Maisha magumu sana ila nina imani ipo siku nitafanikiwa

Maisha magumu sana ila nina imani ipo siku nitafanikiwa

Ya
Maisha yanazidi kunichachia kila kukicha, nimetafuta sana kazi bila mafanikio yoyote mpaka ninahisi nimerogwa.

Mtaani thamani yangu imeshuka mno maaana nilipiga hatua kidogo ya kielimu ila nikakosa mtu wa kuniendeleza baada ya kufiwa na mama (baba yupo ila ni baba jina) hivyo nikakata tamaa ya kuandika barua ya ku-postpone maana nilishawahi ku-postpone lakini mambo hayakwenda vizuri hivyo nikaamua kuacha chuo.

Kwa sasa nahitaji angalau kupata kazi niingize japo elfu 7 kwa siku.

Mawazo ya kujiua yananiandama mara kwa mara ila ninapingana nayo kiume. Nina imani ipo siku nitafanikiwa.
Tatizo watanzania tulizoea kuishi kiujanja ujanja Ndio maana tunaumia
Tii sheria bila shuruti
Lipa kodi
Utafaidi matunda ya awamu hii ya Rais mwema mwenye Moyo wa huruma na upendo kwa RAIA wake
Vinginevyo utaumia sana maana mianya ya wapiga dili imeziba kabisa
 
Kule kila kitu unapewa bure ni wewe Tu na mguu na njia a utakula vinono vya watu mpak ukimbie kwenye dini kuna hela kinyama
Dini inalipa sana Mimi mwenyewe nataka nifungue kanisa hata kama ni la mbao kama banda haina noma naanza mdogodogo.
 
Nenda Kwa wasabato kajiunge na uinjilist wa vitabu upate mtaji ukomae mtaa , miez miwili ni mingi ukikomaa unakuwa na one mill up to 2millio.. ila uwe mcheshi, mchangamfu , mtu wa kuombea watu na biblia ujue kuifunua funua.....Acha ujinga wa kutaka kujiua
Kwa hiyo wasabato ni milionea?
 
Maisha yanazidi kunichachia kila kukicha, nimetafuta sana kazi bila mafanikio yoyote mpaka ninahisi nimerogwa.

Mtaani thamani yangu imeshuka mno maaana nilipiga hatua kidogo ya kielimu ila nikakosa mtu wa kuniendeleza baada ya kufiwa na mama (baba yupo ila ni baba jina) hivyo nikakata tamaa ya kuandika barua ya ku-postpone maana nilishawahi ku-postpone lakini mambo hayakwenda vizuri hivyo nikaamua kuacha chuo.

Kwa sasa nahitaji angalau kupata kazi niingize japo elfu 7 kwa siku.

Mawazo ya kujiua yananiandama mara kwa mara ila ninapingana nayo kiume. Nina imani ipo siku nitafanikiwa.
Usikate tamaa katika haya maisha hata siku moja, jaribu kila unachohisi kinaweza kukutoa utafanikiwa, cha msingi ni kumtanguliza Mungu.
 
Usikate tamas boss. Pambania kombe mpka kieleweke aliekupa mdomo anajua atakulisha vipi na utakula nini.

Pambania kombe boss hauko peke yako tuko wengi tunao taabika. Ila hatukati tamaa.

Tunaamini the sun will shine one day.

Do your best but don't lose yourself.

Sikiliza nyimbo ya John drille- sun will shine.
 
Buku Saba njoo hapa Lumumba utapata, una uandishi mzuri nitakukonekti na Bashiru.
 
Kule kila kitu unapewa bure ni wewe Tu na mguu na njia na utakula vinono vya watu mpak ukimbie kwenye dini kuna hela kinyama

Kama nakuelewa hivi, huwa nawaza kujiunga na dini zenye fursa hasa taaluma yangu. Ukijiweka vizuri ni rahisi kula vinono.

Japo sijui vema kuhusu huo uinjilisti, lakini nimeelewa nukta yako.

Kitu pekee kitachonipeleka kanisani, ni mke ili nifunge ndoa, na fursa kwenye taasisi hizo.
 
Kwanza acha kumdharau baba yako. Hujui amaepitia mangapi mpaka hapo alipo au kama ni makusudi piga kimya sio mpaka ututangazie jf "baba jina".

Anyway una ujuzi gani*?
 
Pole Sana. Usikate tamaa, endelea kuomba na kutafuta vibarua. Mungu akakupe kibali.
 
Siku moja nilienda Temeke hospital nikiwa hoi nachechemea mguu. Baada ya kwenda kwenye sehemu ya foleni kumuona daktari niliacha mara moja kuchechemea. Maana nilikutana na watu wenye vyuma miguuni,Miguu imevimba,wamekatika miguu. Wengine bodaboda wanaletwa naona. Bila kwenda kumuona daktari nilijikuta natembea vizuri wala sisikii maumivu. Na nilirudi home kabisa maana niliona mimi siumwi natania/nadeka.

Huku kuna padri anapenda kusema ukiona umejisahau au umekata tamaa nenda Hospital ya Mount Meru Wodi namba sita. Utakachokiona utajifunza. Ni Wodi ya Wagonjwa wa TB na Kansa.

So my point is pinned to the fact that..No matter what you're going through Never loose focus and never give up. Jitahidi kufurahi na ulichonacho. Kidogo hicho kinachokuliza kuna mtu anakitamani hakipati. Kuna mtu anatamani hata angeweza kupost uzi kama ww ulivyoweza ila kashindwa. Afya yako uliyonayo hapo ni mafanikio makubwa sana kwako maana Maisha ni Afya na sio pesa.

Kila siku Ukiamka asubuhi ukavuta pumzi ikaingia na kutoka mpaka jioni bila msaada wala shida yoyote basi wewe ni moja ya matajiri wakubwa waliopo duniani. Najua hutanielewa na kuniona mbabaishaji/Machi noo ila ndio ukweli maana tumezoea kuyapima mafanikio kwa vile vitu vinavyoweza shikika (Material things).

Embrace what you have.. Happily
Kumbe nna muda mrefu sijaingia Jamii forum.. dogo umemature sana tu.
 
Bony Mwaitege anasema MAISHA NI FOLENI KILA SIKU YANASOGEA, MWAMINI MUNGU IPO SIKU UTAFANIKIWA...
Hold on mkuu nothing is easy and yet nothing is impossible.
 
Back
Top Bottom