Maisha bila Mungu yamekuwa ya amani na furaha

Hata serikali itamzika, sijawahi kuona maiti inagaragara njiani
 
Bom tuu likipigwa unakimbia,Mungu muumba wa vyote akikutokea utasimama wewe!
Huyo Mungu hajawahi kutokea popote pale kwa vile hajawahi kuwepo, hayupo na hata uwezekano wa kuwepo kwake Haupo.

Mnahangaika sana kumwelezea na kumuongelea huyo Mungu kwa vile hajawahi kuwepo na hayupo kujiongelea mwenyewe na kujidhihirisha mwenyewe kwamba yupo.
 
Wajinga hawatakuelewa
 
Mkuu upo level ya OFFLINE (analogy) ulibakisha hatua kadhaa KUIFIKIA INTERNET ili kua ONLINE(digital),

Kijana huu ulimwengu unaouona hauishii hapa tu, kuna ulimwengu mwingine usioonekana kwa kumtumia hii milango mitano ya fahamu.

Kuna ulimwengu wa kiroho kufahamu huu ulimwengu hakuhitaji uwe umesoma Cuba/Akili kubwa/genius wala D mbili... kinachohitajika ni imani hata kidogo tu inatosha.

Nakupa mfano ingawaje haukidhi vigezo vya kuuelezea ulimwengu wa kiroho ila utakupa picha/mwangaza angalau.;

Chukulia mfano Binadamu ni kama kompyuta (mahsusi SIMU JANJA)

🔘ULIMWENGU WA MWILI NI (OFFLINE),

▶ Mambo mengi hapo yanafanyika physically vitu kama kusoma elimu, michezo, shughuli za kiuchumi na huduna mbalimbali, ni sawa sawa na kuandaa mafaili mbalimbali kama PDF spreadsheet, coding. Pia ku play file kama muziki movie offline pia vilevile kushare files mbalimbali kutoka simu moja kwenda nyingine kwa njia kama Bluetooth, USB CABLE etc


🔘ULIMWENGU WA ROHO NI (INTERNET)

▶ Huku kuna malango(sites) Kumbuka katika ulimwengu wa ROHO kuna wa Nuru na ulimwengu wa ROHO wa giza kila mmoja una namna yake ya kuingia Kutokana na dhamira ya madhabau uliyo jiungia. Sasa hii ni sawa sawa na Internet ambayo ndani yake kuna websites/tovuti tofauti tofauti zilizozidiana uwezo ulinzi na muundo tofauti tofauti kulingana na kazi yake.

Nyingine kujiunga bure zingine Zina-subscription fee, KYC, COOKIES, Zingine una-accept terms and conditions unaingia ndani.

🔘KUUJUA ULIMWENGU WA ROHO NI KAMA KUA (ONLINE)

▶ hapa kuna makundi Mbalimbali Kulingana na ulimwengu uliopo ulimwengu wa kiza ndio uchawi Uganga ushirikina freemasonry etcmajini.

Upande wa nuru huku tunatarajia kukutana na wachungaji mitume manabii shekh, malaika etc.

Sasa Mkuu... watu wengi wanaobeza uwepo wa MUNGU (Ulimwengu wa ROHO) yaani hawaamini Mungu yupo wala hawaamini uchawi asilimia kubwa watu wa aina hii wangekua simu(kompyuta) tungesema ni vifaa ambavyo havijawahi kupata access na INTERNET (DATA ZIKO OFF) SHUGHULI zao zote ni offline na ikitokea device imecollapse basi kwisha habali yake maana hakuna backup yeyote katika cloud storage system... Ukiwaambia kuna cloud computing yenye uwezo mkubwa huko katika Internet hawasadiki.

Watu wengi wanashughulika na mambo mengi wakiwa offline wamemaliza dadisi/tafiti na sayansi mbalimbali wakiwa offline na kuifikia hitimisho kua jambo hili haliwezekani kwakua huku offline silioni basi hiki kitu hakipo!!! My friend washa DATA Ingia mtandaoni yasiyowezekana offline, Online yanawezekana.
 
Ulimwengu wa roho ni sawasawa na ulimwengu wa kufikirika.

Ulimwengu uliopo ni huu huu unao onekana.

Hiyo "roho" ni dhana uchwara, iliyo pachikwa na wahuni wahuni tu.

Hakuna ulimwengu wa roho.
Fanya tafiti fupi tu ya kwenda huko nlikokueleza, Kajifunze mambo mapya ambayo hayakuwahi ku make sense kwenye ufahamu wako

( Jifunze kuwa mdadisi wa vitendo, Hapa Jf utabishana hadi siku utakapotoweka Duniani na usifike hitimisho )
 
Kama kuna ulimwengu mwingine usio onekana, Wewe uliuona wapi huo ulimwengu usionekana ukajua upo?

Kama huo Ulimwengu hauonekani, wewe uliwezaje kuuona?

Kama umeweza kuuona ulimwengu usio onekana, Huoni kwamba tayari huo ni ulimwengu unao onekana?
 
Unaweza kueleza ulimwengu wa kiroho kupitia biblia kama ushahidi?
 
Fanya tafiti fupi tu ya kwenda huko nlikokueleza, Kajifunze mambo mapya ambayo hayakuwahi ku make sense kwenye ufahamu wako

( Jifunze kuwa mdadisi wa vitendo, Hapa Jf utabishana hadi siku utakapotoweka Duniani na usifike hitimisho )
Ulimwengu ni huu huu mmoja.

Hata huo utafiti unafanyika kwenye ulimwengu huu huu unao onekana.

Hakuna. Ulimwengu wa roho wa kuufanyia utafiti.

Tafiti zote zinafanyika kwenye ulimwengu huu huu unao onekana.

Ulimwengu wa roho ni dhana uchwara, imaginations just an illusion.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…