Maisha magumu mpaka nataka kuwa mshirikina

Maisha magumu mpaka nataka kuwa mshirikina

We mbona hapo bado yaani ndio unataka kua mshirikina wakati wenzako wapo digrii yatatu
 
Maisha magumu sana mpaka nataka kujaribu ushirikina watu wananishauri huenda nyota yangu imefifishwa maana kila jambo linaishia njiani na kuharibika kabla halijafanyika....
Kwa akili ya kwenda kwa waganga, lazima upigwe tu. Maana hamna jinsi.

Mganga anakufanya fursa bila ya kukusaidia kitu.
 
Pole mkuu kwa changamoto ila kama upo Dar ,jitahidi uende mikocheni industrial area ukaulize mishe wakati ukisubiri kupata white collar job.
Jamaa ebu toa ufafanuzi kidogo hapo mikocheni industrial area kuna fursa gani utakua umetusaidia wengi
 
Mkulungwa nisikilize mimi nakupa ushauri.
Nenda kwanza kasafishwe nyota,ukitoa nuksi mwili ukakaa sawa kila kitu kitakua mundele.

Achana na watu wa mitandao wanatabia ya kuigiza,wanajifanyaga awamo kumbe ndo wenyewe walio kubuhu.
 
uchawi upo na unafanya kazi mzee, km unaamini uwepo wa Mungu basi mshikilie sana, km hujawahi kufunga basi fanya hivyo na uombe kwa dhati na utafunguliwa.

waganga saa zingine wanashirikianaga na wachawi.
 
Jamaa ebu toa ufafanuzi kidogo hapo mikocheni industrial area kuna fursa gani utakua umetusaidia wengi

Kuna viwanda vingi sana mkuu,kama ukienda kutafuta DEIWAKA hauwezi kukosa mkuu ingawa mpunga wake sio mkubwa kivile wanalipa kwa DAY.
 
😂😂😂😂Usipotia akili kichwani hao waganga wa kienyeji watakufilisi.
Maisha magumu sana mpaka nataka kujaribu ushirikina watu wananishauri huenda nyota yangu imefifishwa maana kila jambo linaishia njiani na kuharibika kabla halijafanyika...
 
Maisha magumu sana mpaka nataka kujaribu ushirikina watu wananishauri huenda nyota yangu imefifishwa maana kila jambo linaishia njiani na kuharibika kabla halijafanyika...
Tatizo watanzania tulizoea kuishi kiujanja ujanja Ndio maana tunaumia.

Tii sheria bila shuruti.

Lipa kodi.

Utafaidi matunda ya awamu hii ya Rais mwema mwenye Moyo wa huruma na upendo kwa RAIA wake.

Vinginevyo utaumia sana maana mianya ya wapiga dili imeziba kabisa
 
Mikocheni Industrial area - Shuka kituo cha ITV kuanzia pale kuna viwanda vingi sana vya DEIWAKA.
.. Mkuu, kama hutajali tunaomba ufafanuzi zaidi hapa. Utakuwa umesaidia vijana wetu wengi.
Issue inakuwaje ili kuipata hiyo deiwaka??
 
Back
Top Bottom