Niwape usia mnaotaka kuzamia nje. Kwanza uwe na professional ingia hata veta piga ujuzi wowote tu udereva ni lzm. Piga capentry, nursing, umeme, ujenzi, nk.
Jifunze lugha kuu
Ingia nchi yeyeto kihalali, njia sahihi tumia gia ya kwenda kusoma Ili upate connection na wenyeji.
Ukifika kule usibague Kazi, tii sheria za nchi yaani mtu akikupiga shavu la kushoto mpe na la kulia kabisa.
Kuwa makini kabisa na masuala ya mapenzi, bora ukanunue kama umeshindwa funga zipu, wekeza Sana kwenye uaminifu na uchapakazi. Usifanye vitu haramu.
Fanya saving
Angalizo ni hatari sana kutuma pesa bongo sijui kwa ndugu Ili akufanyie maendeleo wengi wameonyeshwa misingi ya nyumba za watu.
Bora utunze pesa likizo ndo uje ufanye maendeleo, kuliko kujinyima eti unatuma home kumbe wenzio wanatumbua.