Maisha halisi nchini Marekani

Maisha halisi nchini Marekani

Mimi mpaka leo naamini kabisa, kijana mwenye nguvu uliyechomoka kijijini ukaja mjini ukapata hii elimu yetu ambayo naweza sema ni half baked education (ambayo haikupi skills za aina yoyote-by the way siikandii hii elimu maana na mimi ni product ya mfumo huo huo...;-), kwa nini ushindwe kujiongeza kutafuta fursa nje ya mipaka ya Tz?. DAIMA TAMBUA, maendeleo ni juhudi binafsi. Ukiona akina Bavaria wanaongelea magari ya BMW au AUDI ya 100k USD wengine wanaona kama jamaa anajidai au ni utani! Lakini hivi ni vitu vya kawaida kwa wenzetu. Hivi kweli mshahara wa laki tano hardly dola mia mbili unategemea uendeshe BMW bila kuiba hela ya umma?

My point, is hakuna maisha marahisi popote pale. tunachokiongelea kuhusu US, Canada na kwingineko ni mifumo rafiki ambayo unaweza kuitumia ukapambana ukafanikiwa. Imagine bongo unafungua business. Ole wako DC au OCD waje kuomba/kuchukua hela ya mwenge au hela ya mafuta kufanya doria ukatae! utaundiwa figisu mapaka biashara zako zitakufa. Haya yote wote tunayajua na tumewaona victims wengi tuu. lazima ule na TRA! Kufungua kampuni tuu kuna utitiri wa regulators zaidi ya 30!

Kingine; watanzania tunachagua sana kazi. Nawajua watu wameenda nje kusoma..wamesafisha vyoo sana, wameendesha mabasi, wamedeki barabara sana, wamesafisha wazee sana (kazi zote ambazo wabongo wanaona ni za aibu watu wamezipiga na wanazifanya), but guess what? majority ya hao watu sasa hivi wanaishi maisha mazuri na ndo nguzo ya familia zao bongo! Hata humu wamo wengi tuu.

Hivi mnaposikia jamaa wamezamia mnaelewa nini? Kuna kazi nyingi sana za upishi na uyaya huko Middle East. Kuna kazi kibao za ulinzi huko kwenye mainchi yenye vita.....bongo ukiongelea kazi Saudi Arabia ya Uyaya watu wanakimbilia stories za kunyanyaswa nk. which I agree. Lakini pia, kuna success stories! kuna watu wameenda huko kutafuta maisha na wamefanikiwa vizuri tuu. Same na South Africa. Kuna ubaguzi na crime rate kubwa. Bongo watu wana-focus kwenye hizi changamoto. Lakini pia kuna success stories huko South haziongelewi! US watu wana focus kwa Trump na BLM wanachokiona CNN! Lakini mzee US ni nchi ya fursa dunia nzima! Ni ngumu kulielewa hili bila kuingia ukaona.

Kikubwa serikali iache umangi meza kutoa passports it should encourage its citizens waende nje wapate uraia na permanent residences! Hawa kesho na keshokutwa watoto wao utawakuta kwenye system na nafasi nyeti kwenye hizo nchi. Angalieni wahindi wanavyochomoza US...ukiangalia nafasi nyeti hata kwenye cabinet ya Biden kuna wahindi wengi tuu! its not by accident! angalia makampuni makubwa ya google nk...wahindi wamejaa! angalieni wanigeria. Angalieni wakenya. Usije ukashangaa mtoto wa mpiga box alikimbia bongo anateuliwa kuja kuwa balozi wa US Tanzania! Kwa wenzetu yote yanawezekana. Hawa ndo wanakuja kuwa mabalozi na kuzipigania nchi za wazazi wao.

waTanzania popote tulipo. Tubadilike na tubadilishe mindset!
Kazi ngumu sana kumbadilisha mtu midset,

Fear of unknown...

Watu wameridhika na kuzoea shida zao walizozizoea haziwapi tena changamoto...
 
  • Thanks
Reactions: Mit
Jamani inanisikitisha unakuwa job,halafu mtamtanzania peke yako.west kibao,wahindi ndo usiseme,wakenya nao.vijana wenzangu mnaotaka na nia ya kutoka tz,tokeni msiogope.ukiwa nidhamu na juhudi ya kazi lazima utoboe mpka ushangae.Asante masanja umemaliza yote!!
Uko wapi ? Je kuna wabongo uliwapa michongo wakazinguwa?
 
Uzi wa ukweli sana huu kwa tunaofikiri nje ya box mbarikiwe wote mnaotoa positive comments
 
Nina uhakika kwa zaidi ya 90% mleta mada hauishi marekani, ni hadithi zako za kutunga tunga. Nikikusoma between the lines naona wazi kabisa huijui Marekani. Kwa mfano:
1. Unazungumzia suala la Credit card kama kitu cha ajabu wakati ni jambo ambalo karibu kila mtu aliyepo Marekani anamiliki.

2. Unazungumzia issue za kusomea fani kama Udaktari kuwa ni issue rahisi na kawaida kwa mbongo kuweza kusomea akitaka akiwa Marekani wakati sio jambo rahisi kabisa ukiwa marekani.

3. Unasema umeshafanya kazi kwenye zaidi ya makampuni 7 ili kupata exposure tu wakati kiuhalisia huna kazi rasmi na unaishi kama kibarua tu, huku suala la ajira kwa US nalo limekuwa changamoto, na watu wanazisaka na hufanya kazi ili kuweza kuishi tu na sio their choice job.


4. Unasema mtu unatengeneza zaidi ya dola 5000 kwa mwezi lakini unaishi kwa dola 600 tu halafu hizo zote zinazobakia unazileta kuwekeza nyumbani Tz! Hizo ni hadithi za Abunawasi. Wakati kuna utitiri wa Diaspora hawana chochote Tz na hawana chochote US, wapo wapo tu, na siku wakifa huishia kuchomwa moto huko huko marekani.

5. Unazungumzia issue ya Green card kuwa unaimiliki as if ulikwenda marekani na kupewa au kuipata kama njugu, haki yako au uamuzi wako tu kuipata. Wakati kiuhalisia Green card ni mchakato mrefu, na karibu kila mtu anausaka huko Marekani na wachache hubahatika.

6. Unasema ukiwa US ni rahisi kumiliki nyumba! Huu ni uongo wa 100%. Hivi Diaspora wangapi wanamiliki nyumba marekani?
Liongo hilo mkuu
 
Hivi mbona mmoja wenu huko akifariki huko Kusafirisha Mwili tu huwa ni Shughuli Pevu.?
Bakuli La michango linatuhusu mpaka huku Kwa Mtogole.!
Halafu Mkifiwa na Mzazi Utasikia Mtoto Kashindwa Nauli Kuja Kumzika Mzazi Wake..! Hivi Diaspora Tuelezeni shida nini?
Mi mwenyewe nilitaka Kuja kuwa Diaspora ila ninachokishuhudia Kinachowatokea huko nimeghairi..!

Katika Diaspora 20 ni Wawili au Watatu ndo Wanatoboa.
aina tofauti na mei niliembetia baryern leo
 
Mkuu kwani uliwachangia? Mbona una hasira sana na fedha za watu na matumizi yao?
Nimeuliza tu mkuu wala sina hasira. Na ni kutokana tu na mtazamo wangu kuhusu kifo kwa ujumla; na baada ya hapo.

Ukishakufa ushakufa nyingine zote mbwembwe tu. Nimeshaandika na wosia kabisa kuwa nitakakofia basi nizikwe huko huko na hakuna haja ya kuingia haya magharama ya kusafirisha maiti. Na nizikwe na mtu mmoja, mia au nitupwe porini au majini kama Osama wala haijalishi. I am dead! Cha muhimu ni nimeishije maisha yangu hapa duniani na nimejiandaaje kwenda huko niendako!
 
Haya ndio mabox....Sibebi kichwani, si sogezi hata kidole, ni fork lift tu..I can go to Disney...I bought a house...send my kids to Colleges..driving a car of my choice...na kutoa support hapa na pale ndugu zangu wanasumbulia na Ada, au kupigwa mapanga na panya Road! Part time nasoma vitabu na articles malicious mbali to keep my brain sharp! Maana kazi haina kutumia brain.
Mkuu uliingiaje USA kama hutajali nataka kujua.
 
Juma Lokole huwezi kuthibitisha kama wanabanduliwa
Duh, Tanzania hii hii? Hata Bob Junior naye si riziki nini? Nimemwona kwenye clip moja anavyojishebedua! Vijana wa Tz wameharibika!!
 
Duh sio sehemu nzuri ya kuishi kama huna kazi ya kueleweka nina uzoefu napo pia
 
Back
Top Bottom