Maisha halisi ya Watanzania waishio hapa Afrika Kusini

Maisha halisi ya Watanzania waishio hapa Afrika Kusini

Pretoria kuna chimbo kama hilo la CHEECY linaitwa CAPITAL INN
Pretoria sijapiga sana misele lkn ni sehemu moja tamu sana kwa kuishi, hakuna watu wa hovyo hovyo kama Jozi, hakuna uchafu na harufu za kienyeji, pamepangiliwa vizuri na pia hapajabanana na population bado iko chini. Hilo chimbo ntalizukia weekend japo sitegemei kukutana na wabongo wengi.
 
Duh mimi huwa najua wenzangu waliozamia huko maisha yamewanyookea kumbe wanaishi kidananda ngoja niendelee kukomaa hapa hapa kijijini mbaka kieleweke.
76a323c43abe0156c856657576c06a14.jpg
 
Pretoria sijapiga sana misele lkn ni sehemu moja tamu sana kwa kuishi, hakuna watu wa hovyo hovyo kama Jozi, hakuna uchafu na harufu za kienyeji, pamepangiliwa vizuri na pia hapajabanana na population bado iko chini. Hilo chimbo ntalizukia weekend japo sitegemei kukutana na wabongo wengi.
Yap,hata mimi nilikaa kama wiki mbili tu,lipo not far from 244 Hotel.ni pazuri kurelaxisha akili
 
Big up mkuu yaani kweli research umeifanya vzr sana...
 
Ontario..

Inamaana huona mbongo yeyote Mwenye life la uhakika?
Juma3 ya week iliyopita nilienda kwenye ibada kanisa la Shepherd Bushiri ana huduma inaitwa 'Diplomatic service'. Nilibahatika kupata VIP seat, na baadae nikaja kugundua jirani yangu mmoja anasali kwa kiswahili hapo kanisani.

Alikua ni binti mmoja kanawiri haswa. Sikumfatilia sana, tuliongea tu juu juu, nikaamsha zangu maana ibada iliisha saa 7 usiku. Lakini yule dada alionekana kaotea life.

Pia sijui kama umesoma hapo nikiwa pretoria restaurant. Ni vizuri ujitahidi kusoma kitu ili uelewe, si kusoma ili ucomment.
 
Aksante mtoa mada..yote kwa yote nitabaki hapa hapa Mwanza The RockCity nikiendesha taxi mjini huku nikilima matikiti yangu na biashara za hapa na pale bila kumuibia mtu mpaka nitoke kimaisha.ukweli maisha mazuri yapo hapa hapa Tanzania.swala ni kupambana kwa bidii tu.wako jamaa zangu watatu walienda America kwa nyakati tofauti lakini wote walikaa huko wakifanya kazi zaidi ya miaka 7 mpaka 8 na walichorudi nacho ni mikogo tu ya kutembea na kuvaa miwani za kupunguza mwanga basi.mwingine atarudi mwaka huu kama MUNGU atamjalia.maisha yapo mahala ulipo,sema tu itategemea unatafutaje na kwa bidii ipi.unaweza kukaa nje miaka mitano ukifanya kazi ya kumwagilia bustani huku mshahara wote ukiishia kwenye pango na chakula,ktk miaka hiyo mimi huku Mwanza ntakua nimevuna shamba langu la mapapai kama mala 10 hvi huku nikifunga renta ya nyumba ya pili kwa uwezo wa muumba.
I am proud to be an Tanzanian
 
Wengi wanaishia kupiga picha kwenye majengo marefu kisha wanazituma.
Siku akirudi cha maana walichobeba ni simu na cheni za silver kisha wamepauka. Alafu waliokaa muda mrefu South Africa wakirudi wanakuwa hawawezi kabisa kuishi TZ .
 
Maisha nipopote changa karata zako vizuri utafanikiwa hata euro kunawatu wamechoka Mimi tabaki bongo ili mradi mambo yangu yaugari kwamaharage poa lakini kuna siku nakula nyama
 
Kama wananisoma hapa naomba warudi tuje tulime huku maeneo yapo mengi tu.
Ni wengi sana wanatamani kurudi
Ila uwezo hawana,


The more city inavyozidi kuwa modern ndio the more social and economic evil zinaongezeka.

Wale bushmen akina Xi wana maisha mazuri saana kule kijijini kwao kuliko wanaoishi hapo downtown kwa madiba.

Thank God! Sijawahi kuwaza kwenda south, napiga hela nyeupe za bila jasho kwa wauza Maharage hapa karagwe.

Easy money!
 
Back
Top Bottom