Tanzania tuna safari ndefu sana. Kikubwa tunahitaji kubadili fikra/mindset. Kuna watu wanaamini mpaka leo kazi ya serikali ndo yenye insurance. Ndo maana watu hawaishi kugombana na serikali waongezewe mishahara..ukiuliza hiyo nyongeza ni shillingi ngapi..hata 10k haifiki! Mimi leo na umri wangu sijawahi kupata kazi yenye mkataba wa zaidi ya mwaka mmoja (sifanyi kazi serikalini). Ila ukimwambia mTanzania anastuka anaona kama ni ndoto isiyowezekana. Yeye anaamini kazi lazima iwe permanent and pensionable :-0. Wakenya, wa-nigeria ni habari nyingine. Nature ya maisha imewafanya hustle ni sehemu ya maisha yao.
Watu wakiwa wanakunywa serengeti lite ya 1500 na kitimoto ya rosti kwa mama Kamche au Kimara.....wanadanganyana mengi sana kuhusu the so called fursa za bongo! Mfano; Uko kitaa cha makumbusho....unamkaribisha mshikaji unayemheshimu mbadilishane mawili matatu....pale brake point..unamnunulia beer za baridi na mchemsho wa kuku..akishiba na jasho limepungua ...anaanza stories zake..hivi vipi mbona
cassavaleaves harudi? anafanya nini US? aahh..jamaa mimi simuelewi.. Mwambieni bwana..maisha yapo bongo..fursa zipo hapa hapa.... ukimuangalia kiatu chake kimepigwa vumbi, na suruali yake ya Uturuki au ameshona mwenge kwa fundi maiko..... na maybe pembeni amepack Vitz au toyota Raum ya Japan ya mwaka 2005. Sasa unajiuliza huyu anaulizia maisha ya
cassavaleaves ili iweje? Kwani yeye hizo fursa hazioni? Na hapo mkiachana lazima akupige mzinga.
Pia wabongo wengi tuna kasumba ya tukose wote. Ndo maana stories za ufisadi bongo haziishi. ni kweli ufisadi upo, lakini kuna wengi wamekuwa victims tuu simply because wana maisha mazuri au wanaendesha magari mazuri/nyumba nzuri. Wamekwenda kinyume na utaratibu uliozoeleka.
Ukipata opportunities kwenda western countries kama US au Canada ukashindwa maisha..wewe huwezi kufaulu popote. Labda uingie kwenye siasa za CCM ambazo wizi na ulaghai umetamalaki.
On ending note: siku moja napiga story na jamaa yangu kuhusu life nje... nikashare naye fursa ya kazi ya mkataba wa six months ...akasema hawezi kuacha kazi unless mkataba uwe wa five years na kuendelea! Nikajiuliza hivi hii ni akili au ni tope kama la soko la mabibo?