende na sayansi ya leo.
 
Back
Top Bottom