Maisha bora kwa kila Mtanzania inawezekana

Maisha bora kwa kila Mtanzania inawezekana

Masalu Jacob

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2017
Posts
1,446
Reaction score
1,645
Habari Tanzania !

Leo hii maisha bora kwa kila Mtanzania imekuwa ndoto na wakati mwingine inaonekana kama ni jambo lisilowezekana na hii ni chanzo cha aina ya watu na uwezo wao wa kufikiria.

1. Ujenzi wa Nyumba na Makazi ya kupanga yamekuwa aghali sana.
Njia: Punguzeni tozo na kodi kubwa toka kwenye vifaa vya ujenzi - mkumbuke hatukomoani tunajenga nchi yetu sote iwe wewe ni Kiongozi na wengine ni wananchi wachangia kodi.

2. Vyakula vichache na bei juu
Njia: Toeni punguzo la pembejeo na bima ya mazao kwa kila mkulima ili tuwape uhakika wa kazi zao; tupate vyakula vya kutosha mtaani kwa bei ya chini kila mmoja wetu afurahie hii nchi.

3. Mavazi imekuwa shida.
Njia: Tutoe fursa kwa viwanda vidogo na malighafi tupunguze urasimu na kodi ili pawepo na wingi wa mavazi, ajira na kuwawesesha uwepo wa viwanda vya nguo.

4. Elimu itolewe bure.
Njia: Elimu kwenye mfumo wa nchi yetu sio biashara na imekuwa ajabu na ufahari leo hii mashule na vyuo mnatoza fedha kiholela sijui nani aliwaambia kuna faida ya kuumiza watu namna hii. Watu wakipata elimu wataweza kuwa wabunifu, kujiajiri, kujilinda na kuishi kwa amani.

5. Afya sio sawa
Njia: Huduma hii na yenyewe iwe bure na huru kwa kila mwananchi achaneni na hizo mambo zenu za bima ya afya kwa wote. Yaani huduma ya Afya iwe bure 24/7. Wafanyakazi wa hii Sekta walindwe kwa wivu mkubwa.
Ukiwa na afya mbaya utapata wapi nguvu ya kufanya kazi; na wewe mtoza kodi utamtoza kodi mgonjwa asiyejiweza.

NB
Tukiyafanya haya, tutaondoa matabaka nchini na pia hatutakuwa na tatizo la watoto wa mitaani.

Karibu.
 
Maisha Bora yanawezekana pale tu CCM watatoka madarakani
 
Tatizo ni ubinafsi wa kujilimbikizia mimali huku wengine wanataabika na wenyewe (walojilimbika mimali) wanaona fahari
Hii kauli alishawahi itoa Ndugu Rais Benjamin Mkapa.
Kwamba Afrika inateswa na ubinafsi wa viongozi.
 
Back
Top Bottom