Kaunara
JF-Expert Member
- Feb 4, 2013
- 249
- 452
Habari wadau!
Naenda kwenye hoja moja kwa moja.
Kama mnavyojua maisha yanaenda kasi sana. Utandawaz naweza sema umeenea kila pande ya Dunia na hamna binadamu ambaye anakubali kuwa nyuma au jamii flani inakubali kuwa nyuma.
Maisha kabla ya mitandao namaanisha kabla ya mobile phone kuanza miaka ya 2000 kurudi nyuma ilikuwa ni rahisi sana kupata mdada wa kazi. Ilikuwa ni kazi ambayo wadada vijijini wanaigombania.
Miaka ya nyuma ilikuwa mtu akitoka mjini anakusanya kijiji anawasimulia mambo ya mjini. Kuna umeme mjini, kuna rami, maji yanatoka hadi choon, kuna tv kuna movies vitu ambavyo jamii za vijijini wengi walitamani kuona na kuishi.
Wengi waliamini hela na maisha vipo mjini tofauti na sasa. Kuna watu vijijini ni matajiri tena wakubwa sana.
Kuna maduka vijijini yanamtaji hadi mil 30 na kuendelea. Kubadilika huku kwa maisha moja kumeifanya jamii kujanjaruka sana na kuamini sehemu yeyote ile mtu anaweza toboa.
Wale wadada ambao miaka nyuma waliimini kijijini wanakotoka ni local sana kwa sasa hawapo. Wadada wa mshahara elfu hamsin kwa sasa hakuna utaishia kupoteza nauli kila kukicha.
Kuna wadada sasa hivi ni watalii Tanzania anakuja kwako wiki mbili anasema home kuna msiba anageuka. Anaenda mkoa mwingine na kuna madalali kabisa wa hizi mishe.
Shule za kata hazina performance nzuri sana ila zina mchango mkubwa sana vijijini na hata mjini. Kuna elimu mtu anapata kwenda shule achana na ya madaftali ila mtu akienda darasan miaka minne hawezi kuwa sawa na ambae kaishia darasa la tatu au la nne. Miaka ya nyuma wadada walikuwa wanaishia primary na wengine hata wasisome kabisa. Ivyo ilikuwa rahisi kumuaminisha chochote kile.
Sijasema wadada hawapo wapo ila wengi wanaokuja kufanya kazi kwa sasa nimefanya tasmini ndogo ila wengi wanashida kichwani hata familia kama inamtoa inasema sandakalawe. Maana hata kwao ni mzigo. Pili wengi wanakuwa na changamoto za kishirikina(Mapepo,Majini). Angalizo. Kama unapata mdada wa kazi maisha ya sasa hakikisha analala peke yake usimchanganye na watoto wako. Pia hata ndugu zako usiwaamini ukasema alale na mwanangu acha kabisa izo mishe.
Lazima jamii ibadilike sana kwa sasa wazazi mkiamua kuzaa mjipange jinsi ya kulea mtoto au watoto. Sasa hivi hamna binadamu ambaye anaweza kukulelea mtoto wako. Hadi kina bibi sasa hivi wengi hawataki habari za kulea. Namaanisha kwamba kila mtu anataka uhuru maisha ya sasa. Kila mtu anataka kuishi yeye kama yeye sio kupangiwa maisha na mtu. Kwaiyo jukumu kwa sasa la kulea mtoto wako ni wewe kama wewe.
Tumeshuhudia visa na mikasa mingi sana vya wadada wa kazi. Ila kama unaingia ndoani sasa hivi nakupa anagalizo tu jiandie maisha ya kuishi bila mdada wa kazi.