Maisha bila Mungu yamekuwa ya amani na furaha

Maisha bila Mungu yamekuwa ya amani na furaha

Mkuu unachanganya dini na MUNGU mimi ninaamini Mungu hana uhusiono na dini ila dini ndio zinauhusiono na MUNGU.

Tatizo linaanza watu wengi wanapomfikilia Mungu wana refers katika dini walizokulia nazo

Dini zinanafasi yake lakini ukichanganya dini na Mungu lazima uchanganyikiwe kwasababu katika dini kuna sheria zilizotungwa na watu kwa utashi wao wakachanganya na mafunuo ya Mungu kupitia mitume na manabii.

Note: sizani kama kunamahali Mungu aliandaa mpango wakuleta dini. Hakuzindua dini yeyote....

Na kumjua Mungu sio lazima ufuate dini fulani, kinachotakiwa ni Upendo na Imani.
Very perfect
 
Pole sana ndugu, yatakapokufika ya walimwengu kumbuka kuwa YESU ANAKUPENDA, NA ALIKUFA KWA AJILI YAKO PIA.
 
Hivi, kati ya mpumbavu na mjinga ni nani anasema hakuna Mungu.?
 
Science inaendelea kurekebisha makosa aliyofanya Mungu mnayedai yupo. Mimi nilizaliwa na tatizo la macho (myopia) bila Science leo hii ningekuwa siwezi kuona mbali.
Mkuu naona umegusia myopia apo umeponaje ni kwa miwani au kuna namna nyingine...? Naomba kujua.
 
Shukrani Mkuu... Mimi mwenyewe nina tatazo hilo hilo, nikajua wanasayansi wamekuja na tiba mbadala.!
 
Nitarudi ila nimecheka sana huu uzi, kuna mabro mnajua kujenga na kutetea hoja zenu 🙌🙌🙌🙌
Igweeeeeeeeeeee 😹
 
Mkuu unachanganya dini na MUNGU mimi ninaamini Mungu hana uhusiono na dini ila dini ndio zinauhusiono na MUNGU.

Tatizo linaanza watu wengi wanapomfikilia Mungu wana refers katika dini walizokulia nazo

Dini zinanafasi yake lakini ukichanganya dini na Mungu lazima uchanganyikiwe kwasababu katika dini kuna sheria zilizotungwa na watu kwa utashi wao wakachanganya na mafunuo ya Mungu kupitia mitume na manabii.

Note: sizani kama kunamahali Mungu aliandaa mpango wakuleta dini. Hakuzindua dini yeyote....

Na kumjua Mungu sio lazima ufuate dini fulani, kinachotakiwa ni Upendo na Imani.
Huyo Mungu mwenyewe hujaweza kuthibitisha yupo.
 
Habari wana-JF!

Najua huu uzi wafia dini watausoma kwa kusonya ila ndiyo hivyo inabidi tuvumiliane tu.

Mimi nimekulia katika Ukristo, sijaukana ila nimeliacha kanisa kimyakimya. Baada ya kuanza kukua na kujitambua nilikuwa na maswali mengi sana juu ya nadharia zote kumuhusu Mungu na maswali yangu yote yalikuwa hayana majibu yaliyonyooka.

Baada ya udadisi wa muda mrefu nikafikia hitimisho kuwa "hakuna Mungu" kwasababu angekuwepo na majibu ya maswali yangu yangekuwepo.

Uwanda wa imani ni mpana ila ukiwa ndani ya imani chini ya tawi la dini ni mwiko kudadisi uwepo wa Mungu, huko ni "ndiyo" tu hakuna kuhoji.

Maisha baada ya kulikimbia kanisa yamekuwa na amani kwasababu:

1. Maisha yangu yapo mikononi mwangu.

2. Sina hofu juu ya kifo wala kuzimu kwasababu siamini hadithi za maisha baada ya kifo.

3. Naishi kwa kufuata katiba na sheria za nchi na si vinginevyo.

4. Siishi maisha kwaajili ya kumpendeza yoyote au kitu chochote.

5. Napata muda mwingi wa kufanya mambo ya msingi, siku ya Jumapili kwangu ni kama siku nyingine ya wiki.

6. Badala ya kuhangaika kutafuta maarifa ya maisha ya mbinguni (kusoma biblia), natafuta zaidi maarifa yatakonisaidia kwenye maisha ya hapa duniani maana ndiyo sehemu pekee ninayothibitisha ni ya kweli.

7. Najiheshimu. Kwangu kulia na kuomba msaada kwa M(i)ungu ni kutojiheshimu kama binadamu.

8. Nikipata matatizo sikai chini kuomba na kusubiri miujiza badala yake natumia maarifa niliyonayo kutafuta ufumbuzi.

9. Siishi kwa matumaini ya kuzawadiwa uzima wa milele.

10. Nimepishana na utapeli. Kama wanavyosema "wajinga ndiyo waliwao".

Siamini kama kweli Mungu yupo, lakini kama yupo hawezi kuwa mjinga kama anavyoelezewa kwenye vitabu vya dini.

Mungu hayupo, lakini kama angekuwepo hastahili utukufu wala unyenyekevu kutoka kwangu.

The sweet, sweet relief of knowing I'm going to hell no matter what I do! 🙃
Kuna kitabu kimoja kiliandikwa na mmama flan wa MAREKANI ukikisoma utajua kuwa shetani na Mungu wote ni akili yako, yani shetani ni akili yako na Mungu pia ni akili yako.

Usipoamini katika uchawi hautarogwa, ukiwa jasiri mbele ya hatari yoyote bas utakuwa mshindi tu lakini isiwe katika mazingira ya kujitakia et uende ukasimame katikati ya reli eti unasema mimi ni jasiri na train haitanigonga umekwisha.
 
Kwahyo mimi na wewe tunaobishana tu wajinga ?? Iweje tuwe na mawazo yanayolandana wakati huo tumeishi mazingira tofauti
Huenda utofauti huo ukawa ni katika harakati za ku balance mambo.
Dunia yenye watu wenye uelewa mmoja ndio unahisi ingekua perfect it means hata mambo ya biashara yasingetokea mana Ili biashara iende lazima ujinga wa mtu mmoja umfaidishe mtu mwingine
Dunia si perfect.

Haina usawa. Ina ajali za asili zinazoumiza na kuua wengi.

Hivi sasa kuna kimbunga kinakaribia Marekani kitaumiza watu wengi na kuharibu mali zao.

Wangependa kuishi maisha yao vizuri bila kusumbuliwa na kimbunga chochote.

Hapo utasemaje ulimwengu uko perfect?
 
Huyo Mungu mwenyewe hujaweza kuthibitisha yupo.
Ivi unajua kua hapo ulipo una Uungu ndani yako, ni vile tu hujapata namna sahihi ya kuudhihilisha.

Ama laa! Kuna concept moja sitaki kuiamini moja kwa moja ila kupitia wewe unanishawishi niiamini hiyo concept. Ambayo ni NPC (Non player Character).
 
Back
Top Bottom