Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
you must be so naive kutokujua ndoa zote ziko hivyoo......
tangu utotoni mtoto wa kiume hafundishwi kazi za ndani kama kuosha vyombo kupiga deki etc.....mtoto wa kike ndio anambiwa afanye hivyo matokeo yake naye anajijengea hizo ni kazi za kike......sasa wewe leo uniambie wanaume wote hawako hivi nakushangaaa ni sawa uniambie nitafute sindano kny mchanga!
as you said diffrent strokes for different folks,so sidhani kama umeona ajabu sana kukutana na mtu ambaye anaoppose ndoa hapa...ni oppinion tu kama nyie pro marriage mlivyo!
Mimi mwenyewe kama nilivyosema sifagilii ndoa, lakini wanaopenda ndoa siwezi kuwakandya, wala siwezi kuikandya ndoa yenyewe, labda haifai kwangu na inafaa kwa wengine.
Tatizo wewe umekuja hapa na kuishambulia ndoa moja kwa moja kama haifai, halafu unafikiri kwamba ndoa zote ni za mfumodume.
Kati yangu mie ninayeacha room kwamba kuna baadhi ya ndoa hazina mfumodume, na wewe unayesema dunia nzima ndoa zote ni za mfumodume, nani naive?
Hujasikia kuna mama kaoa wanaume wawili katika ndoa yake, wote kawaweka ndani ya nyumba moja, hapahapa Tanzania. tena anawapa amri.
Sasa huyu naye utasema mtumwa katika hii ndoa? Na kama kuna huyu ambaye ana waume wawili, kuna wangapi ambao wana mume mmoja lakini hawataki wala hawaletewi mfumodume ndani ya nyumba?
Kukataa ndoa kwa sababu ya kuogopa mfumodume ni kutuambia kwamba huwezi kuchagua mwanaume atakayekufaa bila kukuletea mfumodume. Hili halituonyeshi kwamba wanaume hawa hawapo, linatuonyesha tu kwamba wewe umeshindwa kuwapata.