Mr sule
JF-Expert Member
- Oct 14, 2021
- 606
- 1,110
Habari JF
leo Katika mada yangu kichwa tajwa hapo juu, Ningependa nishare nanyi Uzoefu wangu wa maisha ya marekani, maana nimeona watu wengi sana wakijadili namna watu wanavyoishi nje, ajabu kati ya mia, tano tu ndo wanaelewa maisha halisi ya marekani.
Licha mimi huwa sipendi kuishi Marekani, lakini fursa zilizopo ndo zinatufanya tuelendelee kunganagia haya maisha, ndomana maisha yangu ya uwekezaji Yapo africa lakini utafutaji ni marekani kwa vile tu sijafikia malengo yangu ya maisha.
Miaka 6 ndani ya nchi ya marekani, ninaishi kwa Green card, nina ruhusiwa sasa kuomba uraia lakini mimi kwangu huwa si kipaumbele, maana nina uwezo wa kutoa na kuingia na kukaa nje ya marekani muda wa miezi sita.
Nimeishi majimbo na kufanya kazi kampuni tofauti tofauti, Mara nyingi nafanya hivyo tu ili kujifunza maisha halisi ya marekani. Mwaka jana nimefanya kampani saba na kuishi majimbo matatu. kufanya kazi marekani huwa nafanya tu kukaa bila kazi. nilichokifanya miaka minne ya marekani niliweka nguvu kuwekeza nyumbani jambo ambalo nilifanikiwa na kunipa huakika wa kuishi hapa bila kuwa na kazi.
Katika Harakati zangu za kucompare africa na marekani sehemu nzuri ya kuishi, niligundua africa kinachotufelisha ni uchumi ila ukiwa na pesa napendekeza kuishi afrca badala ya marekani. Marekani ni sehemu tu ya utafutaji ikiwa africa huna cha kupoteza(maono yangu)
MAZURI YA MAREKANI.
naipenda nchi ya marekani ni nchi ambayo inamuwesha kila mtu bila kujali nchi uliotokea kufanya lolote na ukafanikiwa, tofauti na nchi kama vile urusi, china. marekani ni nchi ya kila mtu kufanya anachoweza yaani nchi ya fursa. ukitaka kuwa doctoe, nurse nk.. hata kama umefeli elimu katika nchi yako marekani kuna njia nyingi za kukuwezesha ukarudi shule na ukatimiza ndoto zako.
Ikiwa ndo mara ya kwanza unaingia marekani, Kitu cha kwanza jifunze sana kingereza, kitu cha pili somea fani yeyote, cha tatu kuchuka Credit card. ukiwa na hayo matatu nchi ya marekani umemaliza mambo mengine yanakuja, na hayo yote inawezekana kufanyika kwa mtu yeyote anaishi marekani kihalali.
kazi na makazi, siwezi kushauri kuishi kwenye miji kama Chicago, New york, washington nk.. mara nyingi miji hii kazi zake ni professional. tena ina gharama kubwa ya rent. badala yake nenda kwenye majimbo kama dakota, kenctuky , mara nyingi ni kazi za viwanda au Entry job alafu rent iko chini.
Watu wengi kutoka nje ya marekani wanafanya ENRTY JOBS kutokana na lugha kuwa ngumu alafu pesa zinawachanganya hawataki kusoma.
Marekani kuna uraisi wa kumiliki nyumba gari na kufanya biashara unayotaka(biashara ya import chakula na kuuza kwenye maduka ya africa inalipa). hata kama huna huwezo huo. unaweza kutumia CREDIT yako na kupata nyumba, gari, au pesa baadae utalipa taratibu. kikubwa deal na Scores zako kuwa HIGH, na Credit ni kitu muhimu sana marekani.
Kazi ni nyingi na unaruhususiwa kufanya kazi masaa yote unayotaka hata kuwa na zaidi zaidi ya kumi, Mfano mimi nina ENTRY JOBS ndo always huwa nafanya kazi za aina hii, Kazi yangu ya Sasa Ni HMI CLASS tunatengenza class, nafanya kazi masaa 8 kila siku nalipwa $21 kwa saa na overtime $27, awali ilikuwa GE Appliance nilikuwa nalipwa $19, Before GE ilikuwa Fedex nilikuwa nalipwa $19.50, kabla ya Fedex ilikuwa Amazon $20.
Now kazi yangu ya sasa nafanya masaa ninayotaka nikisema kwamba nataka nipate $5000 mwezi huu inapatikana na gharama zangu za maisha ya marekani hazifiki hata $600(bills). So hapo nina kitu cha kufanya tayari africa. Imagine miez 12 ya kazi nikiruid africa huwez kusema tunarudi tumechoka.
Fursa nyingine ambayo kwangu huwa naona ni muhumu sana hapa marekani ni technology, Iphone ilipo marekani sio iliopo africa, chrome inavyofanya kazi marekani ni tofauti kabisa na africa, System za simu na Feature baadhi za Social Media ziko tofauti. kuna software kama vile Stripe huwezi kujiunga ikiwa unaishi africa, so mambo kama hayo ni muhimu sana na ni fursa kubwa.
Hat banl system ni tofauti kabisa zinavyotumika africa.
So kuishi marekani kuna fursa ya kuelimika pia, saivi ukimwabia banker maswala ya wallet pay, wireless pay, finger pay haya ni mambo mageni kwake au anasikiaga tu, ila wewe unaelimika kutoka na fursa ya mazingira unayoishi
ITAENDELEA.......
NO PM