Tumepewa hiari ya kuchagua (freewill) kaa utafakari zaidi kama bado unaishi
Hii freewill ni illusion tu.
Huchagui kuzaliwa au kutozaliwa.
Wala utazaliwa lini, wala utazaliwa wapi, wala utazaliwa na wazazi gani, wala utazaliwa na vinasaba gani. Hatuchagui bahati za maisha tu kwamba tutakutana na nani lini katika mazingira gani.
Hapo hakuna freewill.
Haya ni mambo muhimu sana katika maisha yako.
Mimi kuna wakati nilikuwa nabishana na rafiki zangu. Nikasema mimi ni mtu niliyejitahidi sana kusoma mambo mengi. Nimefanya kazi ya kusoma kujielimisha katika dunia yenye wavivu wengi, na hivyo hao wavivu wa kusoma wakishindwa kujua mengi, hilo ni kosa lao, na mimi kujua mengi ni matokeo ya kazi yangu.
Nikasema nimesoma library ya nyumbani, ninesoma Tambaza library, nimesoma vitabu vya library ya IST, nimesoma Tanganyika library, nimesoma British council na kwingine kwingi.
Rafiki yangu mmoja akaniambia hizo zote ni privileges tu. Akaniambia wewe umebahatika kuzaliwa na wazazi wenye elimu ambao wameweza kuwa na home library, umekuwa na access ya hizo libraries zote na kupewa muda wa kusema. Hizo zote ni privikeges zilizotokana na ajali ya kuzaliwa.
Ungezaliwa familia ya wakulima masikini huko Malampaka, usingekuwa na privileges zote hizo.
Nikafikiria sana kuhusu kauli ile, nikajikuta siwezi kujataa kuwa nimeweka juhudi binafsi kujielimisha, lakini pia, kama mtoto wa Oysterbay ambaye wazazi wangu walisoma, ambaye famikia yangu ina mabalozi kadhaa na ranking civil servants tangu siku za uhuru, kuna mambo mengi sana ambayo mimi naweza kuona nimefanya kwa utashi wangu lakini ukweli ni kwamba nineweza kufanya kwa sababu nimeshapeea pa kuanzia vizuri.
Yani hii habari ya freewill ni kama mtu anachagua movie ya Netflix kuangalia, akifikiri yeye ana uhuru wa kuchagua movie anayoitaka, lakini, hizo movies zenyewe anazochagua kashachaguliwa na Netflix, kuna movies hazipo Netflix, hata zikizopo Netflix kuna zike zinazoketwa juu na algorithm ya Netflix, nyingine ziko mbali sana hataziona.
Kwa hiyo hata pale anapoona anachagua movie kwa uhuru wake, uhuru wake mwenyewe hauko huru hivyo.