Maisha magumu mpaka nataka kuwa mshirikina

Maisha magumu mpaka nataka kuwa mshirikina

Naja naja

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2016
Posts
747
Reaction score
1,454
Maisha magumu sana mpaka nataka kujaribu ushirikina watu wananishauri huenda nyota yangu imefifishwa maana kila jambo linaishia njiani na kuharibika kabla halijafanyika.

Nimeshaahidiwa kazi hata humu JF na baadhi ya members lakini ghafla ukungu unaingia mtu anaingia uzito hatimaye ananipotezea.

Sielewi hatma ya maisha yangu nimepitia maduka ya dawa za kisuna nimeanza na kukoga dawa inaitwa mzizima nimeambiwa pia dawa nyingine inaitwa Msaka Uchawi ukiinywa kama ulilishwa Uchawi basi utatapika sana , nyingine nimeambiwa inaitwa Nyota inasaidia sana kupandisha Nyota , nyingine inaitwa Ufunguo na Mkumbi.

Kuna mtu anataka kunipeleka kwa mganga nikaoshwe Dawa maana si kawaida .
 
Pole Mkuu wanasema kila mtu na wakati wake, endelea kuwa na subira usichoke na kukata tamaa, endelea kuwa na tumaini na ukipata mishe ya kusukuma siku ipige kwa uaminifu, vijana wengi Maisha yetu ndo hayo hayo sema hatukati tamaa na tunaimani milango itafunguka tu.
 
Naona umeachiwa simu na baba leo, lazima jeiefu ikutambue

By the way badilisha hiyo avatar, katika ulimwengu tusiouona hiyo ndude si ya kucheza nayo
 
Pole sana Mkuu. Hakuna kitu kibaya kama mtu unakuwa na matumaini ya jambo flani then panapita ukungu mambo yanafeli! Utahisi umelogwa vile. JAPO KIUKWELI WACHAWI WANEONGEZEKA KWA KASI SANA ASEE DUUH!
 
Kama upo Dar, karibu kuwa unatembelea Twiga cement, Wazo hill,wakati wa asubuh saa 1, wafanyakazi wanapoingia au saa 11 jioni wanapokuwa wanatoka, kazi nyingi za pale zinafanywa na makampuni/contactors, Twiga huwa wanasub contract kwa kampuni zingine shughuri nyingi za kiufundi.

Uliza, chukua contacts unaweza ukajipatia ajira.
 
Ety mtu maisha magumu, anaenda kwa mganga analipia na huduma ya mganga. Serious ?
 
Back
Top Bottom