Tatizo kubwa sana tulilonalo sisi Wanadamu ni tabia ya kumchagua Mke au Mume kwa muonekano wake wa nje.
Ukitaka kuishi maisha ya amani katika ndoa kamwe usimchague Mke au Mume kwa kuvutiwa na muonekano wake wa nje.
Anzisha mahusiano ya ndoa na mtu mnayeelewana kwa dhati bila ya kujali muonekano wake wa nje. Vigezo muhimu vya mchumba wako viwe tabia zake na siyo ukubwa wa makalio au uzuri wa umbo na sura.
Amini nakwambia mtu ni tabia, na ukioa mtu au kuolewa basi umeoa au kuolewa na hizo tabia zinazomwakilisha huyo mtu.
Ukioa mtu mwenye tabia nzuri, utaishi katika ndoa nzuri. Ukioa mwenye tabia mbaya hata kama sura yake na umbo lake ni zuri bado ndoa yako itakuwa mbaya.
Binadamu ni tabia, siyo sura wala umbo.