Maisha haya basi tu: Nimelishwa yai la Mbuni bila kutegemea

Maisha haya basi tu: Nimelishwa yai la Mbuni bila kutegemea

Mkogoti

TAPELI Mkubwa
Joined
May 3, 2020
Posts
2,415
Reaction score
3,924
Wakuu Habari! hapa nipo mbio mbio nataka nimeze dawa za tumbo nitulie tu.

Kwa machache tu niseme tu leo Nimepatikana nimelishwa na visivyolika na bila kutegemea kwamba ntakuja kuvila.

Inshu ipo hivi nimeenda kwa jamaa yangu kumtembelea nikamkuta yupo na Kimwana wake, ile nimefika tu sijui walifikilia nini watu wale walikuwa wanataka kuniua, ghafla akaondoka kimya kimya na bila salamu kuelekea anakokujua, mi nikachuna tu sikujali wala nini nikamsalimia mwana pale nikaruka kwenye konchi kuanza kucheck movie.

Masaa kidogo namuona bibie anakuja na kibeseni cha maji ya kunawa mi nipo kimya nimejikausha ndo akanisalimia eti Mambo shem nami nikazuga poa tu, huyo kaondoka karudi na sahani kama tatu hivi harafu juu kuna chapati pembeni kuna mayai nikakaribishwa fresh tu haki ya nani yani namaliza kula ndo naambiwa unajua umekula mayai ya mbuni😳😢 basi tu niishie hapa siwezi kumalizia acha nimeze dawa za kusafisha tumbo wengine Uzungu kwetu ni mwiko ona sasa mmenilisha mayai ya mbuni na sijui kama yanaliwa.

Na kama ni sumu basi mmeniua na lengo lenu nimeshalijua.
 
Jinga wewe, kwani yanatofauti gani na ya kuku, mbuni si in ndege tu na analiwa pia kama tu kuku
 
Wakuu Habari! hapa nipo mbio mbio nataka nimeze dawa za tumbo nitulie tu.

Kwa machache tu niseme tu leo Nimepatikana nimelishwa na visivyolika na bila kutegemea kwamba ntakuja kuvila,

Inshu ipo hivi nimeenda kwa jamaa yangu kumtembelea nikamkuta yupo na Kimwana wake, ile nimefika tu sijui walifikilia nini watu wale walikuwa wanataka kuniua, ghafla akaondoka kimya kimya na bila salamu kuelekea anakokujua, mi nikachuna tu sikujali wala nini nikamsalimia mwana pale nikaruka kwenye konchi kuanza kucheck movie,

Masaa kidogo namuona bibie anakuja na kibeseni cha maji ya kunawa mi nipo kimya nimejikausha ndo akanisalimia eti Mambo shem nami nikazuga poa tu, huyo kaondoka karudi na sahani kama tatu hivi harafu juu kuna chapati pembeni kuna mayai nikakaribishwa fresh tu haki ya nani yani namaliza kula ndo naambiwa unajua umekula mayai ya mbuni[emoji15][emoji22] basi tu niishie hapa siwezi kumalizia acha nimeze dawa za kusafisha tumbo wengine Uzungu kwetu ni mwiko ona sasa mmenilisha mayai ya mbuni na sijui kama yanaliwa,

Na kama ni sumu basi mmeniua na lengo lenu nimeshalijua
Mods wanashangaza sana thread za kijinga na kitoto Kama hii wanaziacha ajabu ukituma thread yenye mafunzo kwa Jamii wanaziondoa bila hata taarifa kwa mwenyewe inauma sana mm jioni hii wamenifutia thread yangu hii

*Hii ndo hekima ya NG'OMBE pamoja na upumbavu wa KUKU.*

*Ng'ombe, akishatoa maziwa ya kulisha familia nzima, hurejea katika malisho yake taratibu. Lakini kuku, akishataga yai moja hupiga kelele ili kila mtu ajue. Je! Yai hilo alilotaga laweza kutosha hata kwa mlo wa mtu mmoja? Jibu ni hapana.*

Katika maisha kuna watu wa aina 2 kuna wale wanaofanana na Ng'ombe na wale wanaofanana na Kuku.

*Mtu afananaye na kuku akikusaidia jambo hata kama ni dogo sana atasema kila mahali ili watu wote wajue jambo hilo. Kama ni kazini/msikitini, nyumbani etc atahakikisha anajisifu sana na kuisambaza ile habari kwa wengi. Kuna watu walisaidiwa na watu hawa wenye tabia ya kuku baadaye wakaishia kuumizwa mioyo yao baada ya kusambaa kwa habari hiyo.*

*Mtu mwenye tabia ya kuku akitoa msaada hata kwenye kituo cha watoto yatima, au akisaidia maskini anatamani aje na waandishi wa habari.*

*Kuna watu wenye tabia ya ng'ombe. Akikusaidia hata kama ni jambo kubwa sana kiasi cha kushindwa kumlipa fadhila, hawezi kukusema na hataki watu wajue. Furaha yake ni kukuona unavuka salama na unafanikiwa. Watu wa namna hii hupata thawabu kubwa. Tamani kuwa na tabia kama hii ya kusaidia bila kujitafutia utukufu.*
 
Jinga wewe, kwani yanatofauti gani na ya kuku, mbuni si in ndege tu na analiwa pia kama tu kuku
Mwambie huyo mkuu watu wanakula mayai mpaka ya kilamba mwiko ye mbuni tu analia komamanga huyu asituchoshe..
 
😂 imladi hatujuani haaa haaaa Good luk
 
kaka iyo ni nyara ya serikali, ww ona raha kusimulia ujinga, utalitapika
 
Back
Top Bottom