mwanamabadiliko
JF-Expert Member
- Oct 30, 2010
- 938
- 1,540
Tanzania na Watanzania wenzangu mmeshuhudia kwa macho yenu kwamba vitu vimepanda Bei Mara dufu hasa vinavyotoka China na ulaya, hali ya maisha imekuwa mbaya Sana, uchumi wa dunia umetetereka.
Tanzania tutegemee maisha kuwa makali zaidi, nchini China kuna shida kubwa ya umeme iliyosabishwa na upungufu wa Makaa ya Mawe katika kuendesha viwanda vingi kutokana na mgogoro baina ya Australia na China kwani ndo muuzaji mkubwa wa Makaa ya Mawe China, hivyo viwanda vingi vimefungwa, na vinavyofanya kazi vinaruhusiwa kwa masaa tu, bidhaa zetu nyingi tunaagiza kutoka China, sio sisi tu Bali ni dunia Nzima, kwahiyo vitu vitazidi kupanda Bei hasa vya Ujenzi. Pia China Wana malengo wa kupunguza matumizi ya makaa ya Mawe kwa sababu za kimazingira.
Ulaya nako kuna mgao wa umeme, kisa kikubwa ni upungufu wa Gesi asilia, na bei ya umeme imepanda Mara tatu zaidi, Sera ya kuacha matumizi ya nuclear na ubeberu wa urusi katika kutoa Gesi yake ndo sababu kubwa hivyo Mambo ni magumu.
Wengine wanasema kila mtu anatunza Nishati yaani Gesi na mafuta kwakuwa kuna vita vya kidunia vinakuja na Ili uwe vizuri lazma uwe na energy kumbuka Ujerumani na Hitler walishindwa Vita vya pili kwa sababu ya kuishiwa mafuta na gesi ya kuendesha mitambo ya Vita. Kwahiyo wamepunguza matumizi
Kutokana na hali ya mbaya huyo duniani katika sekta ya Gesi, mafuta na Makaa ya Mawe basi tutegemee wawekezaji kuja haraka kwa ajili ya Gesi, mafuta na Mambo mengine.
Kupanda vitu bei havihusiani na serikali iliyopo madarakani ni Mambo ya duniani tu huko