Siku moja nilienda Temeke hospital nikiwa hoi nachechemea mguu. Baada ya kwenda kwenye sehemu ya foleni kumuona daktari niliacha mara moja kuchechemea. Maana nilikutana na watu wenye vyuma miguuni,Miguu imevimba,wamekatika miguu. Wengine bodaboda wanaletwa naona. Bila kwenda kumuona daktari nilijikuta natembea vizuri wala sisikii maumivu. Na nilirudi home kabisa maana niliona mimi siumwi natania/nadeka.
Huku kuna padri anapenda kusema ukiona umejisahau au umekata tamaa nenda Hospital ya Mount Meru Wodi namba sita. Utakachokiona utajifunza. Ni Wodi ya Wagonjwa wa TB na Kansa.
So my point is pinned to the fact that..No matter what you're going through Never loose focus and never give up. Jitahidi kufurahi na ulichonacho. Kidogo hicho kinachokuliza kuna mtu anakitamani hakipati. Kuna mtu anatamani hata angeweza kupost uzi kama ww ulivyoweza ila kashindwa. Afya yako uliyonayo hapo ni mafanikio makubwa sana kwako maana Maisha ni Afya na sio pesa.
Kila siku Ukiamka asubuhi ukavuta pumzi ikaingia na kutoka mpaka jioni bila msaada wala shida yoyote basi wewe ni moja ya matajiri wakubwa waliopo duniani. Najua hutanielewa na kuniona mbabaishaji/Machi noo ila ndio ukweli maana tumezoea kuyapima mafanikio kwa vile vitu vinavyoweza shikika (Material things).
Embrace what you have.. Happily