Maisha halisi ya Watanzania waishio hapa Afrika Kusini

Maisha halisi ya Watanzania waishio hapa Afrika Kusini

Huwa najiuliza,inamaana huyu jamaa watu wa vetting hawakumuona au? The guy seems to be with higher IQ.
 
Uliyosema yote ni kweli. Mimi niliishakaa Jobeg (Johannesburg) eneo la westonaria miaka 2. Nilikuwa nazuka mitaa hatarir kama ya hilbrour, n.k, ni hatari
Hillbrow
 
Wengi wanaishia kupiga picha kwenye majengo marefu kisha wanazituma.
Siku akirudi cha maana walichobeba ni simu na cheni za silver kisha wamepauka. Alafu waliokaa muda mrefu South Africa wakirudi wanakuwa hawawezi kabisa kuishi TZ .
Daaah! Kuhusu waliokaa sana SA, na kushindwa maisha wakirudi Bongo.... Ni kweli kabisa. Nina Mshkaji wng alikaaa Cape Town 12 years! Aliporudi! Alirudi na computer monitor 3 na CPU moja! Tangu amerudi dish lake halina uhusiano mzuri na decoder
 
Pretoria sijapiga sana misele lkn ni sehemu moja tamu sana kwa kuishi, hakuna watu wa hovyo hovyo kama Jozi, hakuna uchafu na harufu za kienyeji, pamepangiliwa vizuri na pia hapajabanana na population bado iko chini. Hilo chimbo ntalizukia weekend japo sitegemei kukutana na wabongo wengi.
Nenda machimbo ya Hillbrow, Jozi.
 
Daaah! Kuhusu waliokaa sana SA, na kushindwa maisha wakirudi Bongo.... Ni kweli kabisa. Nina Mshkaji wng alikaaa Cape Town 12 years! Aliporudi! Alirudi na computer monitor 3 na CPU moja! Tangu amerudi dish lake halina uhusiano mzuri na decoder
😀😀😀
 
Na bei yao ni sawa na mahindi mawili ya kuchoma hapo mtaani, yani walikua wanajiuza short time kwa Rand 24 (hii ni sawa na 3,800 Tsh).


Kumbe mahindi ya kuchoma dar yanauzwa 3,800/- , wakati huku kwetu muhundi mmoja ni 200/- nimcheka kifala[emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kitaeleweka tu
Duh mimi huwa najua wenzangu waliozamia huko maisha yamewanyookea kumbe wanaishi kidananda ngoja niendelee kukomaa hapa hapa kijijini mbaka kieleweke.
76a323c43abe0156c856657576c06a14.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sandile kwakweli katusikitisha sana jamii ya traders, sasa hivi traders wote tunaonekana ni 'psychopaths na sociopaths'. Nina uhakika Sandile alikua drug addict kwa muda mrefu.

Boss, you must learn this thing. It's a holy grail. Si ngumu sana kama unavyodhani, unahitaji dedication na right mentorship. Ukiwa makini na optimistic wala hautatumia muda mrefu sana, unaanza kujichotea USD na GBP. Sisi hua tunasema "Kudownload pesa".
Naona ulidownload pesa haswaa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uongo! Ulitembelea maskini.
Kwani wote bongo matajiri?
Oyaa masela maisha popte nenda tu ukipata nafasi na hakuna kurudi mpaka kieleweke.yeye mbona kaenda? Shit!
 
Stori kama ni halisi mbona pocha zechukuliwa Instagram au simu ya mtunzi haikuwa na Camera??![emoji38][emoji38][emoji38][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji377][emoji377][emoji377][emoji2445][emoji2445][emoji2445]

Cᵃʳᵉᵉᵐ ₜₕₑ ᴸᵉᵍᵉⁿD
 
Salute!

Nakumbuka mara yangu ya kwanza kuingia Afrika Kusini ilikuwa mwaka 2015, nikiwa chuo mwaka wa 2. Kuanzia hapo safari za kwenda huko Bondeni zikawa ni za mara kwa mara. View attachment 510219

Lkn kwa bahati mbaya, mara nyingi nilivyokua naenda huko sikuwa na muda wa kutosha sana kuzunguka na kuiona Afrika kusini katika 3 dimensions. Mara kadhaa nilikua naenda Johannesburg na kuishi sehemu 1 bila kupata fursa ya kuzama downtown, na maeneo niliyokua nafikia ni yale ambayo hayana purukushani kama Sandton, Roodport, Midrand na Melrose Arch. Na hata muda ulikua very much limited.View attachment 510225Sandton City Shopping centre.

Tarehe 11 April nikaja hapa Afrika Kusini kwa ajili ya shughuli zangu kadhaa, safari hii ambapo nimemaliza chuo na nipo huru, basi nikaplan nikae hapa kwa muda mrefu zaidi hadi May 23. Na moja ya vitu vilivyonisukuma kukaa huku muda mrefu ni kujua hali ya maisha ya Watanzania wenzangu wa hapa, nikiamini kua kwa namna 1 ama nyingine ningeweza kujifunza mbinu kadhaa za kupambana na haya maisha.View attachment 510227Nikiwa safarini kuelekea Jozi.

Midrand

Siku niliyofika mwenyeji wangu alinichukua na kuniacha hotel hapo Midrand, kisha yeye akaelekea kwake Pretoria.View attachment 510231Mall of Africa - nahisi hii ni mall kubwa zaidi Afrika, maana nilipotea mara kadhaa humo ndani.

Nilivyosettle nikaenda restaurant ya jirani kupata dinner, sasa nilikua nimeingia instagram, nikawa natazama video ambayo ilikua ikiplay kwa kiswahili. Kuna jamaa kama meza 2 au 3 mbele yangu akawa ananitazama sana, nikagundua yule bwana anafahamu kiswahili, lkn sikuweza kuconfirm kama ni Mtanzania, Mkenya, Mkongo ama vipi. Akaondoka zake mimi nikabaki nakula, nilivyomaliza kula nikapata wazo la kubadili sim cards, hivyo nilihitaji kwenda kusajili line ya Telkom SA na Cell C.

Very coincidentally, nilivyoenda kusajili Cell C nikamkuta yule bwana pale. Hata alivyoona passport yangu bado Hakutaka kujitambulisha, lkn kadri alivyozidi kuongea kingereza cha kuunga unga ndipo nikagundua yule jamaa ni Mbongo. Sikukutana na Mtanzania mwingine hadi naondoka Midrand.

Pretoria

Muda wote nikiwa Midrand, trips zangu zilikua za kwenda Pretoria, sikuwahi kukutana na Mbongo yeyote hadi siku nilipoenda Tanzanian restaurant. Kwakeli hata watumiaji wa hile restaurant walikua ni waAfrika kusini, kuna mdingi mmoja alikuja na familia yake yeye na mkewe walikua wakiongea kiswahili, mzee alipaki E- class Mercedes benz na alikua na card nyeusi ya FNB Bank (hii card inamaanisha mtu ana zaidi ya Rand mil 1 kwa account).

Johannesburg

Baada ya siku kadhaa nikaenda kuishi Johannesburg maana hapo pia nilikua na shughuli nyingine ambayo inajitegemea tofauti na ile ya Pretoria, ikawa kuishi Jozi kungenirahisishia usafiri.View attachment 5102561 ya vivutio vya Jozi

Melrose Arch

View attachment 510246mtaa wa QwaQwa, Melrose.

Nilifika hapo Jozi hotel 1 inaitwa Blu Swan, siku ya Ijumaa jioni, nilikua nina weekend yote kurelax then j3 pilika pilika zianze. Nakumbuka siku ya Jumapili jioni, kukawa kama na majibizano, vyumba kadhaa kutoka chumbani kwangu. Sikutilia maanani sana.

Lkn baada km ya nusu saa majibizano yalizidi, nikasikia watu wakitembea kwa veranda, wakasimama karibu na mlango wangu. Nikategesha sikio vizuri, kuna mmoja alikua anajaribu kupiga simu, akaweka 'loud speaker'. Ile call ikaleta sauti ya mhudumu wa Voda "Namba unayoipigia haipatikani kwa sasa...". Nikajua fika huyu ni mbongo, nikatoka nje ya chumba changu ili nione nini kinaendelea.

Majibizano yale yalikua kati ya security wa hotel na huyo jamaa. Alikua kjn mdogo km wa miaka 25 hivi, kilichokua kikiendelea ni kua huyo dogo alikua anafukuzwa atoke pale kwa kushindwa kulipa pesa ya hotel.

Nikatumia uungwana, nikamuomba huyo security aachane nae mimi nitamlipia kwa siku hiyo. Nikaingia ndani nikachomoa Rand 780 nikamlipia huyo dogo. Baada ya kuSort out ile ishu, tukawa na majadiliano nae. Dogo alinambia vitu vya kusikitisha sana.

Ni kwamba, alikua ana siku 2 tangu aingie SA, alikua ametumwa na Boss wake. Kwa maelezo ya dogo ni kua Boss wake anaitwa Jumbe, ni mdau wa Ilala mtaa wa Arusha. Dogo alipewa mzigo aje nao, alikua na mabegi mawili. Kisha akifika SA atakutana na mwenyeji wake ambae atamwachia huo mzigo, baadae atapewa pesa ya kujikimu na nauli ya kurudi Bongo.

Dogo alivyokutana na mwenyeji wake, akamkabidhi mizigo, kisha akapelekwa hotel akalipiwa siku 1 then yule mwenyeji wake akaondoka mazima. Dogo wala hatambui nini kilikua kwenye hayo mabegi, ambayo alidai yalikua madogo ya mgongoni. Kutokana na njaa aliyokua nayo dogo, nikaamua tusile vyakula vya hotel, tukaenda kugonga vyakula local. Dereva akatuendesha hadi Carlton Centre.

Carlton Centre

Kusema kweli sijawahi kua na real experience ya Johannesburg hadi nilipofika hapa mitaa ya Carlton.View attachment 510254muonekano wa Carlton kutoka Jengo maarufu sana la Transet.

Tukafika Simmonds Street, tukapata mgahawa tukaagiza Pap (huu ni ugali) na manyama, ilikua km Rand 40 kwa sahani 1. Baada ya kumaliza kula tukarudi hotel. Keshowe yule dogo akasema kua ni bora akajichanganye kitaa, maana hata passport hakua nayo, ilikua kwenye mabegi aliyompa mwenyeji wake, mimi nikamtakia maisha mema nikamwachia Rand 500.

Wakati tupo hapo Carlton nikagundua kua pako busy sana, hivyo nikapenda nitumie muda kupaelewa zaidi. Baada ya kumaliza ishu zangu za Melrose, sasa nikahamia Carlton Hotel. Nilipofika huku ndio nikapata hali halisi, maisha halisi ya wabongo wengi wa SA.
Kuna muhudumu wa hapa hitelini akatokea kua jamaa yangu sn, hivyo kila alipomaliza zamu yake, alikua ananitembeza mitaa ya Carlton.

Mitaa ya Carlton ambayo sikumbuki majina

Huku kwa kweli nilikutana na wabongo wengi, japo nilikua naficha identity yangu, maana nilishatahadharishwa kua wahuni ni wengi.View attachment 510257Gandhi Square, eneo maarufu hapa mitaa ya Carlton Centre

Wabongo wengi niliwaona wapo kwenye kama vikundi, yani kuna sehemu katika mtaa unakuta watu wote wanaongea kiswahili. Haya yalikua maeneo duni sana, machafu, yananuka kila aina ya harufu. Wabongo wengi walikua ni vibaka, wanategeshea kwenye zebra cross ambayo msongamano wa watu ni mkubwa sana. Kisha wanawazonga watu, na kuwakwapulia mali zao kwa staili ya Chadema.

Nilijibanza sehemu ili niusome mchezo, kwakweli wadada na wamama walikua wanalizwa sana. Simu, hela, vipochi, wallet. Wengi wa hawa wabongo walikua kama mateja, wamechoka sana wanapolala ndio hapo hapo wanapokojoa.

Polly street na Marshall street

Hii mitaa nilikutana na wabongo wengi sana wanaunga unga maisha, wamekata tamaa kabisa.

>Kuna majamaa wawili walikua wanatembea mtaani wamebeba maboxi kama subwoofer wanazungumza. Jamaa mmoja akamuuliza mwenzie - hivi Ally umemuona hivi karibuni, yule mwenzie akajibu - alli si yupo kwa yule muhundi. Jamaa akamjibu tena - dah jamaa kaotea sana maisha. Wale majamaa ghafla wakaingia kwenye duka fulani na hile mizigo. Nahisi ilikua ni mali ya wizi sasa wanaenda kuuza.

>Hapo hapo polly street kuna jengo limechakaa kiasi, hata sikuweza kulitambua kwa jina. Pale wadada walikua wanajiuza kuanzia asubuhi, mchana, jioni hadi usiku, yale kuuza mbunye pale ni kama kuuza mtumba Karume. Na bei yao ni sawa na mahindi mawili ya kuchoma hapo mtaani, yani walikua wanajiuza short time kwa Rand 24 (hii ni sawa na 3,800 Tsh). Hapo wanapojiuza tulikaa kama dakika 15 hivi, nikiwa hapo nilisikia sauti ya mdada yupo ndani anaita "Fetiii fetii njoo mara 1". Nikajua wazi hayo maeneo yana wabongo wengi sana

>Kuna mtaa fulani wa Fox street iliyochoka kuna frame nyingi sana za saloon. Kule saloon inakuwa na huduma zote za kike na kiume. Jamaa yangu akanipitisha hayo maeneo, kuna sehemu tukasimama kununua matunda. Hapo nilimsikia kinyozi mmoja anamkaripia mwenzie "Oyah kula vichwa, kula vichwa. Changamka huoni wanakupita." Hapo nikajua kbs ni mtaa wa wabongo, nikaingia kama kuzuga kunyoa ndevu.

Mule niliwakuta masela wengi sana wamejazana wakiwa hawana mwelekeo, vinyozi ni wa 3 tu na wadada wa kusuka wawili na jamaa mmoja wa kuchora tatoo. Kunyoa pale bei ilikua R15.

Cheeky tiger, diplomatic hotel na patapata Cuisine

Tukiwa tunakatiza mitaa jamaa yangu akanipeleka hapo cheeky tiger. Tukapigwa search pale getini, kisha tukalipa R5 kila mmoja. Jamaa hakuniambia nini kinaendelea, tulipoingua ndani kidogo nikate kauli (hahaha hahaha).

Mimi sijawahi kuona strippers live, nilikua nawaona kwa movies tu, sasa hapa niliwaona live. Yani wadada wanasasambua uchiii, mtu anaenda anamtunza hela labda Rand 50 au 20 au hata 10, akifika hapo anashika shika mzigo anapima wese na kubambia pia.

Humo ndani kuna wadada wengi mno, wakiwa wamevaa nusu uchi, wengine bikini huku juu wakiwa wazi. Mwanzo nilikua nnina hofu sn, nikawa najihisi guilty mno, jamaa yangu akanituliza. Nakumbuka hii ndio ile weekend Arsenal alimchapa Man Utd 2-0. Game kipindi cha kwanza chote tulicheki hapo, baada ya kupata ujasiri nilimwita mdada mmoja hapo nikawa namdadisi. Alianza kuniongelesha Kizulu nikamkatisha haraka sana, tukaswitch into English. Pale short time ni Rand 60-70, yule dada nikampa 50 ili tupige story.

Alichonielezea pale wapo wadada kama 160, kila ukichukuliwa kwenda kusafisha rungu basi Rand 20 ni ya mwenye Cheeky Tiger afu Rand 50 ndio ya mwanamke, kwasiku anapata hadi wateja 50. Na alinieleza na kuniitia watanzania wawili, wengine hakuwaona. Ni wadada mashine haswa hawa wabongo, walipogundua mimi ni mbongo walinichangamkia sana.

Mechi ilivyoisha tukaenda tena sehemu inaitwa diplomatic hotel. Hapa sasa ni kama mara 2 ya cheeky tiger, wadada ni wengi mno humo ndani japo wao kidogo hawapo uchi sana, na bei zao ilikua ni Rand 50. Hapa sikuongea na mdada yoyote lkn nilisikia mdada mmoja mwenye lafudhi ya Zanzibar akisema "naomba unisogezee hiyo tishu". Yani haya maeneo kuna uchafu vibaya mno. Natamani ningeshare picha, lkn naheshimu ID yangu hapa JF na kwamba hili si jukwaa pendwa la chini kabisa.
View attachment 510258 Patapata

Baadae kabisa tukaelekea Pata Pata. Hapa kweli unapata vitu. Tulienda kula, vyakula vyao vilikua kiwango haswa, baadae nikagundua muhudumu mmoja pale ni Mkenya, akaniambia nibaki pale hadi pachangamke. Alinipromise kuniunganisha na Wabongo kadhaa.

Mida ilivyoanza kukata pakaanza kujaa, aloo yani hiki kijiwe ni balaa. Kulikua na wadada wengi wa Kibongo na Wakenya wanauza. Lkn hawa walikua tofauti na wa awali, hawa walikua very professional, na quality ya juu kidogo.

Kusema kweli Wabongo wengi niliowaona hawakua na maisha ambayo wengi hutegemea. Ni huruma sana kuona wenzetu wakiwa kwenye maisha ya namna hii katika nchi za ugenini. Wengi wamekata tamaa, hawana mbele wala nyuma, wapo hopeless sana.

Mpk happ nikawa nimejiridhisha ktk utafiti wangu, sasa nikaamua niende mitaa ya Soweto, kutokana na umaarufu wa Soweto.
View attachment 510259

Soweto

Siku zote mnasikia neno 'Chaf Pozi', hii kitu ipo Soweto, na hapa ndio Chaf Pozi penyewe achana na mambo ya Bill NassView attachment 510260Chaf Pozi, Orlando Towers.
Huku sasa ndio townships, au tuseme kama uswazi. Wabongo huku nilikutana nao wengi mno, na niseme wazi wengi shughuli zao zilikua ni hizi hizi za hapa na pale. Wengi ni vinyozi, wauza mayai, wauza matunda, waziba pancha. Kuna mmoja nilipata bahati ya kuongea nae, yeye alikua anaosha magari na alikua kijiweni kwake kwenye Taxi (daladala)
View attachment 510261

Mwisho

Siwezi nikahitimisha 1 kwa 1 kuwa watu wasizamie kwenda SA, lkn nachojaribu kusema ni kuwa kila mtu mwenye plans za kutafuta maisha SA ahakikishe kuwa kila kitu kipo well sorted out hata kabla hajatoka Bongo, sio kwenda kichwa kichwa na kukutana na mambo tofauti. Hapo Johannesburg kuna kila mwafrika, Botswana, Malawi, Zambia, Kenya, Nigeria nk nk. Tena hawa wanigeria ndio hatari, hua wakiotea mchongo wanahamisha wenzao wote kutoka Lagos na Abuja. So wabongo wengi wanaishia kwenye michongo isiyoeleweka. Sijui hata wakifa hua wanazikwa wapi.

Ontario
Nilichopenda ni habari picha mpaka raha,ila poleni sana wabongo wenzangu ulioenda bila malengo SA
 
Aksante mtoa mada..yote kwa yote nitabaki hapa hapa Mwanza The RockCity nikiendesha taxi mjini huku nikilima matikiti yangu na biashara za hapa na pale bila kumuibia mtu mpaka nitoke kimaisha.ukweli maisha mazuri yapo hapa hapa Tanzania.swala ni kupambana kwa bidii tu.wako jamaa zangu watatu walienda America kwa nyakati tofauti lakini wote walikaa huko wakifanya kazi zaidi ya miaka 7 mpaka 8 na walichorudi nacho ni mikogo tu ya kutembea na kuvaa miwani za kupunguza mwanga basi.mwingine atarudi mwaka huu kama MUNGU atamjalia.maisha yapo mahala ulipo,sema tu itategemea unatafutaje na kwa bidii ipi.unaweza kukaa nje miaka mitano ukifanya kazi ya kumwagilia bustani huku mshahara wote ukiishia kwenye pango na chakula,ktk miaka hiyo mimi huku Mwanza ntakua nimevuna shamba langu la mapapai kama mala 10 hvi huku nikifunga renta ya nyumba ya pili kwa uwezo wa muumba.
I am proud to be an Tanzanian
Am proud to be AN TANZANIAN

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maisha ni popote utajiri ni popote! nje kuna watu wana hela hata ukiwaambia warudi Bongo hawakuelewi, na Bongo kuna wenye hela hawataki kusikia ! wa maisha ya kijiji!

Wewe uliyoko kijijini kaa huko huko ndo kwako, huwezi kwenda nje! na wewe wa nje kaa hukohuko tafuta hela siyo mpaka urudi Bongo! huko ndo kwako!

kila mtu na Maisha yake sasa kuna watu sijui wanaumia nini! utasikia eti! oooh! I love Tanzania, nalima Matikiti! kwani umesikia aliye eenda Nje hai- Love Tanzania? nadhani huenda kuna kitu huko nje! siyo bure ila watu wanavunja wengine mioyo ili wao ndiyo wawe juu tu!

Tuliozaliwa kijijini tulitishwa sana, kuhusu Bongo; utasikia eti Darisalame dhiki sana hakuna chakula, watu hula kitumbua kimoja na maji (chai ya rangi) kutwa nzima, ni Joto, watu wanalala nje! ugali kidogo km ngumi mwala watu Kumi! wakati huko kijijini umekula vizuri ni kauzu bila wese! Nyama , mafuta yakupikia, sukari ni starehe! chai ya maziwa, Habari , magazeti, utaviisikia tu! mleta mada acha uzwazwa!

Kumbe ilikuwa ni wivu tu, hakuna sehemu nzuri utakayo kula na kusaza km Bongo ilimradi upige kazi tu. hata kokoto Beba, Mchicha kidogo tu ukilima msimbazi hela hizooo!!! watu walitishwa sana, kufikia hata kuzomewa wakati wa safari, msione hivi jamani huko Mikoani ni shida sana. Ndiyo nayo yaona hapa leo!

Mwanza kuna wenye hali duni hasa, kati, na juu, nje pia ivo ivo! ukikaa na kuwasikiliza waosha vinywa utakesha unazunguka! kazi kwako! mwana JF! Watu wana malengo yao wengine Elimu, na wengine maisha! wengine Pesa!
 
Back
Top Bottom