Maisha bila Mungu yamekuwa ya amani na furaha

Maisha bila Mungu yamekuwa ya amani na furaha

Habari wana-JF!

Najua huu uzi wafia dini watausoma kwa kusonya ila ndiyo hivyo inabidi tuvumiliane tu.

Mimi nimekulia katika Ukristo, sijaukana ila nimeliacha kanisa kimyakimya. Baada ya kuanza kukua na kujitambua nilikuwa na maswali mengi sana juu ya nadharia zote kumuhusu Mungu na maswali yangu yote yalikuwa hayana majibu yaliyonyooka.

Baada ya udadisi wa muda mrefu nikafikia hitimisho kuwa "hakuna Mungu" kwasababu angekuwepo na majibu ya maswali yangu yangekuwepo.

Uwanda wa imani ni mpana ila ukiwa ndani ya imani chini ya tawi la dini ni mwiko kudadisi uwepo wa Mungu, huko ni "ndiyo" tu hakuna kuhoji.

Maisha baada ya kulikimbia kanisa yamekuwa na amani kwasababu:

1. Maisha yangu yapo mikononi mwangu.

2. Sina hofu juu ya kifo wala kuzimu kwasababu siamini hadithi za maisha baada ya kifo.

3. Naishi kwa kufuata katiba na sheria za nchi na si vinginevyo.

4. Siishi maisha kwaajili ya kumpendeza yoyote au kitu chochote.

5. Napata muda mwingi wa kufanya mambo ya msingi, siku ya Jumapili kwangu ni kama siku nyingine ya wiki.

6. Badala ya kuhangaika kutafuta maarifa ya maisha ya mbinguni (kusoma biblia), natafuta zaidi maarifa yatakonisaidia kwenye maisha ya hapa duniani maana ndiyo sehemu pekee ninayothibitisha ni ya kweli.

7. Najiheshimu. Kwangu kulia na kuomba msaada kwa M(i)ungu ni kutojiheshimu kama binadamu.

8. Nikipata matatizo sikai chini kuomba na kusubiri miujiza badala yake natumia maarifa niliyonayo kutafuta ufumbuzi.

9. Siishi kwa matumaini ya kuzawadiwa uzima wa milele.

10. Nimepishana na utapeli. Kama wanavyosema "wajinga ndiyo waliwao".

Siamini kama kweli Mungu yupo, lakini kama yupo hawezi kuwa mjinga kama anavyoelezewa kwenye vitabu vya dini.

Mungu hayupo, lakini kama angekuwepo hastahili utukufu wala unyenyekevu kutoka kwangu.

The sweet, sweet relief of knowing I'm going to hell no matter what I do! 🙃
Sawa mkuu,Hivi unavyoandika na hiyo pumzicunayovuta bure vyote ni Mungu kakupa!Ila maandiko yantuaminisha ipo siku kila ulimii utajiri.Pole ila umekamatwa na mnyororo,tupo wengi sana wewe hujamzidi Paulo.
 
Unathibitisha vipi pumzi tunayo vuta imetoka kwa huyo Mungu?

Au unafosi mawazo yako uchwara yasiyo na uthibitisho wowote ule?
 
Sasa mbona unaleta hadithi za wakristo?
Mimi nilisema bila kuwakilisha mawazo ya wakristo. Next time soma uelewa ndio ukosoe, napenda tubishana kwa jambo lenye mantiki.
Utaongeleaje upagani bila kuzungumzia ukristo uislamu na uyahudi?
 
Nahitaj kujua ni furaha gani umeipata baada ya kuwa na maisha ya bila Mungu??, Sema ni sawa kuwa na furaha kwa upande wako coz shetani ameweza kuvifanya vitu vyote ambavyo sio mapenzi ya Mungu kuwa vizuri sana l machoni mwa mwanadamu
Kwa upande wako unafuraha ? Na kama ndiyo ,,Mungu yupo? ambatanisha na ushahidi tafadhali
 
Utaongeleaje upagani bila kuzungumzia ukristo uislamu na uyahudi?
Ilitakiwa uniulize " unaposema pagani unamaanisha mtu gani?"
Halafu ukosoaji wako ufate baada ya kujua jibu langu. Otherwise uniambie hakunamtu mpagani ila kama yupo nimemaanisha huyo huyo bila kuleta tafsiri zingine.
 
Ashakupa location za kwenda,

Mimi naongezea nenda Gamboshi ndani ndani kule katest mitambo ukirudi utatueleza uliyoyashuhudia
Gamboshi sio ulimwengu wa roho.

Gamboshi ni eneo katika ulimwengu huu huu unao onekana na kuthibitishika upo.

Huelewi yanayotendeka Gamboshi kwa vile huna maarifa nayo. Ndio maana unadai Gamboshi ni ulimwengu wa roho.

Wana Gamboshi wenye utaalamu wao wanajua maarifa wanayotumia kwenye ulimwengu huu huu unao onekana ambayo wewe huna hayo maarifa ndio maana unadai kwamba ni ulimwengu wa roho.

Hakuna cha ulimwengu wa roho, sema wewe huna maarifa ya watu wa Gamboshi wanawezaje kufanya vitu kwenye ulimwengu huu huu unao onekana mpaka wewe unabaki kushangaa.

Kila kitu ni maarifa tu, Hakuna uchawi.
 
Kwani neno tunaposema "Ulimwengu we roho" wewe hili neno unaelewaje ?
 
Ilitakiwa uniulize " unaposema pagani unamaanisha mtu gani?"
Halafu ukosoaji wako ufate baada ya kujua jibu langu. Otherwise uniambie hakunamtu mpagani ila kama yupo nimemaanisha huyo huyo bila kuleta tafsiri zingine.
Mtoa mada ni atheist , ndio maana nimezungumza hivyo pia wachangiaji wanaounga mkono mtoa mada ni atheist ,bado nipo ndani ya mada mkuu.
 
Ukikua utaelewa hata huko kuniita uchwara umekosea sana,nakusikitikia,pili sikukujibu wewe,kuwa na adabu hata nusu kijiko.
Jibu hoja kwa hoja.

Acha kuleta Viroja na ku bwabwaja bwabwaja.

Naku uliza hivi, Unathibitishaje huyo Mungu anatoa pumzi?

Au unafosi mawazo yako uchwara yasiyo na uthibitisho wowote ule?

Jibu hoja wewe!!
 
Back
Top Bottom